Baada ya Mwl. Mussa Iddy kulalamika, HESLB yatoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa urejeshaji mikopo

Baada ya Mwl. Mussa Iddy kulalamika, HESLB yatoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa urejeshaji mikopo

Kwa nini retation fee ina fichwa fichwa toka watunge sheria 2016 huu mwaka wa tano sasa ndio mnajitokeza kutoa ufafanuzi je mkiitwe nyie ni WEZI mtakataa
Juza raisi magufuli alipokua chato alimuomba waziri mkuu wa china nchi yao isamehe madeni wanayoida serikali ya tanzania je mki isamehe hiyo retation fee kwa wanufaika wa mikopo kuna kosa gani
Kuwa na portal na mifumo ni bla bla kubalini mmeshakosea kwa hiyo msituvuruge
HESLB sio TRA nyie ni bodi ya mikopo elimu inatakiwa itolewe mapema kabla ya kuanza kuleta porojo
 
Dawa ya deni ni kulipa na si vinginevyo
Kwa hili nipo upande wa raia. Unakusanya kodi kupitia mshahara wa mwananchi ili umuhudumie, unamuhudumia kwa kumpa mkopo mwanae asome, mwanae akimaliza anarudisha na fee endapo atachelewa. Ila ukichelewa kumlipa mshahara yeye au mafao ya mzazi wake hakuna fee anayokuchaji. Serikali yetu ipambane pia na haya mambo yanayomgusa mtu wa chini moja kwa moja.
 
Kwa wale waliomaliza mkopo na wakia amini hamdaiwi tena jeumelipokeaje hili suala?
Kwa wale ambao hajabahatika kupata uhakika wa ajira na miaka ina zidi kusonga hii rentation fee una zungumziaje?
Kws wale ambao mmeshafikisha 40's na bado hujamaliza deni je unadhani kuna usahihi wowote ?
HESLB NI KITANZI CHA MAISHA
 
Sijaona majibu yeyote ya maana kutoka loan board zaidi ya kumtisha iddy tu na kutuaminisha eti iddy ameelewa na atakuwa balozi....ameelewa nini kwenye yale malalamiko yake? Retention fees ndio kitu gani? kwani ule mkpo ni biashara? Nimrodi Mkono alituanzishia janga la kitaifa.
Si ajabu Mwalimu Idd kafutiwa deni mazima ohooo [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kama ulisoma zile maudhui zinazo trend kuhusu hii bodi, hakuna ufafanuzi weowote uliotolewa. Waingereza wanasema "The author was beating about the bush"
 
Umewaepukaje?
Jina nililokuwa natumia chuo sio hili nalotumia sasa, yaani yote yamebadilika..pia sipo kwenye ajira rasmi.
Halafu cha kushangaza nilishawahi kuangalia kama jina langu lipo kwenye list ya wadaiwa sikuliona, sisi tulikuwa wa mwanzo kupata mkopo enzi hizo 2004..ilikuwa simple sikumbuki kama nilijaza form..tuliandika majina, course unayosoma na account namba..baada ya wiki mbili mkopo ukaingia..

Hadi namaliza sikumbuki kujaza form yoyote. Nimehisi labda hawakuweka details vzr kwenye system. Sijawahi wauliza wenzangu kama wao wanadaiwa au la...
 
Guys, don't fools us around. Stop going around the bush.....tell us here in naked truth why salary slip shows 47+billion loan amount due? Why? Mnasema kinachoonekana kwenye loan statement

Ninayo, sijaajiriwa. Natumia TIN ya mama yangu na biashara zinasoma zake yeye. Wananipata wapi?

Vipi ukitaka Passport ya kusafiria 😎😎

Yaaani NIN ndo kiboko na mwisho wake yote

Siku isiyo na jina watakupata tu hata akaunti zako za benki watapita nazo. Ombea Mungu uendelee kutumia hadi akaunti za mama milele. Hawa jamaa hawataki mchezo saivi
.
NIN= Namba ya Utambulisho ya Taifa
 
Mbona mi nimeandika nafuga kuku Vikindu, Mkuranga. Naishi Kijichi DSM na barua ya serikali ya mtaa nimeambatanisha.

Serikali yenyewe ipo wapi ya kumtafuta kila mdaiwa door to door ? Hii hii ya CCM?
Huna akaunti ya benki?
 
Baada ya Mwl. Iddy wa Geita kufichua uonevu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Hatimaye Bodi wameamua watoke hadharani tena ni Jumapili [emoji116][emoji116][emoji116]...]
hamna ufafanuzi hapo,porojo tu
 
Mie yaani hata sijawaelewa bado.....wakitaka twende sawa inabidi na madeni yote ambayo serikali inadaiwa yaani yale sugu nayo yawe na value retention fee....vinginevyo huu bado ni unyonyaji na uonevu wa hali ya juu[emoji34][emoji34][emoji34][emoji34][emoji34]
Kuna watumishi wanadai nauli za likizo za mwaka 2014, wakilipwa madeni wanalipwa fedha ileile hiyo value retention fee ni ya upande mmoja?
Magufuli nchi imekushinda.
 
Back
Top Bottom