kipozi
JF-Expert Member
- Jan 23, 2015
- 1,315
- 1,702
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio mkuu toka jamaa alivyo kamatwa sikuvuta tena hadi sasaMkuu vipi bangi umeacha kuvuta now.?
Aisee! Pole sana kamanda.Baada ya kufuta lile tope mdogo mdogo nikaanza kupandisha kimpando cha kuelekea kwa babu nikafika pale nikazuga kama nimeenda kuomba ganja akaanza kusema asubuhi yote umekuja kufanya nini nikamwambia nimekuja kufata dawa.
Akaniambia yamebaki makapi , kisha akaniuliza yule mwenzako agustino mzigo amesha leta nikasema hapana.
Ikabidi aingie ndani aniletee yaleyale makapi
Nilitoka pale kwa babu nikijua agustino hakuuza mtu yoyote kwa polisi basi nikaanza kutembea kurudi shuleni kwa yale mavazi nilishindwa nitarudi vipi ikabidi nitafute sehemu nikae nitulie nione jinsi gani nitatunga hoja .
Nilikaa mahali nikawaza agustino hana ndugu mahali pale nikasema nitafanyaje niende hata kumuona kituoni nikakosa jibu maana na mimi nilikuwa na hofia usalama wangu nilimpigia tena ndugu yake yule nikamwambia awaambie wazazi wake hata na yeye pia aje kumuona maana haikuwa mbali sana
Nilimwambia pia aje niwaoneshe getto ikiwezekana wachukue vitu vyake vya muhimu wa mtunzie jamaa aliniambia yeye anatangulia kashamwambia baba yake atakuja kesho
Basi alivyofika nilienda kumpokea pale centre tukaenda hadi getto jamaa akajitambulisha kuwa nikakaake tukavunja kufuli tumeingia ndani tafuta vitu muhimu kama simu, kadi ya banki,walet vyote hakuna na baadhi ya vitu vingine sivikumbuki
Basi yule kaka yake japo wakuvuta na kamba kesho yake akasema nije nimpeleke kituoni tumpelekee msosi mimi nilikubali ila nikamwambia nitabaki mbali kabisa usikie maafande watakwambiaje.
Kweli kesho yake nilivunja vipindi nikamsindikiza Yule jamaa alivyorudi akaniambia walimuoji ikabidi awaambie yeye ni kaka yake alitokea wilaya nyingine kuja kumletea msosi, Jamaa aliulizia kama anaweza muwekea dhamana ya pale kituoni maafande walikataa wakasema tena jarada lake linapelekwa mahakama ya wilaya
Daa jamaa alichoka tulirudi nae hadi getto kesho yake tena tukaenda kumuona na yule jamaa ndio nikajua kweli bongo nyoso yani hawakupi nafasi ya kuongea na mtu ukishapeleka msosi unaonja askari wanachukua unatembea mbele huwezi ongea hata siri na mtuumiwa , Halafu kituoni kumbe hawapiki sasa nikawa najiuliza hivi waliokamatwa na hawana ndugu karibu huwa wanakula nini kabla hawajapelekwa magereza
Kiufupi agustino kesi yake ilipelekwa mahakama ya wilaya, tena alishitakiwa na jamuhuri kwa kosa la kukamatwa na zaidi ya kili 100 za bangi tena alikamatwa na ushahidi kabisa boda boda wake kwa kujitetea ikabidi amchomee kabisa alisimama kama shahidi wa mwisho
Kulingana na mapambano ya bangi kipindi kile bila huruma hakimu alimtundika miaka 30 jela. Nimechoka kutype
Oky ngoja niendelee nakumbuka siku ya mwisho nimeenda kumuona pale magereza nikiwa nimeshika mkate na vipande vya sabuni + wembe nikajua labda kidogo kule magereza kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuongea na mfungwa asee kufika tuliruhusiwa raia kama 20 hivi kwa mkupuo eti tuongee na wafungwa wetu kwa zile kelele sikuweza kumsikia vizuri neno nililolisikia kutoka kwake ni MWANANGU ENDELEA KUKOMAA
Na hapo nilikuwa nimetoka shuleni wilaya nyingine wakati natoka kwenye lile gereza nilijisikua huzuni sana kiasi kwamba nilijikuta na bubujikwa na machozi baada kama ya mwaka na nusu kupita nikiwa chuoni niliongea na yule kaka yake akaniambia agustino alihamishwa butimba mwanza
Kunakipindi niliona magufuli ameenda pale niliangaika sana kumtafuta agustino kwenye zile camera lakini sikufanikiwa kumuona rafiki yangu kipenzi now kamanda agustino amemaliza miaka 5 gerezani. kwa kifungo cha miaka 30 kwa jinsi wanavyo hesabu amebakiza miaka 15 gerezan
Mimi bado nikijana sana mwaka huu mwezi fulani na fikisha 24 yrs damu bado inachemka naendelea kupambana rafiki yangu mpambanaji agustino, kufa na kupona, kwa hali na mali nijipanue kiuchumii ili siku ukitoka gerezani husije kunicheka eti nilikuwa napoteza muda kitaa
Nataka uje unikute nimesha tengeneza bara bara nzuri ya kiuchumi uje tuishi maisha ya kidoni kama zilivyokuwa ndoto zako.
Nilichojifunza urafiki bora haupimwi kwa muda unapimwa kwa matendo maana niliishi na agustino katika kipindi kifupi sana lakini ameacha historia kubwa sana ndani ya maisha yangu
Nineandika kwa haraka vibaya vibaya kama kutakuwa na makosa tusameeane
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo baada ya nyungu mambo yanakua kitonga?Nyungu nishafanya sana hii maamuzi ni yako uachwe na boxer au uivue......
Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera sana mkuu... Kweli ulipambanaMkuu nilipambana sana semaa kilicho niokoa kwenye yale masomo 3 nilikuwa naelewa sana sana economics na geography toka Olevo maana nilisoma masomo ya biashara
Advanced maths ilinipeleka ila nilipambana nayo vibaya sana
Degree yangu ya kwanza nimemaliza mwaka jana Udsm conas Actuarial science
Sent using Jamii Forums mobile app
Una Moyo... Mimi hapo nishampa Kitusi.Unajua mkuu, ukiwa unaandika story ni kama uko kwenye chumba cha mtihani unashirikisha ubongo, macho pamoja na mikono
Soo kilichokuwa kunatoka kwenye ubongo ndio nilichokuwa naandika
Sorry kama huo uandishi umekukwaza
Sent using Jamii Forums mobile app
Am here baby, saizi nko mita 300 chini ya ardhi naisaka dhahabuAugustino babe popote ulipo wewe ni mwanaume [emoji8][emoji8][emoji8]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]komaaa tu mkuuu kuuza bangi utatoboa wala usiwaze kudakwa
Pia nawe asante kwa kushukuruNimefuatilia Story na comments.
Mazuri niliyochota hapa hayaelezeki...
Ahsanteni nyote kwa kushea na kushiriki ipasavyo.
jooohs umetisha sana
Baada ya kufuta lile tope mdogo mdogo nikaanza kupandisha kimpando cha kuelekea kwa babu nikafika pale nikazuga kama nimeenda kuomba ganja akaanza kusema asubuhi yote umekuja kufanya nini nikamwambia nimekuja kufata dawa.
Akaniambia yamebaki makapi , kisha akaniuliza yule mwenzako agustino mzigo amesha leta nikasema hapana.
Ikabidi aingie ndani aniletee yaleyale makapi
Nilitoka pale kwa babu nikijua agustino hakuuza mtu yoyote kwa polisi basi nikaanza kutembea kurudi shuleni kwa yale mavazi nilishindwa nitarudi vipi ikabidi nitafute sehemu nikae nitulie nione jinsi gani nitatunga hoja .
Nilikaa mahali nikawaza agustino hana ndugu mahali pale nikasema nitafanyaje niende hata kumuona kituoni nikakosa jibu maana na mimi nilikuwa na hofia usalama wangu nilimpigia tena ndugu yake yule nikamwambia awaambie wazazi wake hata na yeye pia aje kumuona maana haikuwa mbali sana
Nilimwambia pia aje niwaoneshe getto ikiwezekana wachukue vitu vyake vya muhimu wa mtunzie jamaa aliniambia yeye anatangulia kashamwambia baba yake atakuja kesho
Basi alivyofika nilienda kumpokea pale centre tukaenda hadi getto jamaa akajitambulisha kuwa nikakaake tukavunja kufuli tumeingia ndani tafuta vitu muhimu kama simu, kadi ya banki,walet vyote hakuna na baadhi ya vitu vingine sivikumbuki
Basi yule kaka yake japo wakuvuta na kamba kesho yake akasema nije nimpeleke kituoni tumpelekee msosi mimi nilikubali ila nikamwambia nitabaki mbali kabisa usikie maafande watakwambiaje.
Kweli kesho yake nilivunja vipindi nikamsindikiza Yule jamaa alivyorudi akaniambia walimuoji ikabidi awaambie yeye ni kaka yake alitokea wilaya nyingine kuja kumletea msosi, Jamaa aliulizia kama anaweza muwekea dhamana ya pale kituoni maafande walikataa wakasema tena jarada lake linapelekwa mahakama ya wilaya
Daa jamaa alichoka tulirudi nae hadi getto kesho yake tena tukaenda kumuona na yule jamaa ndio nikajua kweli bongo nyoso yani hawakupi nafasi ya kuongea na mtu ukishapeleka msosi unaonja askari wanachukua unatembea mbele huwezi ongea hata siri na mtuumiwa , Halafu kituoni kumbe hawapiki sasa nikawa najiuliza hivi waliokamatwa na hawana ndugu karibu huwa wanakula nini kabla hawajapelekwa magereza
Kiufupi agustino kesi yake ilipelekwa mahakama ya wilaya, tena alishitakiwa na jamuhuri kwa kosa la kukamatwa na zaidi ya kili 100 za bangi tena alikamatwa na ushahidi kabisa boda boda wake kwa kujitetea ikabidi amchomee kabisa alisimama kama shahidi wa mwisho
Kulingana na mapambano ya bangi kipindi kile bila huruma hakimu alimtundika miaka 30 jela. Nimechoka kutype
Oky ngoja niendelee nakumbuka siku ya mwisho nimeenda kumuona pale magereza nikiwa nimeshika mkate na vipande vya sabuni + wembe nikajua labda kidogo kule magereza kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuongea na mfungwa asee kufika tuliruhusiwa raia kama 20 hivi kwa mkupuo eti tuongee na wafungwa wetu kwa zile kelele sikuweza kumsikia vizuri neno nililolisikia kutoka kwake ni MWANANGU ENDELEA KUKOMAA
Na hapo nilikuwa nimetoka shuleni wilaya nyingine wakati natoka kwenye lile gereza nilijisikua huzuni sana kiasi kwamba nilijikuta na bubujikwa na machozi baada kama ya mwaka na nusu kupita nikiwa chuoni niliongea na yule kaka yake akaniambia agustino alihamishwa butimba mwanza
Kunakipindi niliona magufuli ameenda pale niliangaika sana kumtafuta agustino kwenye zile camera lakini sikufanikiwa kumuona rafiki yangu kipenzi now kamanda agustino amemaliza miaka 5 gerezani. kwa kifungo cha miaka 30 kwa jinsi wanavyo hesabu amebakiza miaka 15 gerezan
Mimi bado nikijana sana mwaka huu mwezi fulani na fikisha 24 yrs damu bado inachemka naendelea kupambana rafiki yangu mpambanaji agustino, kufa na kupona, kwa hali na mali nijipanue kiuchumii ili siku ukitoka gerezani husije kunicheka eti nilikuwa napoteza muda kitaa
Nataka uje unikute nimesha tengeneza bara bara nzuri ya kiuchumi uje tuishi maisha ya kidoni kama zilivyokuwa ndoto zako.
Nilichojifunza urafiki bora haupimwi kwa muda unapimwa kwa matendo maana niliishi na agustino katika kipindi kifupi sana lakini ameacha historia kubwa sana ndani ya maisha yangu
Nineandika kwa haraka vibaya vibaya kama kutakuwa na makosa tusameeane
Sent using Jamii Forums mobile app
Thanks alot for your inspiration words Paula PaulWhy am I tearing up reading that. Jooohs, you have a lot of emotional maturity. As they say, maturity comes with experience not age.
Wewe ni rafiki wa kweli unajua maana ya urafiki wa kweli. Najua hata rafiki yako huko alipo anajua wewe ni rafiki wa kweli.
I sincerely hope you'd be able to keep that fire and enthusiasm.
Thank you for sharing that. Xoxo.
Shukrani mkuuDah! Hii story n tamu
Inafurahisha na inasikitisha, Agu ni rafiki yako wa kweli fanya uwezavyo angalau uwakumbuke wazazi wake
Pili kama alivyokusihi kwamba ENDELEA KUPAMBANA, hii kauli ifanyie kazi ili hata akitoka jela uweze kumpiga tafu.
Big up sana Jooohs, wewe ni mpambamaji haswa
Kweli mungu atajaaliaNimesikitika mno mwishonii[emoji24], jooohs aendelee kupambana kama rafiki yake alivyomshauri ipo siku atafanikiwa na kuwa na maisha waliyoyatamanii.!!
Ndio hivyo mkuu upendo ndio kila kituNimependa hitimishi mkuu huo ndio upendo tulioumbiwa binadamu
Nimechoka kutype imebidi nipige bla bla tumalize maana kunawatu walikuwa wanatamani wanipige ngumi kisa muendelezo
Sent using Jamii Forums mobile app
Millions 3 [emoji23][emoji23][emoji23] hii ndio alikuwa anazungushia biashara way back . Nashani hadi anatakoa itakuwa pesa ya kawaida sanaMwanangu jooohs jitahidi upambane kiasi kwamba agustino akija kutoka gerezani umpe mtaji japo wa 3m ajiendeleze atimize malengo yake.
Pili jitahidi uwe unaenda kumuona japo kila mwaka na umwambie kabisa kuwa unaendelea KUKOMAA Kama alivyokuasa kuwa MWANANGU ENDELEA KUKOMAA na kwamba siku akitoka una zawadi yake ( mtaji ) , hii itampa nguvu Sana jamaa huko gerezani
WANA JAMII FORUMS, TUSIFANYE MAKOSA TENA OCT 2020