Baada ya Ole Nasha kufariki ni wakati wa Mkataba wa bandari ya Bagamoyo kuwa wazi

Umeweka vizuri. Lakini Je, comparison analysis imefanyika kati ya kupanua bandari ya DSM hata kwa kulipa fidia na bandari kuendeleza operation bila masharti dhidi ya kujenga bandari mpya?
Mimi sikubaliani kujengwa kwa mradi mkubwa kiasi hicho huku tukiwa tumetofautiana na kugawanyika pakubwa kama nchi juu ya mradi wenyewe. Tawala huja na kuondoka na kuja tawala zingine. Nchi isifanyiwe majaribio ya do and undo kila wakati.
 
Mkuu, 'midimay', naheshimu kutokubaliana kwetu, mradi tukiwa tumeelewa vya kutosha tunaposimamia.

Uwezekano wa kupanua bandari ya Dar es Salaam kuwa na uwezo mpana kuhimili matakwa ya mahitaji makubwa miaka michache tu ijayo (weka 10 hadi 15), uwezekano huo haupo kwa mazingira iliyonayo Dar es Salaam. Unazungumzia fidia? Ufidie majumba na makazi ya watu katikati ya mji ili ujenge bandari? Hii itakuwa gharama kubwa sana.
Na siyo hivyo tu, wewe fikiria mazingira ya bandari yenyewe, na lango la kuingilia meli kubwa. Utaanza kuchimba mtaro kama wa Suez canal?

Swala la "kutofautiana" kama umenielewa katika niliyoandika hapo juu siyo swala kubwa sana tukiondoa hawa wenye kundi la u'upigaji' waliopo nyuma ya mradi huo, ambao ndio wengi tunawapinga kuhusiana na mradi wenyewe.
Bandari ya Bagamoyo ikijengwa kama mradi wetu, wa nchi ya Tanzania sioni kutofautiana sana kati yetu zaidi tu ya namna ya utekelezaji wake na gharama zitakazohusika. Vinginevyo sioni pingamizi juu ya mradi huo wenye manufaa makubwa kwa nchi yetu.

Nikisoma mistari yako miwili ya mwisho, naona kuwa hatupingani kati yako na mimi, ila nadhani ni kutoelewana tu katika uwasilishaji wa hoja zetu.
"Kutofautiana" unakokuandika hapa nielewavyo ni huko huko ambako nami sikukubali, kwa sababu ya kutaka ujenzi ufanyike kunufaisha genge la watu. Hata mimi huko sikupendi kabisa.

"...nchi isifanywe majaribio..."; hata mimi sipendi iwe hivyo. Kama ninakuelewa "majaribio" unayoyalenga ni kama mpango huo unaosukumwa na genge kujenga bandari kwa kutumia njia za kujinufaisha, badala ya kulenga mahitaji ya nchi. Mimi mradi huu wa Bagamoyo, au Mwambani Tanga, naipenda, kwa sababu najua uhitaji utakuwepo.
 


Hujajibu maswali muhimu

1. Bandari ya Dar itaendelea kupata mizigo kutoka China?
2. China na miradi yao ya shaba Zambia Je kuna mtu anafikiria watapitisha bandari yetu ya Dar
3. Je watarudisha vipi $10B ya ujenzi kama Bandari ya Dar bado iko wazi na inakuwa?.
 
Ni wazi TZ tunaelekea kubaya manung'uniko yamekuwa mengi dhidi ya baadhi ya watu...watu wanna chuki mno na hili kundi la watu wachache...ngoja tuone mwisho wake...malalamiko ni mengi mno..
 


P, Mradi wa treni umuhimu wake kila mtu anajua na tumekuwa makini sana na kutumia pesa zetu. Bandari ni tatizo. Kwanini tusikuze bandari ya Tanga wakati tayari kuna mafuta pale au Tanga nayo imejaa!!. Tanga sio mbali sana kama kweli hii bandari ni strategic ingekuwa Tanga na sio Dar. Lakini ukweli ni kwamba hii bandari haitakuwa chini ya bandari zetu sisi ni wadau tu na hii mimi sikubaliani nayo. Mimi sikubaliani na Tanzania kutoa bandari kama kwa nchi nyingine. Uendeshaji wa bandari sitashauri apewe nchi tena tujue China kampuni haziko huru zinaendeshwa kisiasa. China kwa wenyewe hii sio bandari ambayo wanategemea faida bali ni kuweka supply chain yao vizuri tu. Treni , ndege na mradi wa stigler ni wetu huu mradi hautakuwa wetu. Na ndiyo maana ni muhimu kuweka mkataba wazi. Je kuna siri gani kubwa za kuficha zaidi ya umiliki na kwanini wafiche. P mimi nashughulikia mikataba kazini najua kampuni zinavyojua kuiba.

Haya maswali sio kwa P pekee ni ya kujiuliza tu.

1. Na hapa ndiyo tunapishana maana mkataba hauko wazi bandari itakuwa ya nani?
2. Je $10B ni mkopo au ni wezezaji kama Mo wa Simba?
3. Je tunawamilikisha wachina uendeshaji wa bandari Je uendeshaji ukiwa mbovu tutafanyaje? tunaweza kufukuza management na kuweka nyingine kama hao CEO wengine au?
4. Vitu gani ambavyo hatutaruhusu China wafanye? mfano meli ya kijeshi ya USA itaruhusiwa kupiga nanga kwenye bandari hii kama wamekuja kufanya shughuli za kijeshi na JWTZ?
5. Wanasema wanajenga viwanda tunaomba list ya viwanda ambavyo wanavijenga na ni kiasia gani cha $10B ni viwanda? au watakuwa wanauza viwanja kwa wawekezaji wengine . Hapa tusipokuwa makini patajegwa magodown tu!
6. Kwenye matumizi na uhakiki wa ujenzi ni kampuni gani ina hakiki gharama za ujenzi? Nani anaiteua hii kampuni Tanzania au China?
7. Je ni vifaa gani vya ujenzi kama chuma, cement ..... vitatoka tanzania?
 
Tupo pamoja. Nikiri kwamba nimekuelewa. Natamani kila mtu hapa akuelewe kama nilivyokuelewa. Nikisema kidogo niling'amua ni juu ya "mode of action" au "mode of delivery". Umeweka wazi kabisa kwamba tunahitaji bandari kubwa kama tulivyowahi kuambiwa na tunavyoendelea kuaminishwa juu ya hiyo ya Bagamoyo. hapo hatupingani. Ninachopinga ni hiyo hiyo unachopinga na wewe. Bandari isijengwe pale kwa sababu tu ya maslahi ya kikundi fulani cha watu na wala isijengwe kwa mashinikizo ya nchi fulani. Kama hii nchi sio "Jamhuri ya Ndizi", basi idhihirike katika hili swala kubwa la Bandari.
 
8. What is the role of(nini nafasi ya) Oman katika huu mkataba wa ujenzi wa bandari? Niliwahi kuona mahali akitajwa kama financier wa mradi. Na hapo pia kama financier huzaa maswali lukuki ya kujiuliza.
 
Kwa uandishi huu unaweza ukawekewa mkataba mezani na ukatoka patupu usielewe mkataba unasemaje!
 
nakumbuka JPM aliwai sema mkataba unachodai ni kwamba kwa hio miaka 99,

Tz hatutaruhusiwa kukusanya kodi wala kudai chochote kwenye Bandari hio,

napia hatuta ruhusiwa kufungua Bandari kwa eneo fulani katika ukanda ule,

na hayo ndiyo aliyokua anayapinga Hayati JPM.

kwa mtazamo wangu, kama kweli hayo ndiyo yaliyomo kwenye mkataba huo,

Naungana na Mawazo ya JPM,

Japo naamini huenda kuna mengi zaidi ndani ya mkataba huo...

#God bless Africa [emoji288]
#God bless Tanzania [emoji1241]
 
Ndege zenu je uliwahi kuona mkataba?!!..Ujenzi wa Bwawa la Nyerere Unao mkataba?!!..Unakumbuka Ujenzi wa Daraja la Nyerere (Kigamboni) tulisema ni mradi wa kifisadi lakini tumeenda kuzindua na makamera kibao!!...Umeona mkataba wa Madini yetu?!!.. Bandari ni Nguzo ya Uchumi?!!..Kwa miaka 20 ijayo Dar es salaam Itakua Ndogo ndio maana lazima tuwe na mbadala!!..( Mbona Bagamoyo kuna Bandari na ilijengwa na wakoloni)... Unaonaje mizigo ya Malawi, Rwanda, Burundi ikiwaja Bagamoyo?!..Hivi na ufahamu wako unakubali kwenye Bandari iwe yetu alafu wachina wasitoe Mapato?!!..Mbona Nchi nyingine Duniani wanazo Bandari za kimkakati kama hii tunayotaka Bagamoyo!!!...
 
Ni kama Ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa Chato?!!..sasa hivi watu wanaweka mazao (kukaushia) kwenye run way....
 
8. What is the role of(nini nafasi ya) Oman katika huu mkataba wa ujenzi wa bandari? Niliwahi kuona mahali akitajwa kama financier wa mradi. Na hapo pia kama financier huzaa maswali lukuki ya kujiuliza.
Mbona barabarani yako ya Mwendokasi wewe sio uliyetoa fedha?!!!...
 
Kwa ukubwa wa China ni wazi Bandari zetu zote bado zitaendelea kutumika!!..

Kwa Nchi zinazo tuzunguka ni wazi Bandari hii itapata mizigo ya kutosha!!..

Miaka 99 nikueleweshe kidogo,Hati zote kubwa za Ardhi ni 99 years!!.. Yawezekana Mheshimiwa alitaka kuongea Jambo lakini akashindwa!!..
 
Umetofautiana na Nani!!..Kwani Bagamoyo hakuna Bandari?!!... Unataka Viwanda vyote vya Bagamoyo walete mizigo Dar es salaam?!!..Shida mnadhani kila kitu ni Personal
 
Mama samia wanampeleka chaka bila kujijua, uyu mama angebaki nyumban kuwapikia wajukuu
Ndio kashakua Raisi wetu hakuna Namna tena!!..Tuna muunga Mkono!!..Akienda kufungua Mkoa wa Chato tuanze kusema au ni Sawa?!!
 
Hiyo inakuwa Bandari ya Uchina. Nil sawa tumemuuzia Mchina ardhi ya kujenga bandari wakati sisi tuna Bandari zetu.
Halafu tumieni akili na kuona kisichoonekana kwa macho ya kawaida.
Unajua kuhusu DP (Dubai Ports) hebu kasome kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…