Tuache ujinga wa kuwa na dhana mbaya na kubeza kila linalofanywa na utawala uliopo na kutaka kuaminisha watu tena kwa nguvu kwamba eti ni Magufuli tu ndiye aliyekuwa na nia njema na nchi hii na kwamba wengine wote ni wapigaji tu,huko ni kumkufuru na kumkosea mwenyezi Mungu kwani mwenyezi Mungu kama aliweza kumuumba huyo Magufuli atashindwaje kuumba wengine kama yeye?
Binafsi naamini utendaji kazi wa Rais Samia ni wa makini na ni wenye lengo la kuleta manufaa kwa taifa na wananchi wake kwa ujumla hivyo sikubaliani na upuuzi wowote unaeletwa na mtu yeyote kwa sababu ya chuki zake binafsi.
Najua hivi sasa kuna vita kubwa inayoendelea baina ya makundi fulani fulani kwa sababu ya utashi wao binafsi tu na wengine wamekuwa wakipinga utawala wa Rais Samia lakini huwezi kuwasikia wakizisema wazi sababu zao(halisi) bali wao wamebaki tu kujificha kwenye box la "uzalendo".
Watu hawa ndio wamekuwa vinara wa kuzua uongo kila kukicha ili tu watimize kile wanachokusudia,
Watu hawa ni sawa na chui waliojivika ngozi ya kondoo,
Watu hawa ukiwatizama usoni wanajionesha tofauti na walichokificha ndani ya mioyo yao.
Hawa watu ni wanafiki na ni wabinafsi na ni watu hatari sana.