Baada ya TPA kutangaza tenda kuhusu uwekezaji Terminal 2, Bado mnaamini Bandari zote zimeuzwa?

Sasa hivi wamekuja na nyimbo mpya, kuwa serikali za Tanzania na Dubai zimewaogopa, TEC, mwambulukusi, mdudu na silaa.
 
Tamko la TEC litaendelea kusomwa ili tuendelee kuona matokeo zaidi.

Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.
 
Hakuna haja ya kupindua meza. Ukweli umefika na umehitimisha hoja kuwa warakd ni takataka
Mnajitahidi kupindua meza😂😂😂😂 waraka ndo umefanya tenda itangazwe unaisi Kila mtu ni mjinga sio kwani iga ilkua inasemaje?
 
Hata hii mikataba leo hii tunayolipishwa kwenye mahakama za kimataifa tulipiga kelele na mkasema hatuelewi. Leo hii kila kesi tunalambishwa mchanga. Tunawajua nyie ni wezi msio na akili.
Muulize kabudi akisaidiwa na mruma waliounda mikataba hiyo.

Unafikiri tumesahau mikataba ya kujimwambafai ilikuwa ya kijinga?

Hivi kwanini waandishi hawamuulizi kabudi na mruma, vipi wanahenyeshwa icsid?
 
Mnajitahidi kupindua meza😂😂😂😂 waraka ndo umefanya tenda itangazwe unaisi Kila mtu ni mjinga sio kwani iga ilkua inasemaje?
Tenda bado zinaendelea kutangazwa kwa kutegemea mahitaji ya sekta ya bandari, serikali haifanyi kazi kwa kutegemea waraka wa taasisi ya dini.

Bagamoyo tenda itatangazwa, Mbamba Bay tenda itatangazwa, Ziwa Tanganyika tenda itatangazwa, itategemea na mahitaji ya TPA ya muda husika.
 
Waambie pia DP yupo Terminsl 1. Gsti 5 hadi 7
 
Kwa hiyo hiyo ndiyo akili mmekuja nayo ya kujifanya mnatangaza tenda ya kuwekeza hiyo sehemu kwa kuwafanya watanzania waonekane akili na ufahamu wao ni kituko kama ulivyo wewe.
 
Unatwanga maji kwenye kinu; bora tu ukae kimya kama ambavyo wamefanya viongozi
 
Basi tufafanulie iga au ilikua kujifurahisha?
 
Basi kama kazi umeshamaliza vuta shuka piga usingizi ama panda juu ya meza burudisha koo/lainisha koo😂
 
Chadema ndio waliosambaza hii sumu kwa wananchi ambao nao bila kupepesa macho wakaingia kichwa kichwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…