Baada ya WB na Denmark kusitisha misaada na uhusiano wanaofuata ni Scandinavia, EU, UK, Canada na Marekani

mbona kama vile unafurahia tz kunyimwa misaada
 
Am just thinking of my mother, she's about to retire Na haya majibwa yamepitisha 25 Kwa 75% Na alivyo spender mamangu Na ccm die hard fan, lord have mercy! No wonder Joyce mapunjo alipotumbuliwa Tu ukatibu mkuu akajifia, dahh!
Acha uchuro. Joice yu hai na afya nzuri
 
Niona Zimbabwe ya Mogabe inakuja !
na wanaoumia na hali ngumu ni mafukara, pombe anaendelea kula kuku wa bure !
 
Nchi ikitekeleza bajeti kwa 40% tu huenda inatekeleza kwa misaada tunayopokea kutoka kwa wahisani ambayo ni 40% tunayo pewa sasa twaweza kujiuliza hizo pesa zingine 40% zinaenda wapi.
Kama wanachangia 40% ya bajeti na huku bajeti yenyewe ikitekelezwa kwa 40% hiyo hiyo ni nini kinafuata nchi hii ?

Enzi za kubandika viraka kwenye makalio imerudi !
 
Mwacheni achape kazi Mh.Mbunge haya yote ni matokeo ya Serikali yenyewe. Miaka yote hiyo waje kuamua leo kutunyima misaada kwa kauli ya Zitto kwani wenyewe hawaoni madudu yanayotendeka acha kuvaa miwani ya mbao.
 
Unaweweseka tu. Hayo masharti ya IMF na WB (SAPI na SAPII ya Kighoma Malima) yalikuja baada ya uchumi kutetereka kufuatia vita vya Kagera na sio kabla ya hapo. Usitake kulazimisha.

=I agree to disagree; sio to disagreed.
Mkuu mmepishana tu' Jamaa anasema kufunga mkanda ilikuwa baada ya vita, Ila si vita tu vilivyosababisha tufunge mkanda, ila mahusiano yetu mabaya na nchi washirika ndio yalisababisha tukafunga mkanda kwa mda mrefu. Sijui kama yupo sawa au la Ila ndicho alichomaanisha nadhani.
 
Tutajuta kukubali kuongozwa na washamba wapenda sifa binafsi
 
Wewe unayesema tutabaki na mchina, hebu pitia hapa.

GOOGLE: Debt-trap allegations push China tighten reighs of foreign aid

SOURCE: scmp.com/Diplomacy
 
Kwani Amba Rutty alitaka msaada??? Ni starehe zenu wengine wakimpenda mtu wanamtunuku marinda kwa vigelegele lukuki.
Yaani unalilia msaada kama mtoto mdogo. Kwa hiyo uko tayari kutatuliwa marinda alimradi tu upewe msaada? Aisee.
 
Ameuwawa Alfonse Mawazo kikatili
Amepotea Ben Saanane
Mbowe ameharibiwa mali zake
Tundu Lissu amepigwa risasi kwa kulenga kumuua
Viongozi wa upinzani ,Hananasif, Morogoro wameuwawa
Upinzani unadhulumiwa kwenye uchaguzi
Rais kubagua wananchi kutokana na walivyompigia kura
Rais kumwagiza spika kuwashughulikia wapinzani bungeni
Kupotea kwa mwadishi wa habari Azory Gwanda
Kutekwa kwa Mo Dewji
Manji kusota bila kesi ya kueleweka
Double standards kuhusu elimu ya Bashite
Habari zote hizo zina trend kwenye mitandao na hao wazungu wanaziona,
Je, wakigoma kutoa misaada yao tutasema ni vita vya kiuchumi? Kuzuia wanafunzi waliopata mimba kuendelea na shule ni uungwana au ubinadamu wakati mazingira yenyewe si rafiki?
Hapo kuna vita vya kiuchumi au kidemokrasia na haki?

Huwezi ukawa unanyanyasa wanao halafu eti majirani na marafiki zako wasikusumbue. Hawataweza kuvumilia na kukuchekea.
 
Wazungu wana chuki binafsi na Ngosha,sababu wanaona ameimalisha uchumi ,na democrasia kwenye utawala wake imekuwa huru zaidi kuliko watangulizi wake, na huru wa kujieleza pia upo vizuri,,

na kikubwa kinachowauma ni kuruhusu jeshi wananunue mazao ya kilimo, kwaiyo wanamuonea gere Rais wetu mtukufu,,na wakae wakijua huyu tunae mpk miaka mia ijayo
 
Yote haya ni kwa sababu ya mtu mmoja, MAKONDA. Mkurupukaji, nchi yetu haiiungi mkono ushoga ila inahitaji busara ya hali ya juu kudili na hili jambo. Membe aliweza
 
Yaani wanachangia40% ya bajeti yetu? Halafu tukijitutumua sana tunaitekeleza kwa asilimia 50, maana yake ni kwamba tuna uwezo wa kutekeleza bajeti kwa asilimia 10 tu. Hii tafsiri yake tujiandae kurudi nyuma miaka 40. Lakini la kujiuliza kama taifa tumekosea wapi?
 
Acha kujitoa ufaham mapema, unataka kusema zito ndo anaawapelekea habari za watu kutekwa na wasiojulikana? Tena wb wamechelewa hizo plan walikuwa nazo tangu utawala huu ulipoanza hata kabla kwa kile kilichoitwa ni democracy depression.
 
Sera ni 'Ujamaa na kujitegemea'. Kiongozi wetu ameamua iwe hivyo kweli basi wananchi tujipange kweli kujitegemea' mtu aliyeamua kujitegemea hajali hata akishindia andazi na chumvi ili mradi anajitegemea. Ni tofauti na mtu anayeamini kwenye 'nipe nikupe, raha tupate'. Kama yakitushinda 2020 kuna nafasi ya maamuzi. Kukiwa na utulivu na akapita ina maana tupo tayari kujitegemea hivyo tuache lawama tumuache Apige kazi.
 
Tatizo wengi mnajua sana....no matter what,God is our refuge. ..ukiiombea nchi yako mabaya,basi ya kukute wewe na familia yako.

Mambo mengine Muwe mnatumia personal nouns....wengine tunamlilia Mungu juu ya Taifa.
Hakuna anayeombea mabaya msiharibu makusudi mtegemee Mungu atasaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…