Baada ya Zambia zamu ya Kenya, China mbioni kutaifisha SGR kulipia deni

Baada ya Zambia zamu ya Kenya, China mbioni kutaifisha SGR kulipia deni

Hata kule zambia vichwa ngumu walikuwa wanasema kama wewe lkn mwisho wake sasa hivi uwanja wa ndege siyo mali yao tena na zesco ipo chini ya futi 4
Hawa viazi watakuumiza kichwa bure.
Juzi crush wa bashite si kasema jamaa masharti yao mazuriiiii.

Yani kweli hata km mtu ana akili za kuazima atawezaje kusema wachina wana misaada mizuri.

Ili hali kabla ya kizazi chetu kupita watakuwa wameshachukua strategic nyingi sana za Africa.

Cha kufanya huko mbeleni ni kubadilisha katiba na wale wote walioleta ujinga wananyongwa kwa kamba.

Kama mtu alishakufa tunafukua na kumchoma.
 
Hamna tatizo kwani hiyo reli wataipakia kwenye meli kwenda nayo China? Si itaendelea kutumiwa Na wakenya.Poa tu
 
Ukila cha mchina jiandae kumpa chake. Ukila cha Mzungu masharti baba ''Kubalini ndoa za jinsi Moja''. Utaweza masharti hayo?
Bora cha mzungu wasio malijali watajijua wenyew lakin mchina kuchukua vyetu tena hapana
 
Magufuli hajatunga kodi mpya toka aingie ndio kwanza amefyeka makodi ya hovyo
fyatilia hiyo hiyo kodi ya kisima alianzisha nani,halafu sheria ya maji ipo wazi kabisa,ukichimba kisima kwa ajili ya biashara lazima ulipe kodi,na sio kisima cha uwani kwako
Ye ndo mwanzilishi wa kodi mpya kwenye vyanzo vile vile vya kodi.Vyanzo vya kodi avijaongozeka kilichongezeka ni Sheria mpya zingine za kodi juu ya vyanzo vile vile vya kodi.mfano kodi ya mafuta ya kula,
 
Kukopa harusi, kulipa matanga

Unakopa pesa za mradi mchina anakupa tena kwa riba nafuu katika maelewano ya malipo anakwambia wacha nikusaidie kuuendesha mradi faida tugawane kwa asilimia kadhaa ili nijilipe na nikimaliza nakuachia wananchi wako wenye utaalamu niliowajengea wa kuendesha mradi. Itakusaidi wewe uendelee na shughuli zingine utaki.

Nikopeshe ntalipa shida yako iko wapi wakati auna weledi wa kuendesha hiyo biashara 'grace period' inaisha faida za mradi azitoshi kufidia deni. Mapato yako ya ndani yanamatumizi mengine, huna hela mtu akichukua mradi kuokoa hasara zake unaanza kelele mchina sio mtu mzuri.

Ndio yangetukuta hayo tungekuwa tumekopa kununua ndege, kila siku itaenda sijui huku au kule wakati mpaka muda huu ujasikia habari zozote za local strategic alliance huko tunapotarajiwa kwenda as if Dar Es Salaam is a major international business hub ya kuweza kujaza abiria kutoka Mumbai au sujui New York.

Kenya tu inatuzidi kwa idadi ya wageni inayopokea kutoka USA na hata wao kujaza ndege wanaitaji abiria kutoka miji yote mikubwa ya states zingine kufanikisha ilo utaona wanamakubaliano na American Airline kuwaletea huko walipo mpaka JFK, leave alone their sky team partners Delta.

Sasa wewe unapeleka ndege kichwa kichwa hiyo biashara unayo kweli, hizo ndio sababu saa zingine mkubwa anashauriwa achana na hayo mambo ya ndege ao watu kuendesha hiyo biashara hatuna na ndege unazoanza nazo kwenye kibishara ambayo economic of scales plays a huge part kupata faida na reputation ya usalama wa angani ni muhimu huko sio size yetu kwa matatizo yaliyopo. Lakini wapi ndege ndege ndege lol.
 
Hao Moody's achana nao. Wapotoshaji wakubwa hao. Hizi ndio 'propaganda' za 'Western' zitakazowaondolea heshima ndogo waliyobaki nayo.
Deni la China kwa Kenya linafanya asili mia ishrini tu ya madeni yote ya nje iliyo nayo Kenya. Tena mengi ya madeni hayo ni kutoka huko huko kwao. Leo wanakuja hapa na uongo wa wazi eti ni asili mia 74?

Kama kuna hatari kubwa kwa Kenya kushindwa kulipia madeni yake, itakuwa ni madeni iliyokopa toka kwenye mabenki ya huko huko kwao.
 
CC: Jiwe

Africa,badala ya ku-focus kuongeza uzalishaji katika nchi nzetu pamoja na kubuni vyanzo vya mapato,tuna focus zaidi kukopa kufanya mambo makubwa ambayo si tu hatuna uwezo nayo,bali hata kiuchumi vinakuwa ni vitu ambavyo vinageuka liability kwetu.

Hizi SGR kwa nchi zetu ambazo sio industrialised ukichunguza utagundua haziwezi kuwa na tija kiuchumi zaidi ya kuwa na faida za kijamii tu kwa watu kusafiri kutoka point A kwenda point B wakiwa na vitu kama virobota viwili au vitatu vya nguo za mitumbo,vikatoni vya sabuni,n.k

We are the next.
Huna maono! Mjerumani alianza kujenga Reli ya kati mwaka 1905 hukona baadae kumaliziwa na Muingereza na mpaka sasa 2018 hipo, TRC imeongeza mapato mpaka sasa wanakusanya zaidi ya Billion 30+ kwa mwaka, Reli ya SGR italifaidisha Taifa na mapato yatapanda kwa % kubwa mno pia itatufungulia njia za kibiashara kwa nchi za jirani kama Rwanda, Burundi hata Congo kuhakikisha tunawafikishia mizigo yao kwa haraka.

Ukiangalia tayari Gate No. 1 tayari limeboreshwa na kuongezwa ukubwa chini ya TPA na hapo yatajengwa Magate 7 lengo kuiongezea uwezo Bandari yetu iweze kutoa huduma kwa kiwango cha juu.

Unachomasema sawa na kusema mradi wa Stlegler;s Goege wa Umeme pale Rufiji ambao utaenda kutumia zaidi ya Trillion 3 hauna tija! Huu ni upuuzi
 
Hawa viazi watakuumiza kichwa bure.
Juzi crush wa bashite si kasema jamaa masharti yao mazuriiiii.

Yani kweli hata km mtu ana akili za kuazima atawezaje kusema wachina wana misaada mizuri.

Ili hali kabla ya kizazi chetu kupita watakuwa wameshachukua strategic nyingi sana za Africa.

Cha kufanya huko mbeleni ni kubadilisha katiba na wale wote walioleta ujinga wananyongwa kwa kamba.

Kama mtu alishakufa tunafukua na kumchoma.
Alisema lakini ujue lile jengo la Maktaba ujenzi wake ni Ruzuku sio Mkopo na pia ukumbuke tu kuwa alijaribu Mh Rais kutafuta mkopo kwaajili ya kuanza kujenga reli ya SGR ila alishindwa kwenye masharti na mmoja wapo ambae akitaka autekereze uo mradi wa SGR ni Mcina lakini alikosa Tender! Huyo ndiye JPM.
 
Hujui maana ya kutaifisha.
Kwanza hawajataifisha kutaifisha kingereza nationalization ni kuifanya mali kuwa ya taifa.Wachina hawawezi ifanya mali yoyote ya nchi yeyote nje ya China kuwa mali ya China.kote mnakosema China imetaifisha au itataifisha sio kweli China wanachofanya ni management contract wanachukua mali uliyoweka dhamana wanasimamia hiyo biashara wakikusanya mapato Na kukata pesa ya mkopo wao ukiisha wanakurudishia mali yako.Ulivyoandika mleta mada umeandika kimbumbu utafikiri mchina atachukua reli kuwa mali yake.Zambia anaendesha reli Na shirika la umeme mkopo ukiisha anawaachia wazambia.Tatizo mumeleweshwa Na wazungu kudanganywa Na vyombo vyao vya propaganda kuwa mchina anachukua forever mali zilizowekwa dhamana mkopo usipolipika.Hilo neno la kutaifisha kwenye kichwa cha habari yako linaonyesha wazi kuwa umejaa ujinga wa kukutosha huelewi hata maana ya kutaifisha au kwa kingereza Nationalization.Uko mweupe kichwani hamna kitu
 
Kenya assets risk seizure by Chinese — Moody's

A large segment of Kenya's Chinese debt is linked to construction of the Standard Gauge Railway (SGR).

Chinese debt stood at Ksh554.88 billion (5.4 billion) or 73.4 percent of total bilateral debt of Ksh756.28 billion (7.3 billion) at the end of September.

Kenya is among countries at the highest risk of losing strategic assets to China over the pile of debt it owes Beijing, global ratings firm Moody’s Investor Service has said in a newly-released report that has raised eyebrows in public finance circles.

Moody’s says in the report that China’s response to sub-Saharan Africa countries facing liquidity pressure has not been uniform or transparent - meaning predictability of credit implications are less clear.

“Countries rich in natural resources, like Angola, Zambia, and Republic of the Congo, or with strategically important infrastructure, like ports or railways such as Kenya, are most vulnerable to the risk of losing control over important assets in negotiations with Chinese creditors,” Moody’s warns.
Hivi kutaifisha ni nini?
 
Kukopa harusi, kulipa matanga

Unakopa pesa za mradi mchina anakupa tena kwa riba nafuu katika maelewano ya malipo anakwambia wacha nikusaidie kuuendesha mradi faida tugawane kwa asilimia kadhaa ili nijilipe na nikimaliza nakuachia wananchi wako wenye utaalamu niliowajengea wa kuendesha mradi. Itakusaidi wewe uendelee na shughuli zingine utaki.

Nikopeshe ntalipa shida yako iko wapi wakati auna weledi wa kuendesha hiyo biashara 'grace period' inaisha faida za mradi azitoshi kufidia deni. Mapato yako ya ndani yanamatumizi mengine, huna hela mtu akichukua mradi kuokoa hasara zake unaanza kelele mchina sio mtu mzuri.

Ndio yangetukuta hayo tungekuwa tumekopa kununua ndege, kila siku itaenda sijui huku au kule wakati mpaka muda huu ujasikia habari zozote za local strategic alliance huko tunapotarajiwa kwenda as if Dar Es Salaam is a major international business hub ya kuweza kujaza abiria kutoka Mumbai au sujui New York.

Kenya tu inatuzidi kwa idadi ya wageni inayopokea kutoka USA na hata wao kujaza ndege wanaitaji abiria kutoka miji yote mikubwa ya states zingine kufanikisha ilo utaona wanamakubaliano na American Airline kuwaletea huko walipo mpaka JFK, leave alone their sky team partners Delta.

Sasa wewe unapeleka ndege kichwa kichwa hiyo biashara unayo kweli, hizo ndio sababu saa zingine mkubwa anashauriwa achana na hayo mambo ya ndege ao watu kuendesha hiyo biashara hatuna na ndege unazoanza nazo kwenye kibishara ambayo economic of scales plays a huge part kupata faida na reputation ya usalama wa angani ni muhimu huko sio size yetu kwa matatizo yaliyopo. Lakini wapi ndege ndege ndege lol.
Tungekuwa na Kiongozi kama wewe Tanzania ingalituchukua Miaka 500 kumiliki ndege.
 
Hizi habari zinazidi kumuumbua tu huyo mtu wenu.

Cha muhimu ni kuchunguza chanzo cha habari - kuna vita baridi inaendelea baina ya Nchi za magharibi specifically Marekani na China - nakwambia hata habari hizi zinatoka huko huko magharibi - lengo lao ni kujaribu kuwatisha Wafrica ili wasishirikiane na Wachina, nchi za magharibi zemejisahau kwamba wao ndio walikuwa vinara wa kunyonya nchi za Kiafrica bila ya kuchangia chochote cha maana, Bara la Afrika liliendekea kubaki nyuma kimaendeleo hasa katika suala la viwanda na infrastructure,Wachina pamoja na mapungufu yao ya hapa na pale lakini ndani ya miaka 15 - 20 China imendeleza sana Bara letu. Someni kitabu cha marehemu Professor Walter Rodney "How Europe underdeveloped Africa"

Tusewe tunarudia rudia propaganda za magharibi zenye lengo la ku-demonise WaChina, tuwe na tamaduni za kuwashukuru wanao tutendea mema.
 
Kwanza hawajataifisha kutaifisha kingereza nationalization ni kuifanya mali kuwa ya taifa.Wachina hawawezi ifanya mali yoyote ya nchi yeyote nje ya China kuwa mali ya China.kote mnakosema China imetaifisha au itataifisha sio kweli China wanachofanya ni management contract wanachukua mali uliyoweka dhamana wanasimamia hiyo biashara wakikusanya mapato Na kukata pesa ya mkopo wao ukiisha wanakurudishia mali yako.Ulivyoandika mleta mada umeandika kimbumbu utafikiri mchina atachukua reli kuwa mali yake.Zambia anaendesha reli Na shirika la umeme mkopo ukiisha anawaachia wazambia.Tatizo mumeleweshwa Na wazungu kudanganywa Na vyombo vyao vya propaganda kuwa mchina anachukua forever mali zilizowekwa dhamana mkopo usipolipika.Hilo neno la kutaifisha kwenye kichwa cha habari yako linaonyesha wazi kuwa umejaa ujinga wa kukutosha huelewi hata maana ya kutaifisha au kwa kingereza Nationalization.Uko mweupe kichwani hamna kitu
Kumbe unajua wanachokifanya China basi endeleeni kuwatukuza, halafu kwa akili yako unadhani habari hii nimeiandika mimi.
 
Kumbe unajua wanachokifanya China basi endeleeni kuwatukuza, halafu kwa akili yako unadhani habari hii nimeiandika mimi.
Kichwa cha mada umeandika wewe habari yenyewe haiongelei kutaifisha au nationalization.Ila kwa uelewa wako mdogo hiyo habari wewe umeielewa kuwa ni kutaifisha!!!!!Ndio kwa huo uelewa wako mdogo below the sea level ukaweka kichwa kwenye mada yako kuwa ni kutaifisha.!!!!
 
Cha muhimu in kuchunguza chanzo cha habari - kuna vita baridi inaendelea baina ya Nchi za magharibi specifically Marekani na China - najwanbia hata havari hizi zinatoka huko huko magharibi - lengo lao ni kujaribu kuwatisha Wafrica, wanasahau kwamba wao ndio walikuwa vinara wa kunyonya nchi za kiafrica bila ya kuchangia chochote cha maana, Bara la Afrika liliendekea kubaki nyuma kimaendekeo hasa katika suala la viwanda na infrastructure,Wachina pamoja na mapungufu yao ya hapa na pale lakini ndani ya miaka 15 - 20 China imendeleza sana Bara letu.

Tusewe tunarudia rudia propaganda za magharibi zenye lengo la ku-demonise China, tuwe na tamaduni za kuwashukuru wanao tutendea mema.
Inawezekana kuwa ni propaganda lkn kwa dunia ya sasa propaganda ndizo zinatawala dunia, lkn kiuhalisia Kenya inadaiwa na China deni kubwa.
 
Kichwa cha habari umeandika wewe habari yenyewe haiongelei kutaifisha au nationalization.Ila kwa uelewa wako mdogo hiyo habari wewe umeielewa kuwa ni kutaifisha!!!!!Ndio kwa huo uelewa wako mdogo below the sea level ukaweka kichwa kwenye mada yako kuwa ni kutaifisha.!!!!
Kwahiyo wewe unachoangalia ni heading tu, endeleeni kuwatukuza wachina kuna siku Tanzania itaitwa TanChing.
 
Wewe tumia akili angalau kidogo basi huyo ndiyo mchina mnaye mpigia magoti na makofi lazima mtazitema hizo fedha zake
Unaongea na makasuku mkuu, hawana lolote la ziada wanalolijua. Moja tu wanalolifaham ni kumshangilia mfalme
 
Kweli kabisa ndugu yangu yaani hawa watu kwao kila kitu ni kushangilia bila ya kusema no kwa malaika wao
Unaongea na makasuku mkuu, hawana lolote la ziada wanalolijua. Moja tu wanalolifaham ni kumshangilia mfalme
 
Back
Top Bottom