Baadhi ya abiria treni ya SGR wadaiwa kuihujumu TRC, nauli haziendani na safari zao

Tanzania tuna tatizo la malezi.
Watu hawana maadili.

Ukisema maadili, watanzania wengi watafikiria ni kuvaa nguo ndefu, kusalimia shikamoo na kutotumia lugha za matusi.

Lakini hatusisitiziwi kuwa waaminifu, wachapakazi, wenye bidii, wawajibikaji, wazalendo n.k
Haya ndiyo maadili sasa!

Kama malezi yetu hayatabadilika, tutaendelea kuwa taifa la watu wa hovyo kwa muda mrefu sana.
 
Ni mchezo uleule kama ilivyo BRT, bila kubinafsisha haya mambo hatuyawezi.
 
Waweke mfumo wa mwendokasi kama ule wa zamani unascan tiketi unavyoingia unascan unavyotoka
 
maana yake hakuna ukaguzi?

hata kwenye daladala konda yupo makini mtu asipitilize kunakoishia nauli yake
 
Huyo Kamanda wa Takukuru hafai kuwepo kwenye hiyo nafas yaani ameongea kama vile mtu asiyekuwa na mamlaka, kwanza ilitakiwa wakamatwe wahusika ndio jambo lizungumzwe.
 
Mbn ndani ya hizo behewa kuna TT wanapitaga kukagua tiketi..!!.km nauli uliolipa inaendana na safari yako.
 
Mbn ndani ya hizo behewa kuna TT wanapitaga kukagua tiketi..!!.km nauli uliolipa inaendana na safari yako.
Ndio maana TAKUKURU wameingilia kati. Watu hawajiulizi TAKUKURU na kutokulipa nauli wapi na wapi. Huyo kamanda wa TAKUKURU hajataka kuwachana moja kwa moja hao TT kwamba wanachukua rushwa. Mtu kalipa buku, zingine wanaweka mifukoni mwao!
 
Hata nyumbani kwako, ikitokea ukaacha wazi mlango, watakuja tu wa kukuibia siku moja. TRC walipaswa kuliona hili kabla, kuliko kuja kulia lia.

Ova
 
Halafu wasikilize wanavyolaumu viongozi wao wakati ni pipa na mfuniko.
 
Ndio maana TAKUKURU wameingilia kati. Watu hawajiulizi TAKUKURU na kutokulipa nauli wapi na wapi. Huyo kamanda wa TAKUKURU hajataka kuwachana moja kwa moja hao TT kwamba wanachukua rushwa. Mtu kalipa buku, zingine wanaweka mifukoni mwao!
Nmekuelewa issue itakua kwa wale TT..wanapitaga na vimachine vya kulipishia additional fair.kumbe hamna kitu
 
Kwani hakuna wakaguzi ndani ya treni?
Hawakujua kuwa wizi na uongo ni jadi yetu
Kwanini wasiliweke katika sheria zao za kulinda treni
Tuna treni kabla hata ya Uhuru na wizi wa kukwepa kulipa ulikuwepo eti leo mmasema watu hawalipi

Kuna upigaji waseme ukweli
Kwani kuna wasafiri wangapi kwa siku kwenye treni moja washindwe kuwauliza tickets?
Naomba anaejua afafanue hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…