PreGE2025 Baadhi ya G-55 wakiwemo Benson Kigaila, John Mrema, Catherine Ruge na Salum Mwalimu wajiondoa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Benson Kigaila ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara amesema yeye na Wanachama wenzake wamejitoa katika chama hicho kutokana na kutoridhishwa na yanayoendelea

Ametangaza uamuzi huo akiwa pamoja na aliyekuwa Makamu wa CHADEMA Taifa - Zanzibar, Salum Mwalimu, aliyewai kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Catherine Ruge, John Mrema na Julius Mwita


View: https://www.youtube.com/live/Z_apgr0qkZM?si=Lj9DabbYPf6LP8KC

===

Updates


Katika mkutano huu na waandishi wa habari wajumbe wote wa sekretarieti ya CHADEMA Taifa iliyopita wapo isipokuwa watu wawili ambao ndiyo hawakuwepo hapo kwa mujibu wa John Mrema. Ambao ni;
  • Catherine Ruge - Aliyekuwa Katibu Mkuu BAWACHA-Taifa
  • Julius Mwita - Aliyekuwa katibu wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa
  • John Mrema - Aliyekuwa Mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano, uenezi na mambo ya nje
  • Salum Mwalimu - Aliyekuwa Naibu Katibu mkuu CHADEMA, Zanzibar
  • Benson kigaila - Aliyekuwa Naibu katibu mkuu CHADEMA, Bara
Wanaeleza kuwa baada ya ushindi, Freeman Mbowe alikubali maridhiano yawepo mara baada ya makundi yaliyopo wakati wa kampeni, ila walishangazwa na kumuona aliyeshinda nafasi ya Uenyekiti Tundu Lissu aliendelea kumshambulia Freeman Mbowe kama vile kampeni bado zinaendelea, ameeleza Benson Kigaila.
Your browser is not able to display this video.

Kigaila anaendelea kueleza kuwa Kuna makundi ngazi ya chini kwenye chama wana vikao vya kuwaengua ama kuwafuta uanachama wanachama waliokuwa wanamuunga mkono Freeman Mbowe.

Wanaeleza pia kuwa ndani ya Chama kuna udikteta uchwara na hivyo wapo kwa ajili ya kuupinga udikteta huo ndani ya chama. Aidha hakuna haki ya kusikilizwa ndani ya chama wala hakuna haki ya watu kuhoji na wanaofanya hivyo wanaitwa wasaliti, njaa. Wanahoji Je, kati ya wao na aliyepinga maridhiano chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe nani msaliti?

G-55 wanasistiza kama unataka kuzia uchaguzi na hakuna mkakati wa kuzuia uchaguzi maana yake umeamua CCM wapite bila kupigwa.

Rasmi wamesema wamejiondoa CHADEMA lakini hawatokwenda CCM, muda ukifika wataeleza ni wapi wanapohamia. Sababu kubwa ni kutokutaka kuwa sehemu ya kifo cha CHADEMA kutokana na yanayoendelea. Hayo yamesemwa na Benson Kigaila aliyekuwa Naibu katibu mkuu Chadema (Bara)
Your browser is not able to display this video.


Soma pia:
 
Kupitia ukurasa wake wa X, John Mrema ametangaza leo kuwa na mkutano na waandishi wa habari Golden Tulip, Masaki.
View attachment 3326611
kila leo conferences.........................nasikia wanakwenda CHAUMA. Wote na Lisu takataka walivyobehave wakati wa kampeni! Takataka tupu, na hili John linaendelea kuwa takataka kiwango cha lami!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…