PreGE2025 Baadhi ya G-55 wakiwemo Benson Kigaila, John Mrema, Catherine Ruge na Salum Mwalimu wajiondoa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mimi nadhani Lissu atatoka mapema tu. Wamemfanya inconsequential. Atajaza watu kwenye mikutano ya hadhara lakini at the end of the day Bunge lijalo halitakuwa na mbunge hata mmoja wa Chadema. Aidha, hakuwa na diwani hata mmoja wa Chadema. Aidha, hawatakuwa na kura hata moja ya mgombea urais. Kwa hiyo 2025-2030 platform zao zitakuwa mitandao na mikutano ya hadhari. Ruzuku pia haitakuwepo kwa hiyo itabidi wafanye juhudi za ziada za kupata fedha za kuendesha chama. By 2030 wale walioingiza watu wao Bungeni watakuwa katika nafasi nzuri ya ku challenge kwa ajili ya ubunge, udiwani na urais. Nawatakia kila la kheri.

Amandla...
 
Acha ulaghai, hao biashara yao ilikua inajulikana toka mwanzo suala la kuhama lilikua la muda tu
Common enemy ni ccm lakini wao kila press ni kuzungumzia lissu badala ya kuikosoa ccm na serikali
 
Chadema ya chini ya mbowe 2020 walipata wabunge wangapi?
 
Ametangaza uamuzi huo akiwa pamoja na aliyekuwa Makamu wa CHADEMA Taifa - Zanzibar, Salum Mwalimu, aliyewai kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Catherine Ruge, John Mrema na Julius Mwita
Wamechukia kwakuwa waliambiwa ukweli kuwa wake zao wana covid 19 wanakula mema na wao wanakwenda kujumuika huko
 
Acha ulaghai, hao biashara yao ilikua inajulikana toka mwanzo suala la kuhama lilikua la muda tu
Common enemy ni ccm lakini wao kila press ni kuzungumzia lissu badala ya kuikosoa ccm na serikali
Wewe huoni wanavyoshambuliwa na watu kama nyinyi? Ulitegemea wabaki? Kwa vile mlijua kuwa watahama, naamini mmejipanga vizuri kuendelea na mpambano wenu dhidi ya common enemy. Kuwa hamtapoteza muda kuwakosoa waliokuwa wanachama wenu bali mtaelekeza nguvu zenu zote katika kupata katiba mpya.

Amandla...
 
John mrema alimnyima vita maalum aliyestahili Esther. Akampa devotha minja kwa kupewa Uchi. Huyo aondoke. Alafu kalivyo kajinga kanawaza Kuna mtu anakafatilia. Chadema ilikua lazima ipate viongozi wa kweli na wapinzani halisi ili wanafiki wakae pembeni na wameanza kukaa pembeni. Kamrema kila siku kanaongela ruzuku ruzuku pumbavu kabisa.
 
Ni kina nani wanapoteza muda kuwakosoa hao G55?? Wao ndio kila siku wanaitisha presa kukosoa viongozi wa Sasa

Nikuulize swali, kwa nnhao G55 hawaitishi press kuikosoa ccm na serikali?
 
Chadema ya chini ya mbowe 2020 walipata wabunge wangapi?
Mmoja. Lakini walikuwa na kura za kutosha za kuwapatia wabunge wengine wa viti maalum na ruzuku. CDM ya Lissu haitapata kura hata moja wala thumni ya ruzuku kwa vile haitashiriki katika uchaguzi.

Amandla...
 
MAMULUKI wote waondoke, na wengine wafukuzwe mara moja. Ili hapo mwishoni mwa mwaka huu chama kitakaposhika dola kisiwe na doa wala mapandikizi na vibaraka.✍️
#NoReformsNoElection
 
Mrema ni mchaga wa Marangu.
Ana njaa kwa vile ni mlevi.

Pili hajui kuwa hana umuhimu mkubwa kivile kwenye chama
Chama ilimbeba sana miaka yote hakuwa na umuhimu kabisa
 
Mmoja. Lakini walikuwa na kura za kutosha za kuwapatia wabunge wengine wa viti maalum na ruzuku. CDM ya Lissu haitapata kura hata moja wala thumni ya ruzuku kwa vile haitashiriki katika uchaguzi.

Amandla...
Chadema haipo kwa ajili ya ruzuku
 
Mmoja. Lakini walikuwa na kura za kutosha za kuwapatia wabunge wengine wa viti maalum na ruzuku. CDM ya Lissu haitapata kura hata moja wala thumni ya ruzuku kwa vile haitashiriki katika uchaguzi.

Amandla...
Unapaswa kufahamu unaongea na mtu timamu. Hizo kura za wabunge wa viti maalum nani alikua anazitaka chadema??

Chadema chini ya mbowe baada ya uchaguzi walisusia matokeo, hivyo wakasusia hata nafasi za viti maalum ndio maana waliofanya uhuni kuchukua hizo nafasi walifukuzwa uanachama. Pia chadema chini ya mbowe baada ya uchaguzi walisusia ruzuku, hawauchukua ruzuku
 
Ni kina nani wanapoteza muda kuwakosoa hao G55?? Wao ndio kila siku wanaitisha presa kukosoa viongozi wa Sasa

Nikuulize swali, kwa nnhao G55 hawaitishi press kuikosoa ccm na serikali?
Ulitaka waite presa kuikosoa CCM wakati wao sio wasemaji wa CDM?
Sishangai kuwa hukuona kebehi ( G Njaa n.k.) walikuwa wakirushiwa maana hata matusi na kejeli alizotupiwa Mbowe hukuziona.
Sasa kwa vile wametoka CDM wataeleza criticism zao dhidi ya CDM na CCM maana vyama vyote hivyo vitakuwa wapinzani wake.

Amandla...
 
Siasa ni Open market ukiona hapo ulipo hauuzi sera zako unaondoka. Na kuondoka kwa mtu katika chama hakimaanishi kitakufa.

Zito aliondoka na kelele zilikuwa nyingi lakin chama bado kipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…