PreGE2025 Baadhi ya G-55 wakiwemo Benson Kigaila, John Mrema, Catherine Ruge na Salum Mwalimu wajiondoa CHADEMA

PreGE2025 Baadhi ya G-55 wakiwemo Benson Kigaila, John Mrema, Catherine Ruge na Salum Mwalimu wajiondoa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mimi nadhani Lissu atatoka mapema tu. Wamemfanya inconsequential. Atajaza watu kwenye mikutano ya hadhara lakini at the end of the day Bunge lijalo halitakuwa na mbunge hata mmoja wa Chadema. Aidha, hakuwa na diwani hata mmoja wa Chadema. Aidha, hawatakuwa na kura hata moja ya mgombea urais. Kwa hiyo 2025-2030 platform zao zitakuwa mitandao na mikutano ya hadhari. Ruzuku pia haitakuwepo kwa hiyo itabidi wafanye juhudi za ziada za kupata fedha za kuendesha chama. By 2030 wale walioingiza watu wao Bungeni watakuwa katika nafasi nzuri ya ku challenge kwa ajili ya ubunge, udiwani na urais. Nawatakia kila la kheri.

Amandla...
Na hapa ndipo wengi tuungane na Prof. Assad aliposema kuwa hatakwenda kupiga kura hadi hapo mfumo wa uchaguzi utakapomhakikishia kuwa kura yake inahesabiwa. Kama tunaamua kuishi kwa kutokutumia akili basi na tumpuuze profesa!

Nadhani siasa ni professional kama zingine na ndio maana kuna shahada kabisa za vyuo vikuu juu ya siasa na TL aliweka wazi kuwa yeye siasa zake ni za ukombozi na sio za udalali. Binafsi sikumuelewa wakati anasema lakini nimeunganisha yaliyopita na yanayoendelea sasa ndio nikaelewa alicho maanisha.

Kilicho wazi ni kwamba, tukichagua aina ya hizi siasa unazosema (za udalali) naamini huwezi kukuza GDP ya nchi kufikia mfano wa Kenya au Mauritius, sana sana tutaishia kugawa kila rasilimali ya nchi kwa wageni na wageni wataleta hadi vibbarua kutoka nje kwa maana uelewa na attitude yetu (wananchi) itakuwa hopeless.

Hadi matundu ya choo tutaomba waarabu na wajapan watujengee wakati housegirls/boys wa watawala (achana na wake/watoto wao) wakiendesha VX zilizotokana na pesa za misaada na vikodi vyetu kidogo.
Na huku strategy ya kujenga uchumi wa mwananchi wa kawaida ikibbakia kufukuzana na wachina Kariakoo kana kwamba kuna mteja analazimishwa kwenda kwao wakati huo huo wazawa wakiuza bidhaa zote kutoka viwanda vya China!
 
Sad ya nini acha zako hizo waondokea hawana maana yoyote wakapate pombe za bure huko waendako
 
Unapaswa kufahamu unaongea na mtu timamu. Hizo kura za wabunge wa viti maalum nani alikua anazitaka chadema??

Chadema chini ya mbowe baada ya uchaguzi walisusia matokeo, hivyo wakasusia hata nafasi za viti maalum ndio maana waliofanya uhuni kuchukua hizo nafasi walifukuzwa uanachama. Pia chadema chini ya mbowe baada ya uchaguzi walisusia ruzuku, hawauchukua ruzuku
Baada ya kuanza maridhiano walipokea ruzuku. Ruzuku ndio iliyowasaidia kununua jengo lao la Makao Makuu.

Kama Chadema walikuwa hawazitaki kura za wabunge wa viti maalum isingegombea. Waliwafukuza wakina Halima kwa sababu waliona wamefanyiwa uhuni na sio kwa sababu hawakuvitaka hivyo viti.

Amandla...
 
Ulitaka waite presa kuikosoa CCM wakati wao sio wasemaji wa CDM?
Sishangai kuwa hukuona kebehi ( G Njaa n.k.) walikuwa wakirushiwa maana hata matusi na kejeli alizotupiwa Mbowe hukuziona.
Sasa kwa vile wametoka CDM wataeleza criticism zao dhidi ya CDM na CCM maana vyama vyote hivyo vitakuwa wapinzani wake.

Amandla...
Sikuwahi kujua anayepaswa kuikosoa ccm ni lazima awe msemaji wa chadema. Kwa hiyo hapo zamani walipokua wanaikosoa ccm walikua ni wasemaji wa chadema?

Wataeleza criticism zao kwa cdm na ccm? Huko watapoenda Wao watapambana na chama dola au chadema? Wataeleza criticism za chadema ili ziwasaidie nn? Wabunge waliopo majimboni ni wa ccm, Sasa wataicriticize vipi chadema?
 
Benson Kigaila ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara amesema yeye na Wanachama wenzake wamejitoa katika chama hicho kutokana na kutoridhishwa na yanayoendelea

Ametangaza uamuzi huo akiwa pamoja na aliyekuwa Makamu wa CHADEMA Taifa - Zanzibar, Salum Mwalimu, aliyewai kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Catherine Ruge, John Mrema na Julius Mwita


View: https://www.youtube.com/live/Z_apgr0qkZM?si=Lj9DabbYPf6LP8KC

View attachment 3326774
===

Updates


Katika mkutano huu na waandishi wa habari wajumbe wote wa sekretarieti ya CHADEMA Taifa iliyopita wapo isipokuwa watu wawili ambao ndiyo hawakuwepo hapo kwa mujibu wa John Mrema. Ambao ni;
  • Catherine Ruge - Aliyekuwa Katibu Mkuu BAWACHA-Taifa
  • Julius Mwita - Aliyekuwa katibu wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa
  • John Mrema - Aliyekuwa Mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano, uenezi na mambo ya nje
  • Salum Mwalimu - Aliyekuwa Naibu Katibu mkuu CHADEMA, Zanzibar
  • Benson kigaila - Aliyekuwa Naibu katibu mkuu CHADEMA, Bara
Wanaeleza kuwa baada ya ushindi, Freeman Mbowe alikubali maridhiano yawepo mara baada ya makundi yaliyopo wakati wa kampeni, ila walishangazwa na kumuona aliyeshinda nafasi ya Uenyekiti Tundu Lissu aliendelea kumshambulia Freeman Mbowe kama vile kampeni bado zinaendelea, ameeleza Benson Kigaila.
View attachment 3326841
Kigaila anaendelea kueleza kuwa Kuna makundi ngazi ya chini kwenye chama wana vikao vya kuwaengua ama kuwafuta uanachama wanachama waliokuwa wanamuunga mkono Freeman Mbowe.

Wanaeleza pia kuwa ndani ya Chama kuna udikteta uchwara na hivyo wapo kwa ajili ya kuupinga udikteta huo ndani ya chama. Aidha hakuna haki ya kusikilizwa ndani ya chama wala hakuna haki ya watu kuhoji na wanaofanya hivyo wanaitwa wasaliti, njaa. Wanahoji Je, kati ya wao na aliyepinga maridhiano chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe nani msaliti?

G-55 wanasistiza kama unataka kuzia uchaguzi na hakuna mkakati wa kuzuia uchaguzi maana yake umeamua CCM wapite bila kupigwa.

Rasmi wamesema wamejiondoa CHADEMA lakini hawatokwenda CCM, muda ukifika wataeleza ni wapi wanapohamia. Sababu kubwa ni kutokutaka kuwa sehemu ya kifo cha CHADEMA kutokana na yanayoendelea. Hayo yamesemwa na Benson Kigaila aliyekuwa Naibu katibu mkuu Chadema (Bara)
View attachment 3326835

Soma pia:

Hawana Impact hata wakati wa uwepo wao hakuna ambacho walibadili ndani ya Chadema. Kama kuna mtu anadhani Chadema itayumba kwa kuondoka kwake…. Anakosea sana na hana akili.

Niliwahai kukutana na JK huku majuu tukawa vijana wengi, kauli yake ilikuwa ni moja ; Vijana someni mje kushika taasisi Tanzania. Lakini mtambue pia hakuna taasisi iliyowahi kufa au kushindwa kufanya kazi kwa kuwa mtu fulàn mwenye skills’fulan hayupo au kasusa.,,, Kama taasisi ikifa kwa kuwa mtu fulan kaondoka… basi hiyo haikuwa taasisi , maneno mazuri kabisa JK akiwaasa vijana kuwa they can be replaced despite of skills they have

Chadema ni Taasisi, kama kuna G55 yoyote anadhan Chadema itakufa kwa kujitoa wao…… ni tatizo lingine la afya ya akili. Waende CCM au waanzishe chama chao

G55 ni bora waondoke mana walizoea Siasa za 10% ; HUU ni ujinga… huwezi kuishi kwa 10% . Mtu anaeishi kwa 10% inaogopesha hata akishika madaraka ni hatari
Chadema ya sasa perfectly align na mission za reforms and constitution ammendment…hakuna maaana ya uchaguzi kama mtu fulan anaweza kuengua yoyote na msifanye kitu…… 2020 we had perfect lesson ….. G55 waendelee kutupiga majungu na kutuombea njaa….. very soon they will be ashamed

Jesus said….., Separate the chaff from the wheat for purification. G55 ni chaffs , we cant be purified if they are in
 
Benson Kigaila ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara amesema yeye na Wanachama wenzake wamejitoa katika chama hicho kutokana na kutoridhishwa na yanayoendelea

Ametangaza uamuzi huo akiwa pamoja na aliyekuwa Makamu wa CHADEMA Taifa - Zanzibar, Salum Mwalimu, aliyewai kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Catherine Ruge, John Mrema na Julius Mwita


View: https://www.youtube.com/live/Z_apgr0qkZM?si=Lj9DabbYPf6LP8KC

View attachment 3326774
===

Updates


Katika mkutano huu na waandishi wa habari wajumbe wote wa sekretarieti ya CHADEMA Taifa iliyopita wapo isipokuwa watu wawili ambao ndiyo hawakuwepo hapo kwa mujibu wa John Mrema. Ambao ni;
  • Catherine Ruge - Aliyekuwa Katibu Mkuu BAWACHA-Taifa
  • Julius Mwita - Aliyekuwa katibu wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa
  • John Mrema - Aliyekuwa Mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano, uenezi na mambo ya nje
  • Salum Mwalimu - Aliyekuwa Naibu Katibu mkuu CHADEMA, Zanzibar
  • Benson kigaila - Aliyekuwa Naibu katibu mkuu CHADEMA, Bara
Wanaeleza kuwa baada ya ushindi, Freeman Mbowe alikubali maridhiano yawepo mara baada ya makundi yaliyopo wakati wa kampeni, ila walishangazwa na kumuona aliyeshinda nafasi ya Uenyekiti Tundu Lissu aliendelea kumshambulia Freeman Mbowe kama vile kampeni bado zinaendelea, ameeleza Benson Kigaila.
View attachment 3326841
Kigaila anaendelea kueleza kuwa Kuna makundi ngazi ya chini kwenye chama wana vikao vya kuwaengua ama kuwafuta uanachama wanachama waliokuwa wanamuunga mkono Freeman Mbowe.

Wanaeleza pia kuwa ndani ya Chama kuna udikteta uchwara na hivyo wapo kwa ajili ya kuupinga udikteta huo ndani ya chama. Aidha hakuna haki ya kusikilizwa ndani ya chama wala hakuna haki ya watu kuhoji na wanaofanya hivyo wanaitwa wasaliti, njaa. Wanahoji Je, kati ya wao na aliyepinga maridhiano chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe nani msaliti?

G-55 wanasistiza kama unataka kuzia uchaguzi na hakuna mkakati wa kuzuia uchaguzi maana yake umeamua CCM wapite bila kupigwa.

Rasmi wamesema wamejiondoa CHADEMA lakini hawatokwenda CCM, muda ukifika wataeleza ni wapi wanapohamia. Sababu kubwa ni kutokutaka kuwa sehemu ya kifo cha CHADEMA kutokana na yanayoendelea. Hayo yamesemwa na Benson Kigaila aliyekuwa Naibu katibu mkuu Chadema (Bara)
View attachment 3326835

Soma pia:

Ikuaa wazi, Lissu lengo lake ilikuwa kuishambaratizha Chadema.
Mission accomplished
 
malengo ni yapi? sasa hivi heche kanyamaza kimya, prado nimezima wese hamna, kwa ujinga wako unaamini Lissu ana nia njema na cdm? ngoja uone
We mbogamboga acha uchawa lissu ni kichwa kile
 
Baada ya kuanza maridhiano walipokea ruzuku. Ruzuku ndio iliyowasaidia kununua jengo lao la Makao Makuu.

Kama Chadema walikuwa hawazitaki kura za wabunge wa viti maalum isingegombea. Waliwafukuza wakina Halima kwa sababu waliona wamefanyiwa uhuni na sio kwa sababu hawakuvitaka hivyo viti.

Amandla...
Ruzuku waliyopokea ilisaidia kununua jengo lao? Hilo ni kosa la nani kutonunua jengo miaka yote hiyo?

Msimamo wa chadema baada ya uchaguzi ni kutoyatambua matokeo ndio maana hawakupeleka majina ya wabunge wa viti maalum.
 
Sikuwahi kujua anayepaswa kuikosoa ccm ni lazima awe msemaji wa chadema. Kwa hiyo hapo zamani walipokua wanaikosoa ccm walikua ni wasemaji wa chadema?

Wataeleza criticism zao kwa cdm na ccm? Huko watapoenda Wao watapambana na chama dola au chadema? Wataeleza criticism za chadema ili ziwasaidie nn? Wabunge waliopo majimboni ni wa ccm, Sasa wataicriticize vipi chadema?
Walikuwa viongozi ndani ya Chadema.
Watakuwa huru kukosoa Chadema kwa sababu wote watakuwa wanataka kushika dola. Watakuwa na haki ya kueleza wapiga kura sababu zao za kuondoka Chadema. Wataikosoa CCM kwa sababu ndio chama dola. Kukoselewa sio lazima uwe mbunge. Uongozi wa chama pinzani ni fair game.

Amandla...
 
haaya bwana sasa mmegawanyika....... Lisu angeliweza kuzuia mgawamyiko kwa kuwa inclusive!
Mgawanyiko upi hao wazee wa 10% percent na bia za bure ndo mgawanyiko kuwa serious bwana hawana effect yoyote ile
 
Ruzuku waliyopokea ilisaidia kununua jengo lao? Hilo ni kosa la nani kutonunua jengo miaka yote hiyo?

Msimamo wa chadema baada ya uchaguzi ni kutoyatambua matokeo ndio maana hawakupeleka majina ya wabunge wa viti maalum.
Hata siielewi hoja yako.
Hawakununua jengo kabla kwa sababu haikuwa priority yao.

Amandla...
 
Walikuwa viongozi ndani ya Chadema.
Watakuwa huru kukosoa Chadema kwa sababu wote watakuwa wanataka kushika dola. Watakuwa na haki ya kueleza wapiga kura sababu zao za kuondoka Chadema. Wataikosoa CCM kwa sababu ndio chama dola. Kukoselewa sio lazima uwe mbunge. Uongozi wa chama pinzani ni fair game.

Amandla...
Sababu za kuondoka wameshazisema, ndio nauliza watapohamia na kushiriki uchaguzi wataikosoa chadema ili wapate kitu gani?
 
Back
Top Bottom