PreGE2025 Baadhi ya G-55 wakiwemo Benson Kigaila, John Mrema, Catherine Ruge na Salum Mwalimu wajiondoa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hata siielewi hoja yako.
Hawakununua jengo kabla kwa sababu haikuwa priority yao.

Amandla...
Huelewi vipi hoja na ipo wazi, chadema iligomea kutambua matokeo ya uchaguzi wakagomea na kuchukua ruzuku. Waliokwenda kinyume na kutambua matokeo kwa kufoji nyaraka ili wapate viti maalum walifukuzwa uanachama

Hapo hujaelewa nini?
 
haaya bwana sasa mmegawanyika....... Lisu angeliweza kuzuia mgawamyiko kwa kuwa inclusive!
Lissu anazuia vipi mgawanyiko?? Awalazimishe wakubali matokeo? Aliwateua mwita na Catherine ruge, lakini bado mwita na ruge wakaendelea walichofanya. Ulitaka lissu awabebe mgongoni?
 
kila leo conferences.........................nasikia wanakwenda CHAUMA. Wote na Lisu takataka walivyobehave wakati wa kampeni! Takataka tupu, na hili John linaendelea kuwa takataka kiwango cha lami!
Waende wakaachiwe majimbo na CCM
 
Yani ilikuwa hivi, mbowe anapewa hela toka serikalini kwa upinzani wa uongo then hawa wananufaika nazo kidogo maisha yanaenda.Ukiongeza na ubunge wa kupewa kwa baadhi yao na baadhi ya wake zao viti maalumu wale covid 19 ni full kuishi.
Sasa mrija umekatwa na kufumuliwa wote ndo matokeo yake ni haya.

waende tu.
 
"Mtu anaeishi kwa 10% inaogopesha hata akishika madaraka ni hatari"
 
Leo Chadema safi, chadema wazalendo...tuna mechi kimataifa.
Anga za kimataifa, bungeni Ulaya...
hawa wezi waruzuku wapotee wasituharibie CV🤣
Mkuu, jifunze kuweka akiba ya maneno.

Nasikia hawa G55 ndio gamechanger - karata turufu!
 
Benson Kigaila ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara amesema yeye na Wanachama wenzake wamejitoa katika chama hicho kutokana na kutoridhishwa na yanayoendelea

Ametangaza uamuzi huo akiwa pamoja na aliyekuwa Makamu wa CHADEMA Taifa - Zanzibar, Salum Mwalimu, aliyewai kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Catherine Ruge, John Mrema na Julius Mwita

View: https://www.youtube.com/live/Z_apgr0qkZM?si=Lj9DabbYPf6LP8KC

View attachment 3326774
===

Updates

Katika mkutano huu na waandishi wa habari wajumbe wote wa sekretarieti ya CHADEMA Taifa iliyopita wapo isipokuwa watu wawili ambao ndiyo hawakuwepo hapo kwa mujibu wa John Mrema. Ambao ni;
  • Catherine Ruge - Aliyekuwa Katibu Mkuu BAWACHA-Taifa
  • Julius Mwita - Aliyekuwa katibu wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa
  • John Mrema - Aliyekuwa Mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano, uenezi na mambo ya nje
  • Salum Mwalimu - Aliyekuwa Naibu Katibu mkuu CHADEMA, Zanzibar
  • Benson kigaila - Aliyekuwa Naibu katibu mkuu CHADEMA, Bara
Wanaeleza kuwa baada ya ushindi, Freeman Mbowe alikubali maridhiano yawepo mara baada ya makundi yaliyopo wakati wa kampeni, ila walishangazwa na kumuona aliyeshinda nafasi ya Uenyekiti Tundu Lissu aliendelea kumshambulia Freeman Mbowe kama vile kampeni bado zinaendelea, ameeleza Benson Kigaila.
View attachment 3326841
Kigaila anaendelea kueleza kuwa Kuna makundi ngazi ya chini kwenye chama wana vikao vya kuwaengua ama kuwafuta uanachama wanachama waliokuwa wanamuunga mkono Freeman Mbowe.

Wanaeleza pia kuwa ndani ya Chama kuna udikteta uchwara na hivyo wapo kwa ajili ya kuupinga udikteta huo ndani ya chama. Aidha hakuna haki ya kusikilizwa ndani ya chama wala hakuna haki ya watu kuhoji na wanaofanya hivyo wanaitwa wasaliti, njaa. Wanahoji Je, kati ya wao na aliyepinga maridhiano chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe nani msaliti?

G-55 wanasistiza kama unataka kuzia uchaguzi na hakuna mkakati wa kuzuia uchaguzi maana yake umeamua CCM wapite bila kupigwa.

Rasmi wamesema wamejiondoa CHADEMA lakini hawatokwenda CCM, muda ukifika wataeleza ni wapi wanapohamia. Sababu kubwa ni kutokutaka kuwa sehemu ya kifo cha CHADEMA kutokana na yanayoendelea. Hayo yamesemwa na Benson Kigaila aliyekuwa Naibu katibu mkuu Chadema (Bara)
View attachment 3326835

Soma pia:

Wao walikuwa wanataka muafaka gani zaidi ya kushindwa na kutulia,Hiki nikipindi cha kutengeneza fedha kwahiyo watu wanakipigia mahesabu kisije kupita kabla hajavuta mpunga wao. Kuwe na mpanggo wakuzuia akutozuia uchaguzi hayo ni maswala ya chama nyie nendeni mkakijenge chauma kama kitaimarika na sisi tutakuja huko nia yenu si kushiiriki uchaguzi muiondoe madarakani CCM na sisi sote nia yetu ndiyo hiyo hiyo kwahiyo mkifanikiwa ndiyo furaha yetu.Lakini najua nyie ni janja janja tu hakuna nia ya dhati nia yenu nikufanya biashara yakisiasa ,mpaka sasa tunajua Chama cha upinzani kimebaki kimoja tu hivyo vingine vyote ni mapandikizi. Hamuwezi kuitikisa CDM .Mtaondoka na njaa zenu mkiona kugumu mtarudi wenyewe.ACT kimesima baada ya CUF makini kuamia huko.kwa mfano Kundi la Lisu lingeamia Chauma Chauma kingesimama ila kundi la Mbowe haliwezi kufanya kitu hilo kundi limewaumiza wanachama wengi sana makini.
 
Sababu za kuondoka wameshazisema, ndio nauliza watapohamia na kushiriki uchaguzi wataikosoa chadema ili wapate kitu gani?
Hakuna chama kinachoitwa upinzani bali vyama vyote ambavyo vinataka kukiondoa chama tawala ni vyama vya upinzani. Hivyo vyama vitafanya uamuzi wa kushindana au kuungana dhidi ya yule uliyemuita common enemy. G-55, Chauma, Act Wazalendo na wengine watakuwa na haki ya kuikosoa Chadema wakati wanaomba kura.

Amandla...
 
Atakayebaki Chadema ndiyo royal kwa Lissu na uongozi aendelee nao. Chadema imepikika wamebaki wanaotembea na wananchi. Hii ni hatua nzuri ya kuimarisha chama upya
Hio ndio objective loyality kwa mtu na sio mawazo na core values za fikra zenu kwa umoja wenu ? i.e. Ideology
 
Hakuna chama kinachoitwa upinzani bali vyama vyote ambavyo vinataka kukiondoa chama tawala ni vyama vya upinzani. Hivyo vyama vitafanya uamuzi wa kushindana au kuungana dhidi ya yule uliyemuita common enemy. G-55, Chauma, Act Wazalendo na wengine watakuwa na haki ya kuikosoa Chadema wakati wanaomba kura.

Amandla...
Hujajibu swali watakua wanaikosoa ili wapate nini? Wabunge wa ccm utawashinda kwa kuikosoa chadema?
 
Benson Kigaila ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara amesema yeye na Wanachama wenzake wamejitoa katika chama hicho kutokana na kutoridhishwa na yanayoendelea

Ametangaza uamuzi huo akiwa pamoja na aliyekuwa Makamu wa CHADEMA Taifa - Zanzibar, Salum Mwalimu, aliyewai kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Catherine Ruge, John Mrema na Julius Mwita

View: https://www.youtube.com/live/Z_apgr0qkZM?si=Lj9DabbYPf6LP8KC

View attachment 3326774
===

Updates

Katika mkutano huu na waandishi wa habari wajumbe wote wa sekretarieti ya CHADEMA Taifa iliyopita wapo isipokuwa watu wawili ambao ndiyo hawakuwepo hapo kwa mujibu wa John Mrema. Ambao ni;
  • Catherine Ruge - Aliyekuwa Katibu Mkuu BAWACHA-Taifa
  • Julius Mwita - Aliyekuwa katibu wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa
  • John Mrema - Aliyekuwa Mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano, uenezi na mambo ya nje
  • Salum Mwalimu - Aliyekuwa Naibu Katibu mkuu CHADEMA, Zanzibar
  • Benson kigaila - Aliyekuwa Naibu katibu mkuu CHADEMA, Bara
Wanaeleza kuwa baada ya ushindi, Freeman Mbowe alikubali maridhiano yawepo mara baada ya makundi yaliyopo wakati wa kampeni, ila walishangazwa na kumuona aliyeshinda nafasi ya Uenyekiti Tundu Lissu aliendelea kumshambulia Freeman Mbowe kama vile kampeni bado zinaendelea, ameeleza Benson Kigaila.
View attachment 3326841
Kigaila anaendelea kueleza kuwa Kuna makundi ngazi ya chini kwenye chama wana vikao vya kuwaengua ama kuwafuta uanachama wanachama waliokuwa wanamuunga mkono Freeman Mbowe.

Wanaeleza pia kuwa ndani ya Chama kuna udikteta uchwara na hivyo wapo kwa ajili ya kuupinga udikteta huo ndani ya chama. Aidha hakuna haki ya kusikilizwa ndani ya chama wala hakuna haki ya watu kuhoji na wanaofanya hivyo wanaitwa wasaliti, njaa. Wanahoji Je, kati ya wao na aliyepinga maridhiano chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe nani msaliti?

G-55 wanasistiza kama unataka kuzia uchaguzi na hakuna mkakati wa kuzuia uchaguzi maana yake umeamua CCM wapite bila kupigwa.

Rasmi wamesema wamejiondoa CHADEMA lakini hawatokwenda CCM, muda ukifika wataeleza ni wapi wanapohamia. Sababu kubwa ni kutokutaka kuwa sehemu ya kifo cha CHADEMA kutokana na yanayoendelea. Hayo yamesemwa na Benson Kigaila aliyekuwa Naibu katibu mkuu Chadema (Bara)
View attachment 3326835

Soma pia:

Chawa wapo kila kona yani 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom