Baadhi ya marais wenye elimu kubwa Afrika, Rais Magufuli ashika namba tano

Baadhi ya marais wenye elimu kubwa Afrika, Rais Magufuli ashika namba tano

Rich Pol

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2013
Posts
7,874
Reaction score
5,685
Sio tu kwamba wana madaraka makubwa ya kisiasa nchini mwao, bali wana elimu kubwa kwenye fani mbalimbali jambo linalothibithisha usemi wa Kiingereza wa “readers are leaders,” yaani viongozi ni watu wenye hulka ya kusoma sana.

Hii ni orodha ya wakuu wa nchi za Afrika wenye elimu kubwa zaidi. Orodha hii ni kutokana na ukubwa wa elimu ya kila mmoja:

Mfalme Mohammed VI (Morocco)

Huyu ni kiongozi wa kwanza kwenye orodha hii; Mohammed wa sita ni Mfalme wa Morocco aliyeshika nafasi hiyo tangu mwaka 1999.

Alimaliza masomo yake ya elimu ya msingi na sekondari katika Shule ya Kifalme nchini Morocco.

Baadaye alipata shahada yake ya kwanza ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Mohammed (V) kilichopo Agdal. Ana cheti Elimu ya Juu kwenye fani ya Sayansi ya Siasa.

Alipata shahada ya uzamivu (PhD.) katika Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nice Sophia Antipolis kilichopo nchini Ufaransa.

Dkt. Peter Mutharika (Malawi)

Dkt. Peter Mutharika ni Rais wa Malawi. Alipata shahada yake ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha London nchini Uingereza na akaendelea na masomo na kupata shahada ya Uzamili (Master) ya Sheria na shahada ya Uzamivu (Ph.D) Sayansi ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani. Pia, Rais Mutharika ni mtaalamu wa Sheria ya Uchumi wa Kimataifa na Katiba.

Alassane Ouattara (Ivory Coast)

Alassane Dramane Ouattara ni Rais wa Ivory Coast tangu mwaka 2010. Alihitimu shahada ya Sayansi Chuo Kikuu cha Drexel kilichopo Philadelphia jijini Pennsylvania, Marekani. Aliendelea na masomo na kupata shahada zake za Uzamili (Master) na Uzamivu (Ph.D) ya Uchumi kutoka chuo Kikuu cha Pennsylvania nchini Marekani. Mwaka jana alichaguliwa kuongoza muhula wa pili wa miaka mitano.

Dkt. Mulatu Teshome (Ethiopia)

Anakaa kwenye nafasi ya nne katika orodha hii. Dkt. Malatu Teshome amekuwa Rais wa nchi ya Ethiopia tangu Oktoba 7 mwaka 2013 baada ya kuchaguliwa na idadi kubwa ya wabunge. Teshome alisoma nchini China ambapo alipata shahada ya Falsafa ya Siasa ya Uchumi wa Siasa na kisha kupata shahada ya Uzamili na Uzamivu katika Sheria za Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Peking.

Dkt. John Pombe Magufuli (Tanzania)

Alipata shahada yake ya Sayansi kwenye masomo ya Ualimu kwenye masomo ya Kemia na Hisabati kama masomo yake ya kufundishia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1988. Pia, alihitimu shahada za Uzamili, mwaka 1994 na Uzamivu mwaka 2009 katika somo la Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais Magufuli alisoma Elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Chato kuanzia mwaka 1967 mpaka 1974 na kwenda Shule ya Seminari ya Katoke iliyopo Biharamulo kuanzia mwaka 1975 mpaka 1977 alipohamia Shule ya Sekondari ya Lake mwaka 1977 na kuhitimu mwaka 1978. Alijiunga Shule ya Sekondari Mkwawa kwa elimu ya juu ya Sekondari mwaka 1979 na kuhitimu mwaka 1981. Mwaka huo huo alijiunga na Chuo cha Elimu Mkwawa na kusomea Diploma ya Elimu ya Sayansi kwenye masomo ya Kemia, Hisabati na Ualimu.

[Dkt. Ameenah Gurib (Mauritius)

Dkt. Ameenah Gurib-Fakim ni mwanamke wa kwanza nchini Mauritius kuwahi kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo. Aliingia madarakani mwaka 2015 akiwa ni Rais wa sita wa Taifa hilo.

Alihamia nchini Uingereza na kusoma katika Chuo Kikuu cha Surrey. Alipata shahada ya Sayansi ya Kemia mwaka 1983. Aliendelea na masomo na kupata shahada yake ya Uzamivu ya “Organic Chemistry” kutoka Chuo Kikuu cha Exeter.

Robert Mugabe (Zimbabwe)

Robert Mugabe ameiongoza Zimbabwe tangu nchi hiyo ilipopata Uhuru mwaka 1980. Alianza kwa kuwa Waziri Mkuu kwa miaka saba ya mwanzo, ambapo ilipofika mwaka 1987 mpaka sasa amekuwa ni Rais wa nchi hiyo kwa miaka yote hiyo. Viongozi wa Mataifa ya Magharibi wanasema kwamba Mugabe ni miongoni mwa viongozi makatili zaidi duniani. Lakini ambacho watu wengi hawakijui ni kwamba yeye ni msomi wa hali ya juu pia.
Huu ni muhtasari wa elimu yake: Shahada ya Uzamili ya Sheria (LL.M.), Shahada ya Uzamili ya Sayansi (M.Sc), Shahada ya Elimu (B.Ed), Shahada ya Uongozi (B.A.A) na Shahada ya Sanaa (B.A.)

Source swahili times
 
Nanukuu andiko kama ilivyoandikwa na Ben Saanane.

Kuanzia nilipoibua mjadala wa Uhalali wa Phd ya Mhe.Magufuli niliacha rasmi kumu-address kama Dr.Magufuli na kutumia Ndugu au Mheshimiwa tu hadi itakapothibitika ni Halali.

Nimesoma Hoja ya Prof.Kitila kuhusu PhD ya Magufuli.

Prof.Kitila ni Rafiki yangu sana.Yeye ni kaka yangu na ananichukulia kama mdogo wake.

Katika Kuchangia Mjadala wa PhD ameandika "UDSM hakuna namna mtu kupata Cheti Fake na huwa hatuangalii sura ya Mtu...". Kwa hiyo. .. "PhD ya Magufuli haina kasoro".

Vilevile kuna watu Mwanzo walisema masuala ya Machapisho hayana maana lakini cha ajabu wameweka waliyoita Machapisho ya Magufuli na pia kuweka Picha akiwa amevaa mavazi ya Graduation kama vile ndio Authentificatio
n ya PhD ya Magufuli.

Wengine wakaanza kusema Rombo ina matatizo hivyo niachane na PhD ya Magufuli.Utadhani kuhoji uhalali wa PhD ya Magufuli ndio kumeleta madhara Rombo.Wasomi wetu wengine wakoje?

Nataka kugusia hoja ya Prof.Kitila kuhusu kuwa hakuna namna ya kufanya Udanganyifu UDSM .

1-Prof.Kitila anaweza kuwa Mwaadilifu sana katika kusimamia taaluma na kazi yake kama Mhadhiri Chuoni.

Lakini ni kosa kubwa ku-assume kila mtu ni mwadilifu.

Tukienda hivyo tutaua nchi na ndio maana wengine tunasizitiza sana Kuimarisha Taasisi zetu na mifumo.

Hapo ni kama vile ku-assume kuwa kila mtu ni mpigaji.Hivyo tunasizitiza haja ya kuimarisha taasisi na mifumo ambayo itadhibiti mafisadi na watu wasio waadilifu baadala ya ku-assume kila mtu ni mtakatifu .

Kama watu waliweza ku-forge documents Serikalini na Kuchota Fedha Za EPA au ESCROW ni mechanism gani itakayozuia PhD za Mbeleko vyuoni kwetu hasa zinazohusu wanasiasa?

Tena katika mazingira yanayoashiria mbeleko kwa Mbebaji kumshusha aliyembeba nae akambeba kwa kumteua kushika ujumbe wa Bodi?

2-Kama Seif-Al Islam Mtoto wa Ghaddafi alikuja kuibuliwa kwa kashfa ya kuhonga na kupata PhD ya mbeleko Kule London School of Economics(LSE) sass UDSM ina mfumo gani thabiti wa kuepuka fraud kuliko LSE?

Kwa Mujibu wa Academic Perfomance Center chuo kikuu cha London School of Economics kilishika nafasi ya pili kwa miaka kadhaa mfululizo kwa ubora duniani wakati UDSM ikishika nafasi ya 1618 kati ya Vyuo 2,000.

LSE iko vizuri kiteknolojia na kitaaluma katika kuzuia academic Misconduct kuliko UDSM lakini bado Seif Al-Islam alifanya.

3-UDSM imewahi kukumbwa na staff waliofanya Udanganyifu kwenye taaluma na Prof.Maboko aliwahi kuutangazia Umma.

UDSM hii hii imeshawahi kutoa wanafunzi waliofanya udanganyifu na baadhi yao kuvuliwa Degree zao.

Charles I . Ng'imba aliwahi kuvuliwa Digrii yake aliyoipata kwenye Graduation ya Tarehe 29 August ,1987.

Unasema haiwezekani?
4-Kuna hao walioleta machapisho waliodai ni Ya Magufuli na kudai kuwa alistahili PhD kwa sababu alishaandika tangu 2003.

Tena nimeona ameshirikiana baadhi na huyo Supervisor wake.
Sasa watuambie alifanya PhD by Publication?

Sweden ,Australia na hata Uholanzi(Najua Unafahamu) inaruhusiwa PhD by Publication.

Kwa faida ya mjadala tu: Ni kuwa PhD by Publication zinakusanywa paper zote na kuziandikia Covering Essay na jumla na paper iwe na maneno si chini ya 20,000 ikiwa condition na masharti mengine ya submission yapo constant.

Pia inazingatiwa ni paper ngapi umeandika mwenyewe na ni ngapi umeshirikiana(Co-Author).

Na katika kushirikiana ni ipi jina lako limekua la kwanza maana inabeba uzito wa synopsis.

Sasa Katika hizo Paper alizoweka the so called (Dr.!?) Chahali ni Tatu tu anazooneshwa kaandika yeye na zipo kwenye vijarida vya uchochoroni tu sio kwenye respectable Journals huko.

So swali la PhD Candidate huyu kuipata PhD kwa miaka 3 akiwa Part time Candidate kinyume na Prospectus halijajibiwa.

Ingawa Prof.Kitila umetoa maoni yako tu kama mchangiaji na Sio Authority ya UDSM au Supervisor wake(Ofcourse hawezi kujitokeza tena maana ni mteule wa Bodi) lakini naheshimu maoni yako uliyotoa kistaarabu bila matusi kama hao waliomtetea kwa vitisho na matusi kwa hoja zao za kula nae Canteen au kumuona amevaa vazi la graduation.

UDSM kama vilivyo vyuo vingine au taasisi nyingine nchini haina kinga thabiti dhidi ya Academic Fraud hasa zinazohusisha wanasiasa na vigogo serikalini.Hiyo hoja haijaleta uzito wa kutosha katika authentification ya PhD ya Mkuu wetu.

Tena nilicheka sana nilivyo-imagine jinsi kazi ya Literature Review ya Mkuu wetu ingefanana. With knowledge that Examiners may tolerate grammer idiosyncratic than any other mess.Sijui Lugha na VIVA ilikuaje. Don't joke! Ile lugha yake ile ...! Haya!

Hoja ya Prof.Buchweshwaija kuwa co-author kwenye paper yake kisha kuja kuwa Supervisor wake na kisha kuja kuwa mteuliwa wa Waziri aliyeteuliwa na yeye mwanafunzi wake tunaweza kuli-debate left-right-center hasa tunapoangalia mfumo wetu wa elimu na uadilifu.

Ofcourse nakiri kuwa wakati wa kuanza PhD yangu niliwahi kukuambia nilipata headache sana kuhakikisha kuwa napata Supervisor maahiri ndani yawanakamati.Maana uliwahi kufanya mchakato wa kujiunga na chuo hicho kabla hujajiunga Southampton University kwa PhD yako.

I knew as PhD candidate,Institution'll gain through my presence by gaining credibility,profile and funding. Why should I allow them to treat me as an inconvinient ,Incompetent fool? Si lazima nami niwe smart kujilinda?

So kwa Case ya Magufuli na SUP wake twaweza kui-debate kweli kuanzia co-authorship.

Sijui independence ya Mwanafunzi huyo ilikuaje hata kama ilikua ni Ph.D by Publication.

Ni vyema tu akajitokeza kutoa ufafanuzi au Chuo .Mbona lile la silaha alipohakiki hadi watu wengine walikua proud kuiweka picha yake na bastola kama Profile ya groups za Watsap?
 
Back
Top Bottom