Baadhi ya Viwanda vya kimkakati alivyoanzisha Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambavyo ni magodauni na magofu

Hiyo haikuwa sababu toshelezi kuamua kuvitupa shimoni. Ni bora wangetafuta ushauri wa aliyevijenga kwanza pamoja na kupata ushauri wa waliofadhili ujenzi wake kuliko walichokifanya.

..Mwalimu Nyerere alikuwa anajadiliana na IMF, World Bank, na Paris Club [ nchi wakopeshaji wakubwa.]

..Mzee Mwinyi alipoingia aliendeleza mazungumzo na nchi na taasisi hizo kuhusu namna ya kutukopesha na kusamehe baadhi ya madeni.

..Majadiliano hayo ndiyo yaliyopendekeza zoezi la Ubinafsishaji. Baada ya hapo sheria ilijadiliwa BUNGENI na kupitishwa.

..Ubinafsishaji ulifanyika baada ya mashauriano, mazungumzo, na mijadala mipana na mikali wakati mwingine.
 
Sasa kwanini walishindwa kusimamia hilo zoezi liwe na Tija kwa Taifa? Badala yake wakalitumia kujinufaisha wao pamoja na familia zao? Inasaidiaje Taifa kuja kukiri baadaye kwamba hukulisimamia vyema hilo zoezi wakati ilikuwa ni wajibu kama Mkuu wa nchi? Na kwanini ukubali kuuwa vyoote kwa pamoja kipindi kimoja.Why not plan such a dangerous and unpredictable move in phases? Ili kujiridhisha baada ya kuchunguza katikati ya utekeleza kwamba uamuzi unafaa kuendelea au la? There is no excuses brother! That was a deadly mistake.
 
Jiwe yeye alijenga kiwanda kipi ati!?

Au kiwanda Cha Hawa mazuzu wanamtukana Samia na January kila kukicha!?

Mzee alikuwa msanii yule!
 

..kwanza sio kweli kwamba ubinafsishaji haukuwa na tija.

..pili sio kweli kwamba ubinafsishaji uliua viwanda.

..tatu zoezi lilifanyika kwa muda mrefu na kulikuwa na muda wa kutafakari, kushauriana, na kupima matokeo.

..kwa maoni yangu, ubinafshaji ulichelewa kufanyika, matokeo yake tukawa tunabinafsisha viwanda vilivyokufa.

..Zipo taarifa kwamba wataalamu toka SWEDEN waliishauri serikali ya awamu ya kwanza kuendesha viwanda kwa ubia ili kuviokoa lakini wazo hilo lilikataliwa.
 
Sahvi kuvirudisha shuguli maana
Wale importers wanaleta zengwe
Wanataka nchi iendele kuimport tu..

Ova
Nyie matahira simnasema mungu wenu alijenga viwanda elfu tatu na Mia kenda!!? Vipo wapi hili tuvione au kuviona mpka tuwe na jicho la kiroho
 
NBC nakumbuka kama iliuzwa kwa billion 15 tu, na majengo yake yote.
 
Umesahau na kiwanda Cha MOPROCO
 
... Mkapa ndiye aliyekuja kuvigeuza magodown kwa kilichoitwa ubinafsishaji.
Yeye mwenyewe alikuwa analalamika kuwa wawekezaji wa ndani wanavililia halafu wakipewa wanavigeuza magodown. Wakinyang'anywa na vikapewa wawekezaji wa nje wanalalamika kuwa kwanini serikali haina uzalendo.
 
Mkapa aliviua vingi kwa kuviuza ovyoovyo na vingine kuwagawia wahuni.
Nakumbuka nyerere alishauri wabinafsishe viwanda vyenye kufanya vibaya tu ili vipate uwekezaji na ujuzi kutoka nje. Mabwanyenye na adui wa ujamaa wakataka vile vinavyofanya vizuri ndio wauziwe. Mkapa kwa ulevi tu akageuza nchi kuuza viwanda vyake vyote. Mabeberu wakanunua na kuvigeuza magodauni ya kuweka bidhaa kutoka viwanda vyao ng'ambo.
Hakika ilikua makosa makubwa yasiyo kifani kuhusu jitihada ya kujenga viwanda. Nakumbuka enzi hizo vijana wengi wakifanya kazi viwandani.
 
Kiwanda Cha nyavu nafkiri kinapakana na UFI.
DarBrews -Chibuku au siyo Cha Nyerere kile?
 
Unasema kwamba General Tyre haikuwa na ubora?
Au Khanga ya urafiki haikuwa na ubora?
Aiseee....
 

..tujiulize ni viwanda vingapi vilikuwa vinafanya vizuri?

..kiwanda gani kilikuwa kinaendeshwa kwa faida na kinatoa gawio serikalini?

..pia tujiulize viwanda vingapi vilikuwa vinafanya vibaya na vimekuwa mzigo kwa serikali.

..mwisho, tujiulize kwa ujumla viwanda vilikuwa vinaendeshwa kwa faida? Vilikuwa vinatoa gawio serikalini? Au vilikuwa mzigo na vikitegemea ruzuku toka serikalini.
 
Kuuliza kiwanda/viwanda gani vilikuwa vinatoa gawio au vinafanya vizuri haitoshi kusaidia km uamuzi wa kuviuza ulikuwa sahihi au la, nadhani walikosa hekima kujaribu kuona mbali hatua kwa hatua kuvipatia majibu changamoto zilizokuwa kiini cha kutofanya vizuri, vingi vilikuwa na matatizo ya mtaji, ujuzi na teknolojia..kwa rasilimali tulizo nazo, hasa madini..kupata majibu ya hayo matatu si vigumu kabisa.
Kwa kifupi waliamua vibaya, tena walikuwa na haraka na kosa lile lile ambalo hadi leo bado wanalirudia rudia kulifanya..mentality ya kudhani ndani ya serikali kuna majibu ya changamoto yoyote na hivyo kutohitaji majibu nje ya serikali..tabia hii haifai ni ya kukumbatia umaskini.
 

..ubinafsishaji maana yake ni kufikabidhi viwanda kwa private sector huwezi kusema huko ni kutafuta majawabu serikalini.

..vijana hamjui nchi ilikuwa na hali gani kiuchumi, na matatizo ya fedha serikalini yalikuwa makubwa kiasi gani.

..Kwa kifupi nchi ilikuwa imekwama wakati Mwalimu Nyerere anang'atuka. Kulikuwa hakuna mahali tunaweza kupata fedha za kufufua hivyo viwanda. Nchi ilikuwa haikupesheki.

..Kujinusuru na nchi kuwa kama Zimbabwe au Sri Lanka tulilazimika kukubali masharti na maelekezo ya IMF, WB, na wakopeshaji wa Paris Club.


..Kwa hiyo ubinafsishaji ulitokana na sisi wenyewe kushindwa kuendesha uchumi wetu vibaya, hali iliyopelekea uzalishaji viwandani kuporomoka.

..Uamuzi wa kuviuza ulikuwa ni sahihi kwasababu tulikuwa hatuna uwezo wa kifedha kufufua viwanda vyetu.
 
Hiyo siyo sababu ya uamauzi na utekelezaji hafifu namna ile bila kujali Taifa. Nikuulize swali, TANESCO ilikuwa inaliingizia nini Taifa? Kwanini hiyo hawakudhubutu basi kuibinafsisha?
 
kwa vyovyote vile vitapaswa kurudishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…