Mzee Wa Republican
JF-Expert Member
- Jul 20, 2013
- 1,666
- 847
Ubinafsishaji wa Tanzania Breweries kwa kiasi kikubwa nawezakusem umefanikiwa...ukweli ni kwamba tulianzisha viwanda lakini tuliviendesha vibaya na kilichotuponza ni siasa za Ccm kuingilia utendaji.
..pia wapo viongozi ambao walimshauri Mwalimu Nyerere atafute wabia, na wawekezaji, ktk viwanda na mashiriki, lakini ushauri huo ulipingwa, na walioutoa waliitwa WASALITI wa Ujamaa.
..Kosa letu lilikuwa kuchelewa kubinafsisha tukajikuta tunafanya hivyo wakati viwanda vimekufa.
NB:
..Ubinafsishaji wa Tanzania Breweries ulipingwa sana. Watu walikasirika kwasababu aliyeuziwa ni KABURU.
..lakini wakati Breweries inabinafsishwa bia zilikuwa haba. Quality ya bia ilikuwa mbaya, wakati mwingine bia zilikuwa na uchafu. Kampuni ilikuwa imekwama ktk ujenzi wa kiwanda cha Mbeya.
..Tanzania Breweries ni moja ya makampuni ambayo yalibinafsishwa at the right time, to the right investor.
Je, kuna ubinafsishaji mwingine wa viwanda uliofanikiwa kama wa TBL ?
Tuna mkwamo wa kitaifa aisee usikatae