Baadhi ya Viwanda vya kimkakati alivyoanzisha Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambavyo ni magodauni na magofu

  • Kiwanda cha nyembe Perma Sharp
  • Kiwanda cha magunia - Tanzania Bag Corporation (hivi vilikuwa viwili kwa pamoja MILL I na MILL II)
  • Viwanda vya Sukari TPC na Kilombero
  • Kwanda cha mafuta - MAPROCO Morogoro na kingine cha Mwanza/Shinyanga nimekisahau jinakilichokuwa
kinatengeneza mafuta ya Tanbond na Supa Ghee
- Kiwanda cha baiskel - Swala
Sahv magunia tuna import
Na viwanda kufa kumewafanya
Wafanyabiashara fulani kuwa mabilionea

Ova
 
  • Kiwanda cha nyembe Perma Sharp
  • Kiwanda cha magunia - Tanzania Bag Corporation (hivi vilikuwa viwili kwa pamoja MILL I na MILL II)
  • Viwanda vya Sukari TPC na Kilombero
  • Kwanda cha mafuta - MAPROCO Morogoro na kingine cha Mwanza/Shinyanga nimekisahau jinakilichokuwa
kinatengeneza mafuta ya Tanbond na Supa Ghee
- Kiwanda cha baiskel - Swala
Dah ! Swala nimenyonga sana kipindi niko standard two natumbukiza mguu kwenye tobo long time sana na vile viti vyake vipana
 
Iko hivi. Viwanda vingi havikuwa vinajiendesha kwa faida. Serikali ilikuwa ina vipa ruzuku ili viendelee kuwepo. Kuna sababu mbalimbali ambazo zilisababisha haya.
Haswaa!
Asilimia kubwa ya hivyo viwanda vilikuwa ni hasara tupu.
Sababu nyingine ilikuwa mkuu akiharibu kwenye taasisi moja Nyerere anamuhamishia nyingine. Mwinyi akaleta Ruksa, hali ikawa mbaya zaidi.

Na Mkapa naye badala ya kurekebisha mapungufu, akagawia Mafisi
 
Kabla haujambebesha lawama Mh. Mkapa ni vyema ukaangalia sababu ambazo zilimfanya Mkapa kufikia hatua hiyo.

Iko hivi. Viwanda vingi havikuwa vinajiendesha kwa faida. Serikali ilikuwa ina vipa ruzuku ili viendelee kuwepo. Kuna sababu mbalimbali ambazo zilisababisha haya.
1. Management Mbovu. Wabongo tunajijua. Pamoja na kwamba Nyerere alijitahidi kusomesha watu na kuwapa nafasi..wengi walimuangusha.

2. Technolojia iliyopitwa na wakati. Baadhi ya viwanda alikuwa anapewa msaada...vilikuwa vimeshapitwa na wakati. Kumbe wale jamaa walikuwa wanatafuta sehemu ya kuvitupa. Wao wana move kwenye tech mpya ile ya zamani ndo wanawa wapa au kuwauzia. Hivyo ilikuwa gharama kubwa kuviendesha na havikuwa na ubora kama vya ulaya. Hivyo kufanya kutokuwa na ushindani katika soko. Maana una produce low quality at high cost.

So kipindi cha Mwinyi vingi ya hivyo viwanda vilifungwa. Hali ilikuwa mbaya sana. Watu walikaa nyumbani huku wakiendelea kulipwa mishahara.

Mkapa alipokea nchi ikiwa namna hiyo. Yaani una watu wako nyumbani wanalipwa mishahara. Una viwanda ambavyo havifanyi kazi na technolojia yake imepitwa na wakati.

Je utafanya nini.?

Mkapa aliamua kuvibinafsisha. Kwa sababu ni dhahiri serikali haiwezi kuendesha miradi ya kibiashara. Angali tu kwa mfano Mabasi ya Mwendo kasi, Angalia Tanesco etc..zote zinaendeshwa kwa ruzuku.

Sasa kwa nini uchukue gela ya walipa kodi uvipe viwanda visivyoingiza faida.?

Hivyo Mkapa akaamua kuvibinafsisisha. Ili private investors waendeshe na watoe ajira. Akawapunguza wafanyakazi kwa kuwalipa haki zao ili wasiendelee kula mishahara bila kazi.

Kuna tuhuma kwamba Mkapa aliuza viwanda kwa bei rahisi bei ya kutupa. Ukweli ni kwamba ingawa vilikuwa vinaitwa viwanda...havikuwa viwanda kiuhalisia. Mitambo yake mingi ilikuwa ya kizamani na haifanyi kazi. Hivyo Mkapa aliuza vyuma chakavu na majengo.

Baadhi ya walionunua walifanya vizuri..Viwanda kama TBL vinafanya vizuri hadi sasa. Ila baadhi ya walio nunua walivigeuza ma godown na wao ukiwauliza kwa nini hawakuviendeleza wana sababu zao.
Mkapa kubinfsisha haikua tatizo..Ila mikataba ya kimangungu ndiyo tatizo
 
Kuna sehemu naweza kukubaliana na wewe na sehemu nyingi si kweli, kwa sababu kuna baadhi vilinunuliwa vikaendelea kwa muda na waliouiziwa leo hii ni mabilionea. Vingine walionunua walifungua ile mitambo wakasafirisha nchi jirani mitambo ikaendelea kufanya kazi wakazalisha wakatuletea bidhaa kwa bei ya juu au ya chini kidogo kutokana na kuzalisha kwa wingi. Hii inamaanisha nini? Kwanini na yeye akajimilikisha Mgodi wa Makaa ya mawe? Inaonyesha wazi kulikuwa na ubadhirifu wa hali ya juu.
 
Mkuu Mkapa ndie alieuza NBC ikiwa ndio benki kubwa ya biashara.
Aliuza bank na majengo yake nchi nzima kwa bei ya kutupa,
Fedha kidogo iliyopatikana ndio iliyoanzisha NMB
Baba wa taifa alipinga sana lakini hakuwa na sauti tena, Mkapa allimweka mwenyewe, kibaya zaidi akawauzia makaburu ambao aliwapiga vita muda mrefu
Hili jambo la kuiuza NBC lilimuuma sana Mwalimu... Benki ilikuwa na mtaji mzuri kabisa lakini iliuzwa kwa bei ya kutupwa...
 
Back
Top Bottom