Baadhi ya Viwanda vya kimkakati alivyoanzisha Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambavyo ni magodauni na magofu

Nimesema vingine vilikuwa na matatizo ya uongozi (Management), Vingine Technolojia na vingine yote mawili.

Ndo maana vipo ambavyo waliovinunua waliviendeleza kwa faida.

Vingine waling'oa vyuma chakavu wakabaki na magodown.

Hii ya kupeleka mitambo na mashine nje sina reference yoyote..hivyo siwezi kubiasha au kukataa. Lakini all in all watakuwa wameangalia mazingira ya biashara..maana at the end mwekezani anataka faida
 
Hivi ni tanzania tu ndo kulikua na viwanda vya zamani?.Au ni tanzania tu ndo serikali ilikua inamiliki viwanda?.Mambo yote hayo uliyoyataja yalisababishwa na uongozi mbovu wenye ubinafsi na kutokujali maslahi ya nchi.Tungekua na viongozi makini hivyo viwanda vingekuwepo hadi leo.
 
Namba 20.kiwanda kilikuwa kinaitwa TAMCO...
 
afu kuna jamaa akatu fix kwamba ati anaitengeneza Tanzania ya viwanda wakati kumbe viwanda vilikuwepo tena vingi tu miaka ya 70 na 80 ila uzembe wetu wenyewe.

Akaishia kutupatia viwanda wa vyerehani mbili mbili za darizi - afu katoka nduki.
 
Hivi kiwanda kama TIPER, au cha Unga kinawezaje kufa? Kinawezaje kufilisika? Kwa kweli haiingio akilini?
 
Hatuvihitaji kwani kuendesha viwanda ni aghari sana kuliko kuwaacha wamachinga wafanye biashara barabarani ili kuinua uchumi wetu.
 
Umeeleza vizuri sana mkuu, wabongo tunapenda sana kulalama bila kujua sababu.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Usiwalaumu siajabu Kuna wengine hawajui hayo wamemezeshwa mazuri tu

..mnamsingizia Nkapa kuwa aliua viwanda.

..Waziri Mkuu Sokoine aliwahi kutembelea mikoa ya kusini akakuta wananchi wanavaa kaniiki.

.Sasa kama viwanda vya nguo vya Nyerere vilikuwa vinazalisha kwanini wananchi walilazimika kuvaa kaniki?

..Hapo kuna maana moja tu kwamba viwanda vilikuwa vimekufa au vimedorora tangu wakati wa Mwalimu.

..Pia maeneo ya mijini kila wakati kulikuwa na kurupushani za mgambo na JKT kukamata wazururaji na kuwapeleka wakalimu. Hali hiyo ilisababishwa na tatizo la ukosefu wa ajira. Kama viwanda vingekuwa vinazalisha na kutoa ajira tusingekuwa na tatizo la wazururaji enzi za Mwalimu Nyerere.

..Mwalimu alikuwa na nia njema kabisa kuanzisha viwanda. Lakini wakati wa utekelezaji wa nia hiyo tulikosea na kushindwa kukabiliana na changamoto za kukuza viwanda tulivyoanzisha.

..Kuna umuhimu wa kuambiana ukweli kuhusu viwanda vyetu vinginevyo hatutajifunza kutokana na makosa yetu.
 
Sasa hapo ni kwamba Baraza zima la Mawaziri kipindi hicho lazima liwe responsible
Kwa Katiba yetu si kweli,Baraza la mawaziri huwa wanapewa kujadili mipango Kama formality tu,rais na deep state yake wanakua washafanya maamuzi
 
Ongeza kiwanda cha matunda TANGOLD Korogwe Tanga (NMC)
 
Ila usichokijua ni kwamba waliotusaidia kuvijenga ndio walihamasisha kuviua.
 
Mkapa alikua sahihi kabisa. Serikali haiwezi kufanya biashara. Na Kama ikiamua kufanya biashara basi inabidi iwe na kiongozi katili sana kwa wanaoenda kinyume. Lakini kwa ujumla hali ya watz kutopenda kufanya kaz na ufisadi iliwaangusha sana mkapa na Nyerere sera zao zikawa zimefeli.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 

umeleta historia nzuri kwa vizazi vya sasa....wazee wetu walifedheeka sana na kuuwawa kwa viwanda hizi kwa ukosefu wa uzalendo na ubinafsi wa walielimishwa na kuamniwa na taifa hili
 
Ila usichokijua ni kwamba waliotusaidia kuvijenga ndio walihamasisha kuviua.

..kwa kiasi kikubwa viwanda vilikufa kwasababu ya tabia zetu za kijamaa-jamaa ktk kuviendesha.

..Viwanda vingi havikuzingatia kanuni za kibiashara ktk uendeshaji, na menejiment zilikuwa zikiingiliwa kimaamuzi na wanasiasa.

..kwa mfano, vipo viwanda ambavyo vilikuwa javizalishi ktk full capacity, lakini kwasababu ni kiwanda cha umma basi kililazimika kuajiri kana kwamba kinafanya kazi kwa asilimia 100.

..Mtu binafsi anapokuwa na biashara yake huajiri na kupunguza wafanyakazi kulingana na uzalishaji ktk mradi wake.

..Jambo lingine ni viwanda na mashirika kuwa na shughuli nyingi za ziada zisizohusiana na biashara husika. Kila chama kilipotoa tamko fulani viwanda na mashirika yalilazimika kuitikia au kutekeleza.

..Kwa mfano, baada ya chama / Ccm kutoa tamko kuhusu michezo na utamaduni makampuni ya mashirika ya umma yalianzisha timu za mpira, netiboli, bendi za muziki, vikundi vya ngoma, etc.

..Na shughuli zote hizo zilikuwa ni mizigo kwa mashirika na makampuni ya umma.

..Lingine ni mashirika na makampuni ya umma kushindana kutoa ufadhili kwa shughuli za chama/ Ccm. Kwa mfano, mashirika yalikuwa yanashindana kugharamia mkutano mkuu wa chama/Ccm, mkutano wa Nec, etc

..Jambo lingine lililoua viwanda ni URASIMU ktk uendeshaji wake. Kwa mfano kiwanda kilipohitaji kuagiza vipuli nje ya nchi kulikuwa na mlolongo mkubwa wa kiserikali kupata vibali na fedha za kigeni kuagiza toka nje. Mtu binafsi akihitaji kipuli cha kiwanda chake hufanya maamuzi ya haraka.
 
Viwanda vya kusindika nafaka NATIONAL MILLINGS vilikuwepo karibu mikoa yote huku bara !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…