Baadhi ya Viwanda vya kimkakati alivyoanzisha Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambavyo ni magodauni na magofu

Ubinafsishaji wa Tanzania Breweries kwa kiasi kikubwa nawezakusem umefanikiwa.

Je, kuna ubinafsishaji mwingine wa viwanda uliofanikiwa kama wa TBL ?

Tuna mkwamo wa kitaifa aisee usikatae
 
Zote hizi ni White elephant , Misallocotion of resources
 
Ubinafsishaji wa Tanzania Breweries kwa kiasi kikubwa nawezakusem umefanikiwa.

Je, kuna ubinafsishaji mwingine wa viwanda uliofanikiwa kama wa TBL ?

Tuna mkwamo wa kitaifa aisee usikatae

..TBL walifanikiwa kwasababu hawakusubiri mpaka kiwanda kife.

..Wangekibinafsisha wakati kimekufa na kwa muwekezaji asiye na uwezo kiwanda kisingeweza kushindana na waagizaji toka nje.
 
..TBL walifanikiwa kwasababu hawakusubiri mpaka kiwanda kife.

..Wangekibinafsisha wakati kimekufa na kwa muwekezaji asiye na uwezo kiwanda kisingeweza kushindana na waagizaji toka nje.
TBL tayari ilikuwa mahututi iCU..
Enzi hizo ukitaka kreti 10 unatoa Kwanza rushwa halafu unasubiri wiki, then unapata kreti pungufu!!

Kilichosaidia pale ni kuibinafsisha Kwa mwekezaji mwenye uwezo mkubwa wa mtaji na uzoefu, SABMiller ya Afrika Kusini
 
Laana ya Viwanda vya Nyerere haitataucha huru mpaka ipatikane Katiba mpya na wahusika wote kuchukuliwa hatua stahiki kisheria na ku-reclaim vile viwanda hasa ambavyo havikufufuliwa vinatakiwa virudishwe tuanze upya. Hatuwezi kukubali kukaa kama Taifa mfu lisilokuwa na sheria wala taratibu lisilokuwa na mikakati ya maendeleo yenye vipindi maalum vya kujipima mafanikio yake.
 
Viwanda vya kukoboa na/ au kusaga nafaka (Nationa Milling) vilikuwepo angalau kimoja kila mkoa
Vilisaidia nini? watu walikuwa wanapanga foleni kununua unga na wengine kula unga wa yanga , monopoly ya National milling ndio iliua ushindani na kufanya watu kutegemea serikali kila kitu
 
Mawazo ya kijima haya, haturudi na hatutaki monopoly za serikali kumiliki viwanda mpaka vya viberiti na kumuona mfanyabiashara ni muhujumu uchumi
 
Ubinafsishaji wa Tanzania Breweries kwa kiasi kikubwa nawezakusem umefanikiwa.

Je, kuna ubinafsishaji mwingine wa viwanda uliofanikiwa kama wa TBL ?

Tuna mkwamo wa kitaifa aisee usikatae
Kila kitu kilifanikiwa, ilipunguza zigo la kutoa billions kama ruzuku kwa viwanda vibovu visivyo na faida yeyote, ilikuwa kama serikali ina flush pesa chooni kila mwaka
 
Kila kitu kilifanikiwa, ilipunguza zigo la kutoa billions kama ruzuku kwa viwanda vibovu visivyo na faida yeyote, ilikuwa kama serikali ina flush pesa chooni kila mwaka
Baada ya kuuzwa pesa zikawa zinaflashiwa matumboni !! Waliokuwa wanatakiwa kuuzwa ni wale walioshindwa kuviendesha viwanda sio kuviuza viwanda !! Je na nyumba za serikali zilizouzwa nazo zilikuwa ni mzigo kwa Serikali ??!!
 
Ni kweli Mwalimu aliumizwa sana na kuuzwa kiholela kwa viwanda vile na akawaambia mtabinafsisha hadi magereza na bado mambo yatakuwa magumu tu !! Kweli kiongozi yule na mawaziri wake walitakiwa washitakiwe kwa yale waliyoyafanya !!
 
Vingi alijiuzia mwenyewe na kugawana na ndugu na marafiki kule Kiwira makaa ya mawe ndio walikomba live wakanunua jumla bei ya kutupa ,yeye na Mramba,na mwanae bila aibu
 
Vilikufa kidogo kidogo kipindi cha Mwinyi, halafu Mkapa ndo akaja akavipiga nyundo vyote vilivyokuwa vinapumua bado katika awamu yake.
Baada ya vita vya Uganda,World Bank na IMF.walitaka Tanzania ifanye reform za uchumi.
Raisi Nyerere akakataa masharti hayo yaliosababisha Waziri wa Fedha Edwin Mtei na mshauri wa uchumi Professor Rweyemamu kujizulu.
Baada ya Mwalimu kugeuka mbogo na Raisi Reagan wa Marekani akageuka kiboko.IMF na World Bank wakasitisha mikopo au hata misaada na wakazionya taasisi nyingine za fedha za nchi za magharibi kutoisaidia Tanzania .
Katazo hilo tokea IMF,World Bank lilisabisha uchumi wetu kuyumba sana,kukosekana kwa pesa za kigeni.Viwanda vyetu vikashindwa kuagiza vipuri toka nje na kusababisha viwanda vyetu vizalishe chini kabisa ya kiwango.
Lakini nchi za Danmark,Norway,Sweden na Finland zikazidisha misaada mingi ya maendeleo lakini bado haikutosha kukwamua uchumi wetu.
 
Vilisaidia nini? watu walikuwa wanapanga foleni kununua unga na wengine kula unga wa yanga , monopoly ya National milling ndio iliua ushindani na kufanya watu kutegemea serikali kila kitu
Kibaya kilikuwa nini nini? Idea au utekelezaji? Wazo la viwanda haliwezi kuwa baya hata siku moja. Tatizo tunapenda muno hujuma; kuhujumu Serikali halafu tunaanza tena kuilalamikia. Kama havikusaidia kitu basi ujue kulikuwa na hujuma; wazo la kiwanda haliwezi kuwa baya au kushindwa kuzaa matunda hata siku moja, haiwezekani

Kwa upande wako unaonaje katika hili? Bora aliyekuja kuviuza, si ndiyo? Vipi baada ya kuuzwa vimesaidia zaidi kuzidi kabla ya kuuzwa kwake?
 
..TBL walifanikiwa kwasababu hawakusubiri mpaka kiwanda kife.

..Wangekibinafsisha wakati kimekufa na kwa muwekezaji asiye na uwezo kiwanda kisingeweza kushindana na waagizaji toka nje.
Vingine kama MWATEX na MUTEX vilikuwa vinafanya kazi ila vimebinafsishwa zaidi ya miaka ishirini lakini hamna kitu mpaka sasa
 
Mawazo ya kijima haya, haturudi na hatutaki monopoly za serikali kumiliki viwanda mpaka vya viberiti na kumuona mfanyabiashara ni muhujumu uchumi
Tunachohitaji ni waliovichukua wahakikishe vinazalisha na kuchochea maendeleo ya Teknologia nchini badala ya kuvitumia kama warehouse za kufichia bidhaa haramu. Nadhani sasa utakuwa umeelewa vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…