Baadhi ya vyombo vya habari vya nchi jirani vinaeneza uongo, vichukuliwe hatua Kali

Baadhi ya vyombo vya habari vya nchi jirani vinaeneza uongo, vichukuliwe hatua Kali

kitu ninachoweza kukwambia ni kwamba hajafariki.
Unaweza kuniambia pia kwamba wewe ndiye Magufuli mwenyewe, lakini kama wewe si Magufuli, ukiniambia wewe ni Magufuli, kuniambia huko hakukufanyi uwe Magufuli.

Weka habari ambazo zinaweza kuwa independently verified.

Na mpaka sasa hujaweka habari zinazoweza kuwa independently verified kwamba Magufuli yupo hai.
 
Magazeti ya nchi moja jirani yanaandika habari za uongo na kusababisha taharuki, naomba mamlaka zinazohusika zichukue hatua stahiki.
Mfano People Daily online hasa la leo.

Ni wakati mzuri Sasa Watanzania tushikamane kuitetea nchi yetu.
Mbona unaandika kwa kupanick.Kwani wamesema nini.Kama unaogopa kusema si ungeacha kuandika humu. Wachukuliwe hatua na nani,kwa sababu gani, wamesema nini. Vyombo vya wenzetu viko huru usidhani wanazibwa mdomo na pua kama hapa kwako. Tena ukajisahau kabisa eti,wachukuliwe hatua,bila kueleza sababu hasa.Lakini pia kuna International Laws zinazowalinda. Wenzetu sio wabongo, wana uhuru wa kutoa habari. Midomo yao haijabanwa na makufuli kama hapo kwako. Subiri mahakama kuu.
 
Mimi kutoweka habari ambazo ni independently verified hakumfanyi magufuli kuwa amekufa au kuanza kuugua huko aliko.

lakini pia wewe kukosa ushahidi ulioonyeshwa na mimi,hakufanyi nilichokwambia kuwa uongo.
na kama utaamua kukataa, wala sitakuzuia kufanya hivyo.
 
Usijali atakujibu mpaka tumbo la uzazi likucheze. Si unajua alivyo na nongwa???
 
Ushikamane na nani, mlipoulawiti uchaguzi mkuu majuzi mnadhani wote tulifurahi. Usitutishe, kila mtu ashinde mechi zake.
 
Wewe kuwa huru au wao kuwa huru hakuwafanyi waandike chochote maadam wameshiba.
ndio maana hata hapa kwetu kuna udhibiti wa habari,sio kila habari inarushwa tu.

lakini kwakuwa mnawaangalia kama benchmark,hamfikirii kuwatahini.
 
Hata wakichukua mwendo mkali, haina maana ikiwa kama hawamuonei mtu. Wakiweka ushaidi ubaoni utatoka show
 
Sawa,

Kama Magufuli yupo hai, mzima, kwa nini inakuwa vigumu sana kumuonesha kwa kadamnasi, kusema huyu hapa rais mzima, watu waondoe shaka na uzushi wote uzimwe?
na ndio sababu hata Yeye na wasaidizi wake hawaoni sababu ya kufanya hivyo.
mtu kutoonekana wiki mbili basi anaumwa au amekufa na amelazwa nairobi!!!

wakati mwingine swali, aina ya uulizaji inaamua jibu.
 
Serikali ya TZ haipo kwa ajili ya kukanusha uongo..
Wananchi wa Tanzania wana haki ya kikatiba ya kujulishwa mambo muhimu yahusuyo mustakabali wa nchi yao.

Unaelewa hilo?

Unaelewa kwamba nchi ipo katika mtafaruku, rais hajaonekana hadharani wiki ya pili?

Unaelewa kwamba, kama yupo hai na ni mzima, ukimya huu unasababisha uzushi mwingi sana uenezwe bila sababu, na kumuonesha rais kuwa yupo hai na ni mzima kutamaliza uzushi huu mara moja?

Unaelewa kwamba kama rais anaumwa, wananchi wana haki ya kujulishwa rais wao anaumwa?
 
Kwanza kabisa, hujathibitisha kwamba yupo mzima na hajafa.

Kwa hiyo hizo habari za "yeye na wasaidizi wake hawaoni sababu..." ni habari za kusadikika tu zisizo na ushahidi hata kwamba yupo hai!
 
Mpaka sasa mleta habari, habari yake haina kichwa wala miguu, habari inaelea. Ameulizwa humu, hana majibu. Afadhali atuache.
 
Hujathibitisha kwamba yupo mzima na hajafa.
Nikithibitisha ni mzima wa afya na hajafa ili kukanusha taarifa za kukisia tu mtandaoni nitakuwa natumia nguvu kubwa sana kukuridhisha.
 
Nikithibitisha ni mzima wa afya,na hajafa,ili kukanusha taarifa za kukisia tu mtandaoni,nitakuwa natumia nguvu kubwa sana kukuridhisha.
Hizi si taarifa za kisiasa tu. Nchi ipo katika sintofahamu Rais yupo wapi.

Unaelewa kwamba wananchi ndio waajiri wa rais, na kama waajiri wana haki ya kujua muajiriwa wao yuko wapi na anafanya nini?
 
Back
Top Bottom