Nimetafakari jinsi Aljazeera walivyoripoti kwa uhakika kwamba JPM AMELAZWA INDIA KWA CORONA. Unaporipoti habari kubwa kama hii unapaswa uwe na vyanzo vitatu. Reliable, Credible na Authoritative source.
Credible source ni daktari anayemhudumia JPM. Reliable source anaweza kuwa Mhe.Lissu aliyeibua mjadala huu. Na Authoritative source anaweza kuwa Msemaji mkuu wa serikali, au Waziri wa habari, au Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu.
Lakini niliposoma nikakuta source pekee waliyotumia ni Tundu Lissu, which is reliable source. Hakuna Credible wala Authoritative source. Maana yake ni kwamba habari haijabalance. Aljazeera wameripoti kama Carrymastory.
Lissu anaweza kuwa reliable source yani chanzo cha habari cha kuaminika, lakini hiyo haitoshi. Tunapaswa kupata chanzo kutoka kwa madaktari wanaomhudumia (credibility) na serikali (authority). Hivyo ndivyo maadili ya journalism yanavyotaka.
Nimejiuliza hivi baada ya Aljazeera kuripoti hivi halafu JPM akajitokeza hadharani itakuaje? Je hawaoni watakua wameharibu reputation yao? Labda wana njia zao wamezitumia kujiridhisha kwamba kweli JPM yupo India ndio maana wakaripoti. Otherwise wasingeweza kujirisk kwa jambo kubwa hivi.
Hata hivyo Aljazeera wanadai wamehangaika kutafuta viongozi wa serikali lakini hakuna aliyetoa ushirikiano. Hivyo wamejikuta hawawezi kupata taarifa kutoka mamlaka za serikali na hawawezi kupata taarifa kutoka hospitalini kwa sababu hakuna anayejua JPM kalazwa hospitali gani.
#MyTake:
Inaonekana tatizo sio media, tatizo ni viongozi wa serikali ambao hawataki kutoa ushirikiano kwa media. Kitendo cha viongozi kukataa kuzungumzia suala hili kunafanya kuwepo kwa speculations nyingi kwenye jamii.
Nashauri serikali ijitokeze kutoa taarifa rasmi. Kama ni mzima tujulishwe, na kama ni mgonjwa tujulishwe pia ili tumuombee. Watanzania tuna haki ya kujua kuhusu afya ya Rais wetu (Ibara ya 37 ya Katiba). So hakuna sababu ya kufanya siri.
Kuugua ni jambo la kawaida kwa mwanadamu yeyote. JPM si Mungu kiasi kwamba akiugua tutashangaa. Yeye ni mwanadamu kama sisi, so kuugua ni jambo la kawaida. Serikali kuendelea kukaa kimya ni kuzidisha taharuki bila sababu. Ijitokeze, iseme.!
Nimequote kutuka: IG