Baadhi ya vyombo vya habari vya nchi jirani vinaeneza uongo, vichukuliwe hatua Kali

Baadhi ya vyombo vya habari vya nchi jirani vinaeneza uongo, vichukuliwe hatua Kali

People who value privacy over transparency have no business being public servants, much less heads of state.

Presidents are entitled to a minimum modicum of privacy, but they are obligated to be transparent...
Waziri mkuu kasema Rais yupo.

Neno la waziri mkuu kwako halitoshi?
 
Naona wameanza kuwa wapole.

Migogo mapema kabisa akajisema"sisemi neno"
dada yao wa ugaibuni nayeye akaikana post yake.

Walishtuka kwamba wanawezakuwa wanadakishwa tonge la moto.
Ndio maana yake
 
Magazeti ya nchi moja jirani yanaandika habari za uongo na kusababisha taharuki, naomba mamlaka zinazohusika zichukue hatua stahiki.
Mfano People Daily online hasa la leo.

Ni wakati mzuri Sasa Watanzania tushikamane kuitetea nchi yetu.
Leta ukweli wako ili waumbuke,ccm mtataga misumari
 
Nimetafakari jinsi Aljazeera walivyoripoti kwa uhakika kwamba JPM AMELAZWA INDIA KWA CORONA. Unaporipoti habari kubwa kama hii unapaswa uwe na vyanzo vitatu. Reliable, Credible na Authoritative source.

Credible source ni daktari anayemhudumia JPM. Reliable source anaweza kuwa Mhe.Lissu aliyeibua mjadala huu. Na Authoritative source anaweza kuwa Msemaji mkuu wa serikali, au Waziri wa habari, au Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu.

Lakini niliposoma nikakuta source pekee waliyotumia ni Tundu Lissu, which is reliable source. Hakuna Credible wala Authoritative source. Maana yake ni kwamba habari haijabalance. Aljazeera wameripoti kama Carrymastory.

Lissu anaweza kuwa reliable source yani chanzo cha habari cha kuaminika, lakini hiyo haitoshi. Tunapaswa kupata chanzo kutoka kwa madaktari wanaomhudumia (credibility) na serikali (authority). Hivyo ndivyo maadili ya journalism yanavyotaka.

Nimejiuliza hivi baada ya Aljazeera kuripoti hivi halafu JPM akajitokeza hadharani itakuaje? Je hawaoni watakua wameharibu reputation yao? Labda wana njia zao wamezitumia kujiridhisha kwamba kweli JPM yupo India ndio maana wakaripoti. Otherwise wasingeweza kujirisk kwa jambo kubwa hivi.

Hata hivyo Aljazeera wanadai wamehangaika kutafuta viongozi wa serikali lakini hakuna aliyetoa ushirikiano. Hivyo wamejikuta hawawezi kupata taarifa kutoka mamlaka za serikali na hawawezi kupata taarifa kutoka hospitalini kwa sababu hakuna anayejua JPM kalazwa hospitali gani.

#MyTake:
Inaonekana tatizo sio media, tatizo ni viongozi wa serikali ambao hawataki kutoa ushirikiano kwa media. Kitendo cha viongozi kukataa kuzungumzia suala hili kunafanya kuwepo kwa speculations nyingi kwenye jamii.

Nashauri serikali ijitokeze kutoa taarifa rasmi. Kama ni mzima tujulishwe, na kama ni mgonjwa tujulishwe pia ili tumuombee. Watanzania tuna haki ya kujua kuhusu afya ya Rais wetu (Ibara ya 37 ya Katiba). So hakuna sababu ya kufanya siri.

Kuugua ni jambo la kawaida kwa mwanadamu yeyote. JPM si Mungu kiasi kwamba akiugua tutashangaa. Yeye ni mwanadamu kama sisi, so kuugua ni jambo la kawaida. Serikali kuendelea kukaa kimya ni kuzidisha taharuki bila sababu. Ijitokeze, iseme.!
Nimequote kutuka: IG
 

Attachments

  • FB_IMG_1615606668997.jpg
    FB_IMG_1615606668997.jpg
    74 KB · Views: 1
Hili lilikuwa funzo zuri kwao, next time habari zinazotoka kwa Lissu na genge watajua ni uzushi na hawatakurupuka kuandika ovyo ovyo. Kipindi cha uchaguzi pia kulikuwa na habari nyingi za uzushi ambazo international media walikuwa wanazibeba tu kutoka kwa Lissu na genge lake, sasa wajifunze kuchuja.
 
Hili lilikuwa funzo zuri kwao, next time habari zinazotoka kwa Lissu na genge watajua ni uzushi na hawatakurupuka kuandika ovyo ovyo. Kipindi cha uchaguzi pia kulikuwa na habari nyingi za uzushi ambazo international media walikuwa wanazibeba tu kutoka kwa Lissu na genge lake, sasa wajifunze kuchuja.
Sawa
 
credits? umecopy huu ujumbe kama ulivo kule IG then umetuletea hapa. Akili tu yakudraft wazo lako na kuliwasirisha huna hata ukipewa muongozo utaweza kudealkweli na vyombo vya habari aina ya Aljazeera?
Je, Kama huyu aliyeleta hii mada ndiye kaiandika huko IG?
 
Kwenye dunia ya sayansi na teknolojia huwezi kubana uhuru wa habari kirahisi.Ukiminya vyombo vya habari vya ndani basi vile vya kimataifa vitatangaza tu!
 
Back
Top Bottom