Baadhi ya wanaume kiuhalisia wanatufanya tuonekane wote ni wapumbavu hapa JF

Mkuu kidonto,
Kama una hoja ya kuhalalisha mama yako aumizwe basi nipo tayari hapa kufundishwa....

Karibu.
Wewe umewatetea unaowatetea kwa Ujumla wao, na ukiokoteza Mifano Michache tu toka hapa JF....!

Kuna habari ilowahi kuletwa hapa toka Zambia, Mwanaume mwenye kipato cha Kati, Mwenye Mke na Watoto 3, akiwasomesha Watoto na kuitunza Vyema familia yake, mtoto wa kwanza katika age ya miaka 12 wakipishana kidogo na wadogo zake!

Anakuja kugundua Watoto wote 3 sio wake.....! Sasa nataka ujaribu kumsemea huyu Mwanaume hapo chini...!

Hata week haijapita hapa JF kuna mtu kaja kuomba Ushauri, kaoa Single Mother, mwenye Watoto 2, kwa miaka 3 Jamaa anahudumia Mke wake majuzi tu anakuja kugundua kumbe Mke wake kila akibeba Mimba yake huwa anatoa, kagundua Mkewe keshachomoa mimba zake 5....! Nasubiri kuona Ukimsemea huyu Mwanaume pia hapo chini...!

Nimeshawahi kushuhudia Mtaani kwangu, Dada Mtu, anamtafutia Mabwana mke wa Kaka yake, walikua ni Mashoga kupitiliza, na ni mke wa Kaka yake wa Damu, hii chukua wewe itakusaidia, ukiwa na Dada hafu wakawa ni marafiki wakubwa wenyewe wanaita Mashoga, chunguza...!
Utagundua kitu....!

Aisifuye Mvua imemnyea....! Ndo nikasema ukitaka kujua Kunguru hafugiki, jaribu kumfuga....! Ukiona uko salama kwenye Ndoa ama Mahusiano yako, Mshukuru Mungu...! Ila usije hapa na kuwaona wengine hawana akili na hawajui....!


By the way mimi Mama yangu alishafariki.
 
Huu mwandiko ni wakike Kabisa....
 
Mkuu Kidonta,
Pole sana kwa kuondokewa na mama mzazi.

Mosi, nieleweke hivi si kwamba wanawake hawana makosa, sivyo maana yangu! Lakini tukubali tukatae wanaume sisi ni waharibifu 98%.

Nenda nami polepole, mwanaume huyo aliyegundua hao watoto si wake, hao watoto walizalishwa na nani? Si mwanaume mwenzake ndiye aliyemzalisha? Na akakimbia au kupishana kauli, kwanini mwanaume huyo hayupo akilea watoto hao mpaka mwanaume mwingine anakuja kudanganywa na kubeba mzigo ambao si wake? Japo mwanamke hakufanya sawa.
Suala la singo mama kesi itarudi pale pale.
Huyo dada anayemtafutia mke wa kaka yake mabwana sijui, vipi kama dada huyo kaongea na kaka yake wapate sababu ya kumtimua mwanamke huyo ambaye labda kaka yake hamtaki?

Hilo siwezi kulisemea, hata wanawake wanazingua, lakini huko kote kwenye taasisi za kazi mwanamke anapitia changamoto nyngi za kuombwa ngono hili si geni kwako na ipo hivyo mwanamke awe anajiheshimu au ajiheshimu lazima iwe hivyo.
 
Mwanaume tumeumbwa tuwe na miliki yetu yani family,unakupasa utambua kama Mwanaume amemzalisha binti na kumuacha jua kuna mambo mengi ame consider.kama unabisha fanya research.
Mku Eco,
Kumiliki si kutesa na kunyanyasa.

Kwahyo alimuacha baada ya kumpa mimba na kuona kuna mambo ambayo hayapo sawa? Ila kipindi hajampa mambo hayo hayakuwepo?

Basi sawa, yeye hayupo sawa na vipi suala la kulea mtoto wako wewe.
Wengi wamekimbia na kuacha mzigo kwa wanawake?

Vipi yule mtoto naye hayupo sawa?
 
Kwa Majibu yako haya, ngoja nihame kwenye huu Uzi.
 
Ukijipendekeza kwa wanawake haikupi assurance ya wao kukupenda. Hua wanaishia kukudharau. Acha kujipendekeza dogo, by nature wanawake wameumbwa kua submissive jifanye unamuheshim sana uone atakavyokudharau.
Kuna kundi la wanaume liko hapa jf wanatafuta huruma za wanawake na kujipendekeza kwao.

Wanawake wa miaka hii hawana huruma na wanaume hata kidogo. Kujipendekeza kwa mwanamke ni kujiumiza

Wanawake wameshajiwekea standard za wanaume wanaowataka

Kwa hiyo inashangaza wanaume wakijiwekea standard ya wanawake wanaowataka wasiwe single maza inaonekana kama wanawadhalilisha single maza

Tusiwe tunadouble standard mada hapa jf, ndio maana mods hawaoni maana ya kufuta nyuzi za single maza
 
Hakuna mtu alokataa usichague mtu wa kuoa, kufanya nae urafiki na vingine.
Shida kubwa kauli yani kuna vitu vya kitoto sana, mnawadhalilisha dada zetu.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…