Baadhi ya watoto wa maboss huwanyanyasa kingono wasaidizi wa kazi za nyumbani

Baadhi ya watoto wa maboss huwanyanyasa kingono wasaidizi wa kazi za nyumbani

Dkt. Gwajima D

Minister
Joined
Nov 28, 2015
Posts
1,710
Reaction score
8,690
Wasaalam wote.

Huenda visa viko vingi ila, vinafichwa na kimoja kati ya hivyo ni kama hiki ambacho, kimefikishwa kwangu kwa ufupi:

...."Nimefanyiwa ukatili na mtoto wa boss kwa kupigwa sana kisa nimekataa kutoka naye kimapenzi. Alinitishia kuniua kwa sababu nimekataa kufanya naye mapenzi. Tayari tumeripoti ingawa, anaendelea kutuma vitisho na alishaapa kuwa, msichana wa kazi yoyote yule lazima alale nae uwe kwa hiari au kwa lazima. Mama tunaomba msaada".....

LENGO LA KUKUSHIRIKISHA MWANAJAMII; ni ufahamu kuwa haya nayo yapo na huenda huko kwako pia yapo ila, yanafichwa kwa uoga au kumlinda mtoto wa boss. Hivyo, chunguza chukua hatua a.k.a FAHAMU, ELIMIKA, CHUKUA HATUA [FAECH].

WITO; wasaidizi wa kazi waheshimiwe na tukipata taarifa mtoto wa boss atajua hajui. Wengine vunjeni ukimya tafadhali.

KINACHOENDELEA; ufuatiliaji wa karibu unaendelea kwenye hatma ya tukio hili.

Ahsanteni kwa ushirikiano, tunafikika na watu wote hadi vijijini hata wenye simu za vitochi hivyo, tuongeze ushirikiano ukatili utaisha siku moja.
✍️🇹🇿

Ikumbukwe, wasaidizi wa kazi wanaweza kuwa wa kike au kiume.

Naye @peace_maker_pm kasema kumbe, hata baadhi ya maboss wako kama watoto wao..... 🤔🤔🤔PIA TOENI TAARIFA HARAKA.

Wengine nao wanasema, kuna wasaidizi wa kazi wananyanyasa watoto wa maboss... ko, nao tupate taarifa pia.

Nawatakia ushirikiano mwema✍️

IMG-20250707-WA0008.jpg
 
Safi sana ..Kuna hawa vijana wanapenda tu kuwashika wanawake kwenye maungo yao bila ya sababu.Unakuta akimuona tu mdada wa watu anaanza kumfuata mpaka anakosa raha na kukimbia hovyo ..

Wanawashika tu bila ya sababu ,kitu ambacho wasichana wanakosa kujiamini wakiona wanaume kabisa...


Siku moja mtu ashtakiwe ile iwe ni fundisho .
 
Na wanaliwa kweli,japo asilimia kubwa wanajilengesha wenyewe...na wachache ni tamaa za mwili za maboss....ukichunguza hata comments za baadhi ya wanaume wa jf wanachukulia binti wa kazi kama sehemu ya kupozea pale wake zao wanapowagomea unyumba.Changamoto sana
 
Safi sana ..Kuna hawa vijana wanapenda tu kuwashika wanawake kwenye maungo yao bila ya sababu.Unakuta akimuona tu mdada wa watu anaanza kumfuata mpaka anakosa raha na kukimbia hovyo ..

Wanawashika tu bila ya sababu ,kitu ambacho wasichana wanakosa kujiamini wakiona wanaume kabisa...


Siku moja mtu ashtakiwe ile iwe ni fundisho .
Wapeni ujasiri waseme tupate taarifa. Vitolea taarifa 👇sambaza tafadhali

IMG-20250503-WA0006(2).jpg

IMG-20250503-WA0005(2).jpg

IMG-20250510-WA0045(16).jpg
 
Shida kubwa ni wakina mama.

Narudia tena shida kubwa ni wakina mama wenyewe.

Binti hana pa kusemea kwa sababu, mama mwenye nyumba (mlezi wake) ndio utakuta anafuga huo ukatili. Binti atalazimishwa kimapenzi na mwanaume yeyote wa ndani ya nyumba (mume, mtoto, wajomba, wageni nk) lakini akiripoti tu kwa mama, moto utamuwakia.

Ukatili kwa mabinti wa kazi kwenye jamii zetu utaendelezwa daima mpaka siku wanawake wenyewe watakapoamua uishe.
 
Yulle Joyce kiria hana nia ya kuwasaidia wafanyakazi za ndani ndio maana serikali inabidi iwe inazikagua hizi NGO.

Kwenye Kodi naamanisha ni Paye
Sasa boss hapo ni mpaka kuwe na kampuni inayowaajiri ili hayo yafanyike ?

Na mishahara PAYE inakatwa baada ya kutoa NSSF

Mishahara yao inafika hata 300k ?
 
Sio watoto wa mabosi tu hata mabosi wenyewe. Yani wanatumia mwanya huo wa uhitaji kunyanyasa wafanyakazi.

All in all tazania imepata kiongozi. Huyu dada anajua kutupambania sana ,, Mungu azidi kukubariki sana kiongozi
 
Kama mhimili wa jamii na kiongozi, una mpango gani wa kuhimiza uwajibikaji wa maboss wenyewe , ambao pengine kwa kunyamaza au kulinda watoto wao, wanakuwa washirika wa ukatili huu?
 
Kuna utafiti fulani, usio rasmi sana, unaonyesha kuwa, zaidi ya nusu ya vijana kwenye jamii zetu, walipo balehe walianza kufanya mapenzi au kujifunza vitendo vya kimapenzi kupitia wafanyakazi wa ndani waliopo kwao, wa ndugu zao au wa majirani zao.
 
Back
Top Bottom