Baadhi ya watu wanajiuliza kwanini ''bwana yule'' hapati tena siri za Ikulu?

Watakoma, mchawi akila nyama ya mtoto wa jilani ukampa na pili pili, usijetoa mlio siku anatafuna wa kwako.

Kuna kanuni moja kwenye haya mambo inasema, hakuna adui mbaya kama uliyeshirikiana naye kufanya uovu.
Kweli kabisa
 
Inamaana kwa sasa sheria inafuatwa? Uchaguzi wa majimbo ya muhabwe n.k umefanyika kipindi cha mwendazake,au ndo kusema ulikuwa wa haki? kama ulikuwa wa haki,basi hata chaguzi zilizopita zilikuwa za haki.
Mimi ninachokiona hata wengi wa wapinzani wa JPM hawakuwa watetezi wa haki bali mirija yao ya unyonyaji ilikatwa,akiwemo bwana yule.
kama ni kweli bwana yule alitaka haki,mbona kwenye post zake hakuwahi kudai katiba mpya,yeye kama yeye badala yake alisisitiza upinzani wafanye hivyo? Ok katika post zake za sasa mbona hasisitizi tena katiba mpya? au katiba mpya nayo tuliitaka ili imdhibiti mwendazake na baada ya kuondoka hatuna haja nayo?
Nimalizie kwa kusema,JPM aliendesha nchi kwa kadri alivyojaariwa na Mungu na pengine akaweka mapungufu yake kama binadamu,aliweza kuyafanya yale ambayo kwa mtu aliyetegemea nguvu zake na jitihada zake kuishi hakumhathili hata kidogo. Taasisi na watu binafsi waliotegemea njia mbadala ki ukweli wameathirika sio kidogo
na ndo hapo uadui ukaibuka kila kona,bahati mbaya na sisi tuliozoea kulamba makombo yaliyosazwa tukapiga kelele maana makombo nayo
yalionekana kuwa ndo chakula cha kutegemea kwa mabwenyenye.
 
Mkuu pole kwa msiba , hivi Chadema unayoiandika humu kwenye uzi wako ndio ile uliyosema ilshakufa na kuzikwa au kuna Chadema nyingine ?
 
Yuko katikati ya kumushukuru Mungu kwa kumulinda kwa kipindi cha miaka5 na kumvusha akiwa mzima wakati wengine kipindi cha miaka5 wamekimaliza wakiwa ni marehemu na walioponea chupuchupu wanachechemea kwa kukung'utwa risasi.
 
Nina ndugu yangu yeye ni chapombe na hana kazi na ni mwana ccm ila nae alipokufa Magufuli alikuwa anasema bora alivyokufa, sasa ukimuuliza sababu anakwambia Magufuli alizui hela kwenye chama, hivyo alikuwa hapati hela kwenye chama kwahiyo hakuna watu wa kuwapiga vibomu hovyo na kuweka heshima bar. Kwahiyo kuna watu wengi wana sababu zao binafsi zaidi zenye kuwafanya waingie kwenye mkumbo wa kumchukia Magufuli.
 
Yuko katikati ya kumushukuru Mungu kwa kumulinda kwa kipindi cha miaka5 na kumvusha akiwa mzima wakati wengine kipindi cha miaka5 wamekimaliza wakiwa ni marehemu
Mwenye akili timamu hujibidiisha katika kuwatendea wengine wema na kuwaombea kheri na sio kuwaletea na kuwauzia madawa ya kulevya ili wafe,

Lakini pia, unachokisahau mkuu, aliyeanzaga kufa ni Habili baada ya kaini kumuua, na hivyo, Dunia haijawahi kupumzika kumeza watu, na hata Mimi na wewe, ni swala la muda tu, na Kwa sababu hiyo, litakuwa Jambo la kipumbavu na kijinga kuliko chochote akiwako mtu mwenye kufurahia mtu mmoja afapo Wakati huohuo naye muda wake wa kufa ungalipo na asijue ni lini na saa ngapi atakufa

Kivyovyote, Hayati JPM kama ilivyotokea Kwa wengine kufa, Ilibidi tu aondoke Kwa maaana muda wa yeye kuishi duniani ulikuwa tayari umeshakwisha, ama ni Kwa sababu Mungu alimwita ama tu pengine shetani alihusika, lakini Kwa sababu Mungu ndiye mwenye mamlaka na umauti, aliruhusu Hilo litendeke ili tu iwe tamati ya kila kitu alichokipanga kwenye maisha ya Mtumishi wake

Sasa kazi kwenu, kudhihaki kazi ya Mungu ama mnyamaze Kwa kuwa, hakutakuwa na ujanja wa yeyote kukwepa umauti,

Lililobora zaidi, Ishi, Kwa sababu Mungu bado anataka uishi, Watendee wema waja wake na sio wewe uwe sababu ya kuwaangamiza kuwaletea sumu na madawa ya kulevya ili kuuwahisha uhai wao na wakati walustahili kuendelea kuishi

Mungu bariki Tanzania, na uwamlike wote wanaosababisha kumwaga damu na kuuwa wengine
 
Kila kitu kina mwisho.
Mtoa mada na za kwenu zimekwisha?
 
Wewe bado umelala. Naona huenda umenza kufuatilia haya mambo juzi juzi.
 
"Naamini Mama Samia hana timu mpya sana na wala waliomzunguka siyo ndugu Wala rafiki yake Bali ni Watumishi wale wale waliomzunguka JPM. Watumishi hawa wanasali na wana imani lakini kikubwa wanautambuzi wa mema na mabaya. Wengi wa watendaji kwenye ofisi hii nyeti wameapa kuiilinda nchi ndipo wamlinde kiongozi wa nchi. Ikitokea kiongozi mwenye nchi akaisaliti nchi watu hao lazima watatafuta namna ya kuvujisha taarifa kudhibiti damage.

Kwa muktadha huo naanza kuamini wbado Wapo Wazalendo ikulu ambao pamoja na kukabidhiwa nafasi nyeti wanaweza kutoa taarifa wanazodhani zinaliumiza Taifa ili wananchi wajue na mwenye nchi ajue wananchi wanamjua kuliko anavyojijua.

Kosa lililofanywa na mfumo ni kupambana kuzuia taarifa zisitoke badala yakudhibiti uharibifu wa Taifa letu. Uwekezaji uliofanywa kudhibiti Siri ulikuwa mkubwa na wanufaika wanaweza kuwa ni walewale waliovujisha Siri ndio walipewa jukumu lakujitafuta bila kujua ni vigumi kujipata "

mwisho wa kunukuu
 
Sisadhani kama kuvujisha siri ni uwezo mkubwa au kuwa na akili. Huyu hana lolote wala chochote. Kwanza si mzalendo. Pili ni Mmbea tu kama wambea wengine, ambae akipata kihabari baada ya kuhabarishwa na vyanzo kadhaa, ambavyo vilikiuka maadili ya kazi yao ndipo nae uvujisha mtandaaoni. Sasa hiyo ni akili gani kubwa hapo? Hana lolote, kwanza muoga, hajiamini. Akili kubwa ujitambua na hawaishi kwa hofu.
Mfano Lisu, alikosoa wazi wazi, aliongea kile asichokiamini, na kupinga. Lissu na wenzie kadhaa waliojitokeza wazi ndo akili na uwezo mkubwa. Si huyu alokuwa anajificha kwa kuelezea umbea. Kule Mara watu kama hawa wanawaona waoga na wasio na uwezo wa akili. Pia nikimnukuu Spika mstaafu, Marehemu Sitta, huyo jamaa japo umemsifia ANATABIA ZA KIKE.
 
Ni vizuri ukajikita kupigania chato kuwa Mkoa. Hayo ya huyo bwana Achana nayo! Mtaishia kuwa na speculations tu veronica france

Mkuu;
Nadhani na wewe ungejikita kwenye hoja inayotokana na mada niliyoileta!

Hayo ya Chato kupigania kuwa mkoa achana nayo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…