Baba achinjwa na familia yake akidaiwa kuwa kikwazo cha kutumia mali za familia

Baba achinjwa na familia yake akidaiwa kuwa kikwazo cha kutumia mali za familia

Nakumbuka 2008 watoto wa baba yangu mdogo walimuua baba Kwa Mali za watu hata sio zake .

Alikuwa na ml 20 za kujenga kanisa walijua tu kuwa Mzee atakuja kutoka Nairobi so wakatega na saa wakamsubiria wakamkita na akafaa baada ya wiki mbili Kwa maumivu makali .

Na walipofikishwa mahakamani hawakuwekwa jela kwasababu kipindi hicho wao walikuwa wakubwa Tena wanahela bado ni mapolisi so hakuna njia ya wao kufikishwa mahakamani so ndio ikaisha hivyoo.
mda mwingine bora kumalizana hapahapa duniani,yaani bora kuvunja chungu haki mahakamani ngumu kupatikana
 
Huwa najiuliza Sana yaani Mimi baba nitafute Mali zangu na kuwalisha hao wanaoitwa watoto Hadi wanakua afu eti bado Ni Mali zao kwa kisingizio Cha familia?

Huu upumbavu nimekuwa nauona sehemu nyingi yaani ukiwa tuu na familia huna chako,Sasa Nini maana ya sijui kupambana kote huko?

Kwa mantiki hii nimeona Bora uwe na Mali za pembeni wasijue hao kima wanaoitwa wanafamilia Ni Bora zipotelee kwenye mikono ya watu kuliko kuja kuteswa na Mali za jasho lako.
Mkuu kuna muda huwa una mawazo mazuri sana
 
Kwa hyo sie watu wa Mwanza tuna roho mbaya.
Sema hata mim baba angu aliuliwa na mdg ake kwa kuwekewa sumu akinitumia mchepuko na alilipwa pesa ndogo sana.
Hakuna hukumu ilotolewa kesi ukikosa ushahidi baada ya muda huyo ba angu mdg mtoto ake alikua teja akafariki mtoto ake mwingine akawa kama vile chizi si chizi. Amebaki na mtoto mmja mzima.
Huyo mchepuko sa hiv anauza viaz vitamu sokoni yani anatia huruma acha kabisa.
Soma habari za mauaji hata humu JF uone mikoa inayoongoza ni Mara, Mwanza na Shinyanga. Lini ulisikia mtu Tanga kaua mzazi sijui mtoto wake
 
Kwa hyo sie watu wa Mwanza tuna roho mbaya.
Sema hata mim baba angu aliuliwa na mdg ake kwa kuwekewa sumu akinitumia mchepuko na alilipwa pesa ndogo sana.
Hakuna hukumu ilotolewa kesi ukikosa ushahidi baada ya muda huyo ba angu mdg mtoto ake alikua teja akafariki mtoto ake mwingine akawa kama vile chizi si chizi. Amebaki na mtoto mmja mzima.
Huyo mchepuko sa hiv anauza viaz vitamu sokoni yani anatia huruma acha kabisa.

Wengi wenu mnamatatizo ya Akili na upeo mdogo wa kufikiri. Sema watu wanafiki watabisha au wataona haya/aibu kulisema Jambo Hilo.

Ninaushahidi wa kutosha juu ya Jambo Hilo. Sema sio site wapo wachache wanaojielewa.
Ola wengi wenu ni macherema.

Hasira za kijinga,
Kutokujiamini na ubabe usio na kichwa wala miguu.
Imani za kichawi na ushirikina ninyi ndio nambari moja.

Lazima mubadilike bhana.

Soma hapa👇🏽👇🏽
 
Hata bila kukuua wanauza au wanakuzuia kuuza na huna Cha kufanya kwa sababu hata sheria zinawalinda wanafamilia yaani wakizuia hata Kama uliuza ,aliuenunua inakula kwake yaani yeye na mzee wanonekana Wana makosa.

Hizi Ni Sheria za kipumbavu.Ukiacha Hilo mitoto huwa haitaki mzee aoe Kama mama Yao kafariki kwa maelezo kwamba atakula Mali ya mama Yao.

Wakati huo huo sijui wanategemea baba Yao atawatomba wao au wao ndio watakuja kimpikia ,kufua nk akiwa kwenye utu uzima huo..

Huu.ni ushenzi kwa sababu Mali zimetangulia kuliko utu.
Hiyo sentensi ya mwisho imenichekesha sana
 
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linawashikilia watu watano akiwemo Mkazi wa Kijiji cha Kiliwi wilayani Kwimba, Hoka Mazuri (48) na wanaye wawili kwa tuhuma kumuua mumewe, Mange Washa (49)...

Daaah sisi wazazi tuombee sana hawa watoto wetu, hao walishidwa tu kuelewa uyo mzee wao alikuwa akiwatunzia wao hao hao watoto izo mali!! Ila watoto na mama wamekosa maarifa! R.I.P

Hawa wauza bange, gongo, mirungi wangeachana nao tuu maana life ni gumu na mkuu kasema tule kwa urefu wa kamba.... sasa kamba zao zinaruhusu kulq hapo[emoji1353]

Police, takukuru kama kweli mpo siriazi na hii inchi anzeni na zile behewa za SGR,
 
Kwakuwa ni Mwanza basi utalaumiwa umaskini ila ingetokea Kilimanjaro ambapo ni nadra mauaji kutokea hapa makelele yangekuwa mengi.

Ukweli ni kwamba Mwanza na Shinyanga ndipo wanaongoza kwa mauaji si wanawake si wanaume, hatua zakupambana na hiyo zichukuliwe either kielimu kwa jamii au kiroho.

Too much stereotype kwa Kilimanjaro hasa wanawake wakati hawana shida kama huko kanda ya ziwa
 
Mkiambiwa mkitaka kuoa mushirikishe wazazi mnajifanya wajanja mnataka pisi kali matokeo yake ndo hayo.
 
Wengi wenu mnamatatizo ya Akili na upeo mdogo wa kufikiri. Sema watu wanafiki watabisha au wataona haya/aibu kulisema Jambo Hilo.

Ninaushahidi wa kutosha juu ya Jambo Hilo. Sema sio site wapo wachache wanaojielewa.
Ola wengi wenu ni macherema.

Hasira za kijinga,
Kutokujiamini na ubabe usio na kichwa wala miguu.
Imani za kichawi na ushirikina ninyi ndio nambari moja.

Lazima mubadilike bhana.

Soma hapa👇🏽👇🏽
Khaaaaah
 
Watu watano akiwemo mama na watoto wake wawili wanaodaiwa kuhusika katika mauaji ya baba yao mzazi mkazi wa Kijiji cha Kiliwi wilayani Kwimba mkoani Mwanza, Mange Washa (49) wamepandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza na kusomewa shtaka la mauaji.

Waliopandishwa kizimbani leo Jumatano Disemba 14, 2022 katika mahakama ya Wilaya ya Kwimba ni Hoka Mazuri (48) ambaye ni mke wa marehemu pamoja na watoto wake wawili Masunga Mange na Paskali Mange. Wengine ni wanaume wawili wanaodaiwa kulipwa Sh800, 000 na wanafamilia hao kutekeleza mauaji hayo ni Shija Masalu (28) na Makoye Lusana (53) ambaye ni mshtakiwa namba moja katika kesi hiyo ya Jinai namba 12/2022.

Akisoma shtaka linalowakabili mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya hiyo, Ndeko Dastan, Mwendesha mashtaka wa Serikali, Robert Mwanakatwe amesema Disemba Mosi mwaka huu washtakiwa hao walimuua, Mange Washa kwa kumkata kichwa akiwa amelala nyumbani kwake kisha kutenganisha kichwa na kiwiliwili chake. "Washtakiwa wote mnashtakiwa kutenda kosa hilo la mauaji kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha Kanuni ya Adhabu marekebisho ya mwaka 2022, mauaji ambayo mnadaiwa kuyatekeleza huko Kiliwi tarafa ya Bupamwa wilayani Kwimba," amesema. Baada ya kuwasomea shtaka hilo ameomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa kwa sababu upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ndeko Dastan ameahirisha kesi hiyo hadi Disemba 28,2022 itakapoitwa kwa ajili ya kutajwa tena. "Washtakiwa mtaendelea kukaa rumande hadi hapo kesi itakapoitwa tena kwa ajili ya kutajwa, shtaka linalowakabili halina dhamana," amesema Hakimu Dastan
Washtakiwa hao wanadaiwa kupanga njama na kutekeleza mauaji ya mwanaume huyo waliyemtuhumu kuwanyima uhuru wa kutumia mali za nyumbani kwao, Disemba Mosi mwaka huu kabla ya kukamatwa Disemba 5, mwaka huu kwa hatua zaidi za kisheria.

Source: Gazeti la Mwananchi la Disemba 14, 2022.
 
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linawashikilia watu watano akiwemo Mkazi wa Kijiji cha Kiliwi wilayani Kwimba, Hoka Mazuri (48) na wanaye wawili kwa tuhuma kumuua mumewe, Mange Washa (49).

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amewataja watoto wa mwanamke huyo wanaoshikiliwa kwa mauaji hayo kuwa ni, Masunga Mange na Paskali Mange.

Mutafungwa amedai, ili kufanikisha lengo lao bila kushtukiwa wanafamilia hao walimlipa mkazi wa Bugembe wilayani humo, Shija Masalu (28) na Makoye Lusana (53) Sh800, 000 ili wamuue baba wa familia hiyo ambaye taarifa zinadai alikuwa kikwazo wanapohitaji kutumia mali za familia hiyo.

Amesema Desemba Mosi mwaka huu Saa 1:00 usiku baada ya kulipwa fedha na familia hiyo, Masalu na Lusana walimvamia Mange Washa akiwa amelala wakamkata kichwa na kukitenganisha na kiwiliwili kisha kutokomea kusikojulikana.

"Mauaji ya Mange yalipangwa na mke wake akishirikiana na watoto wake wawili kutokana na ugomvi wa mali uliyodumu kwa muda mrefu, kwani mmoja wa wana familia hiyo, Masunga Mange alifukuzwa na baba yake (Marehemu) kwa kuhusika na wizi wa mifugo ya familia yake na ya wakazi wengine wa kijiji hicho.

"Baada ya mauaji hayo Hoka Mazuri na wanaye wawili waliwahadaa watoto wengine ambao walikuwa wamelala nyumba nyingine jirani kwamba, baba yao amekatwa mapanga na mtu asiyejulikana, wakati wanaujua ukweli kuwa wao ndiyo waliopanga na kuratibu mauaji hayo," ameongeza.

Amesema watuhumiwa hao wanaendelea kushikiliwa chini ya jeshi hilo kwa mahojiano zaidi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Katika hatua nyingine, Kamanda Mutafungwa amesema jeshi hilo kupitia doria zake linawashikilia watu 104 kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukutwa na kilo 29 za Bangi, na miche 40 ya bangi, mirungi kilo 62.6, lita 4,270 za pombe aina ya Gongo, mitambo 14 ya kutengenezea pombe hiyo na gramu 2.3 za dawa za kulevya aina ya Heroine.

Pia, amesema watuhumiwa wengine 18 wanashikiliwa kwa tuhuma za makosa ya uvunjaji wa nyumba na maduka kisha kuiba mali zikiwemo televisheni, simu na pikipiki.

"Pia tumekamata vifaa mbalimbali vilivyoibwa katika mradi wa ujenzi wa daraja la JPM Kigongo-Busisi na nyavu haramu za kuvulia samaki ndani ya Ziwa Victoria," amesema Mutafungwa.

Katika tukio lingine, Kamanda Mutafungwa amesema jeshi hilo linamshikilia mkazi wa Mtaa wa Jiwe Kuu kata ya Kitangiri wilayani Ilemela mkoani hapa, Merry Seni (21) kwa tuhuma za kutoa ujauzito wenye umri wa miezi saba na kutupa kichanga hicho.

MWANANCHI
Hii inazidi kutujuza kuwa kina mama ni wabinafsi tofauti na jamii inavyoamini na kuwatwisha wanaume lawama kila kukicha.
 
Back
Top Bottom