scolastika
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,863
- 5,719
mda mwingine bora kumalizana hapahapa duniani,yaani bora kuvunja chungu haki mahakamani ngumu kupatikanaNakumbuka 2008 watoto wa baba yangu mdogo walimuua baba Kwa Mali za watu hata sio zake .
Alikuwa na ml 20 za kujenga kanisa walijua tu kuwa Mzee atakuja kutoka Nairobi so wakatega na saa wakamsubiria wakamkita na akafaa baada ya wiki mbili Kwa maumivu makali .
Na walipofikishwa mahakamani hawakuwekwa jela kwasababu kipindi hicho wao walikuwa wakubwa Tena wanahela bado ni mapolisi so hakuna njia ya wao kufikishwa mahakamani so ndio ikaisha hivyoo.
Mkuu kuna muda huwa una mawazo mazuri sanaHuwa najiuliza Sana yaani Mimi baba nitafute Mali zangu na kuwalisha hao wanaoitwa watoto Hadi wanakua afu eti bado Ni Mali zao kwa kisingizio Cha familia?
Huu upumbavu nimekuwa nauona sehemu nyingi yaani ukiwa tuu na familia huna chako,Sasa Nini maana ya sijui kupambana kote huko?
Kwa mantiki hii nimeona Bora uwe na Mali za pembeni wasijue hao kima wanaoitwa wanafamilia Ni Bora zipotelee kwenye mikono ya watu kuliko kuja kuteswa na Mali za jasho lako.
Zinakujaga automaticMbona mie sina sifa hizi? 😀😀
Soma habari za mauaji hata humu JF uone mikoa inayoongoza ni Mara, Mwanza na Shinyanga. Lini ulisikia mtu Tanga kaua mzazi sijui mtoto wakeKwa hyo sie watu wa Mwanza tuna roho mbaya.
Sema hata mim baba angu aliuliwa na mdg ake kwa kuwekewa sumu akinitumia mchepuko na alilipwa pesa ndogo sana.
Hakuna hukumu ilotolewa kesi ukikosa ushahidi baada ya muda huyo ba angu mdg mtoto ake alikua teja akafariki mtoto ake mwingine akawa kama vile chizi si chizi. Amebaki na mtoto mmja mzima.
Huyo mchepuko sa hiv anauza viaz vitamu sokoni yani anatia huruma acha kabisa.
Kwa hyo sie watu wa Mwanza tuna roho mbaya.
Sema hata mim baba angu aliuliwa na mdg ake kwa kuwekewa sumu akinitumia mchepuko na alilipwa pesa ndogo sana.
Hakuna hukumu ilotolewa kesi ukikosa ushahidi baada ya muda huyo ba angu mdg mtoto ake alikua teja akafariki mtoto ake mwingine akawa kama vile chizi si chizi. Amebaki na mtoto mmja mzima.
Huyo mchepuko sa hiv anauza viaz vitamu sokoni yani anatia huruma acha kabisa.
Timua kabisa!!Watoto wakianza kujielewa tu, fukuza nyumbani wakaanze kujitegemea, ukiwachelewesha sana wanaanza kutegemea Mali zako.
Hiyo sentensi ya mwisho imenichekesha sanaHata bila kukuua wanauza au wanakuzuia kuuza na huna Cha kufanya kwa sababu hata sheria zinawalinda wanafamilia yaani wakizuia hata Kama uliuza ,aliuenunua inakula kwake yaani yeye na mzee wanonekana Wana makosa.
Hizi Ni Sheria za kipumbavu.Ukiacha Hilo mitoto huwa haitaki mzee aoe Kama mama Yao kafariki kwa maelezo kwamba atakula Mali ya mama Yao.
Wakati huo huo sijui wanategemea baba Yao atawatomba wao au wao ndio watakuja kimpikia ,kufua nk akiwa kwenye utu uzima huo..
Huu.ni ushenzi kwa sababu Mali zimetangulia kuliko utu.
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linawashikilia watu watano akiwemo Mkazi wa Kijiji cha Kiliwi wilayani Kwimba, Hoka Mazuri (48) na wanaye wawili kwa tuhuma kumuua mumewe, Mange Washa (49)...
Kisura, upo? Siku nyingi hujasikika.Imagine ingekua ni kilimanjaro[emoji28][emoji28]
Hapa wahusika wanaupita kama maiti
KhaaaaahWengi wenu mnamatatizo ya Akili na upeo mdogo wa kufikiri. Sema watu wanafiki watabisha au wataona haya/aibu kulisema Jambo Hilo.
Ninaushahidi wa kutosha juu ya Jambo Hilo. Sema sio site wapo wachache wanaojielewa.
Ola wengi wenu ni macherema.
Hasira za kijinga,
Kutokujiamini na ubabe usio na kichwa wala miguu.
Imani za kichawi na ushirikina ninyi ndio nambari moja.
Lazima mubadilike bhana.
Soma hapa👇🏽👇🏽
Ndugu zetu Wa kanda ya ziwa ndio mnaongoza Kwa matukio ya Ukatili hapa nchini. Tatizo ni nini?
Kwema Wakuu! Tangu napata Akili nikiwa sekondari nasikia matukio ya kikatili yanayotokea huko Kwa Ndugu zetu wa Kanda ya ziwa, mpaka nafika chuo na sasa nimekuwa mtu mzima bado nasikia matukio ya kikatili huko kanda ya ziwa. Haiwezi kuisha siku mbili bila kusikia matukio ya kikatili kutokea...www.jamiiforums.com
Hii inazidi kutujuza kuwa kina mama ni wabinafsi tofauti na jamii inavyoamini na kuwatwisha wanaume lawama kila kukicha.Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linawashikilia watu watano akiwemo Mkazi wa Kijiji cha Kiliwi wilayani Kwimba, Hoka Mazuri (48) na wanaye wawili kwa tuhuma kumuua mumewe, Mange Washa (49).
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amewataja watoto wa mwanamke huyo wanaoshikiliwa kwa mauaji hayo kuwa ni, Masunga Mange na Paskali Mange.
Mutafungwa amedai, ili kufanikisha lengo lao bila kushtukiwa wanafamilia hao walimlipa mkazi wa Bugembe wilayani humo, Shija Masalu (28) na Makoye Lusana (53) Sh800, 000 ili wamuue baba wa familia hiyo ambaye taarifa zinadai alikuwa kikwazo wanapohitaji kutumia mali za familia hiyo.
Amesema Desemba Mosi mwaka huu Saa 1:00 usiku baada ya kulipwa fedha na familia hiyo, Masalu na Lusana walimvamia Mange Washa akiwa amelala wakamkata kichwa na kukitenganisha na kiwiliwili kisha kutokomea kusikojulikana.
"Mauaji ya Mange yalipangwa na mke wake akishirikiana na watoto wake wawili kutokana na ugomvi wa mali uliyodumu kwa muda mrefu, kwani mmoja wa wana familia hiyo, Masunga Mange alifukuzwa na baba yake (Marehemu) kwa kuhusika na wizi wa mifugo ya familia yake na ya wakazi wengine wa kijiji hicho.
"Baada ya mauaji hayo Hoka Mazuri na wanaye wawili waliwahadaa watoto wengine ambao walikuwa wamelala nyumba nyingine jirani kwamba, baba yao amekatwa mapanga na mtu asiyejulikana, wakati wanaujua ukweli kuwa wao ndiyo waliopanga na kuratibu mauaji hayo," ameongeza.
Amesema watuhumiwa hao wanaendelea kushikiliwa chini ya jeshi hilo kwa mahojiano zaidi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.
Katika hatua nyingine, Kamanda Mutafungwa amesema jeshi hilo kupitia doria zake linawashikilia watu 104 kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukutwa na kilo 29 za Bangi, na miche 40 ya bangi, mirungi kilo 62.6, lita 4,270 za pombe aina ya Gongo, mitambo 14 ya kutengenezea pombe hiyo na gramu 2.3 za dawa za kulevya aina ya Heroine.
Pia, amesema watuhumiwa wengine 18 wanashikiliwa kwa tuhuma za makosa ya uvunjaji wa nyumba na maduka kisha kuiba mali zikiwemo televisheni, simu na pikipiki.
"Pia tumekamata vifaa mbalimbali vilivyoibwa katika mradi wa ujenzi wa daraja la JPM Kigongo-Busisi na nyavu haramu za kuvulia samaki ndani ya Ziwa Victoria," amesema Mutafungwa.
Katika tukio lingine, Kamanda Mutafungwa amesema jeshi hilo linamshikilia mkazi wa Mtaa wa Jiwe Kuu kata ya Kitangiri wilayani Ilemela mkoani hapa, Merry Seni (21) kwa tuhuma za kutoa ujauzito wenye umri wa miezi saba na kutupa kichanga hicho.
MWANANCHI