Baba anatoa nyumba yake ya Kariakoo wakfu iwe mali ya msikiti, huku watoto wake wamepinga hawana urithi, why Watu weusi hatujui Generational wealth

Baba anatoa nyumba yake ya Kariakoo wakfu iwe mali ya msikiti, huku watoto wake wamepinga hawana urithi, why Watu weusi hatujui Generational wealth

Nachukiaga sana binadamu mwenye nguvu zako huna ulemavu, akili timamu kuanza kugombea mali za urithi.
Kwann usitafute zako?, umekuja dunian kuwa tegemezi?, yaan mzee wawatu kaamua zake atumie jasho lake kujitolea kwaajili ya dini yake (sadaka yenye kuendelea) ila mitoto utakuta imefuga vitambi na misuli inagombea mali za mzee wao ambazo muda huo utakuta mzee alishatimiza wajibu wake wa kuwalea, kuwalisha, kuwasomesha n.k. ila bado wanampangia matumizi ya mali zake😡
Nyie ndo wale mnaoambiwe mkaijaze dunia na mnakubali hata kama hamna cha kuwalisha watoto.

Badilikeni tafadhali.
 
Hakuwasomesha na kuwapa chakula mpaka pale mlipoweza kujitegemea ? Kwani yeye Babu yake alimuachia nini tuanzie hapo kwanza ?

Tutofautisha Obligation (wajibu) na uamuzi / maamuzi ; By the way kitendo cha hawa kumpeleka mahakamani inaonyesha ni jinsi gani they don't deserve hata sumni ya huyu mzee...
 
Wazazi wamekuwa wakorofi sana hivyo tuwafute kusiwe na wazazi duniani!
 
Tafuta mali zako mzee yupo sahihi kabisa.

Matoto Kama wewe ni hasara mnapenda vya urithi TAFUTA MALI ZAKO KAMA NI RAHISI.

NB. KUNA MTOTO WA BA MKUBWA BAADA YA MZEE KUFARIKI WAMEUZA ASSET ZAKE ZOTEEE NOW WAPO MAHAKAMANI KUDAI MIRATHI.
Pia atwambie. Wale watoto waliouza nyumba hapo kariakoo je kuna yeyote alishawahi jikwamua kiuchumi kwa kuuza nyumba??
 
Unafikiri hata Ulaya mtu akiacha mirathi kwa mbwa huwezi kujua alikuwa na maana gani

Kila mmoja ana haki ya kugawa Mali zake atakavyo

Kuna watu wanawaachia jirani
 
Ni sawa na mzazi kwenda kutoa sadaka kanisani au masikitini wakati umeacha watoto wako nyumbani wamealala njaa. Sidhani kama kuna thawabu hapo.
Mithali 13:22 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.
Labda quran inafundisha tofauti.
Atakuwa yupo sawa kama tu anajua watoto wake ni wa pumbavu akiwaachia urithi watauana au ni wapumbavu walitaka kumuua ili warithi au hawataki kufanya kazi wanasubiri mzee afe warithi.
 
Nyie ndo wale mnaoambiwe mkaijaze dunia na mnakubali hata kama hamna cha kuwalisha watoto.

Badilikeni tafadhali.
Kama hao watoto wangekuwa wadogo tungemlaumu mzee kwa maamuzi yake, ila kwakuwa mzee keshatimiza majukumu yake kwa kuwalea mpaka wamefikia utu uzima wa kujitafutia basi mzee hana lawama maana alishakamilisha majukumu yke
 
Watu hudhani urithi ni lazima na haki yao,ndiyo maana mahakama hutaka wosio wa marehemu maana unaheshimiwa
 
Hakuwasomesha na kuwapa chakula mpaka pale mlipoweza kujitegemea ? Kwani yeye Babu yake alimuachia nini tuanzie hapo kwanza ?

Tutofautisha Obligation (wajibu) na uamuzi / maamuzi ; By the way kitendo cha hawa kumpeleka mahakamani inaonyesha ni jinsi gani they don't deserve hata sumni ya huyu mzee...
Yeye kama hakupewa chochote basi baba yake anamakosa. Kama hataki kuwapa urithi watoto kwani aliwazaa? Nani alimwambia ajamiiane kwa raha zake na kuwazaa watoto ambao hataki kuwahudumia?

Umalaya uachwe kama ni hivyo?
 
Unawapangia watu cha kufanya
je ni sawa baba yenu aliyezeeka kutoa nyumba yake ya pekee kwenye prime area kariakoo kuwa mali ya msikiti huku watoto wake hamna maisha ya kueleweka, mnateseka kutafuta mtaji wa kujikomboa ?

video inaonesha mzee akiitoa nyumba yake yenye ardhi yenye thamani kubwa kariakoo kuwa mali ya msikiti, watoto walipinga ila mzee ndio kashaamua

kwa nini watu weusi wengi hatutambui Generational wealth ? kama kina Donald Trump walivyofaidika nayo kutoka kwenye ardhi za prime areas alizorithi kutoka kwa baba yake na babu zake

Hata tajiri kama Bakhressa na GSM huwezi kukuta wanatoa sadaka ardhi yao ya Kariakoo ama prime area kama masaki na oysterbay.

Ardhi ya kariakooo ni kama mgodi wa dhahabu isiyoisha... hakuna tajiri aliewahi kutoa sadaka ardhi ya kariakoo.. hao kina bakhressa sadaka wanazitoa ardhi za huko chamazi ama kisemvule, ila sio kariakoo


imagine hilo eneo lao kariakoo wangeingia mkataba na tajiri angejenga ghorofa la ma fremu hapo,,, watoto wake wangekula hadi kizazi cha nne kingekula matunda yake

View attachment 3379922
Kwa mali zao walizotafuta wenyewe? Acha kuwapangia wenzio maisha bwana huu ushauri ungempa baba yako
 
Kama hao watoto wangekuwa wadogo tungemlaumu mzee kwa maamuzi yake, ila kwakuwa mzee keshatimiza majukumu yake kwa kuwalea mpaka wamefikia utu uzima wa kujitafutia basi mzee hana lawama maana alishakamilisha majukumu yke
Kama watoto bado wanalamika juu ya kitendo cha mzee kutoa nyumba kwa msikiti inamaanisha kuwa hakuwalea watoto wake vizuri/hakuwaandalia maisha mazuri.
 
je ni sawa baba yenu aliyezeeka kutoa nyumba yake ya pekee kwenye prime area kariakoo kuwa mali ya msikiti huku watoto wake hamna maisha ya kueleweka, mnateseka kutafuta mtaji wa kujikomboa ?

video inaonesha mzee akiitoa nyumba yake yenye ardhi yenye thamani kubwa kariakoo kuwa mali ya msikiti, watoto walipinga ila mzee ndio kashaamua

kwa nini watu weusi wengi hatutambui Generational wealth ? kama kina Donald Trump walivyofaidika nayo kutoka kwenye ardhi za prime areas alizorithi kutoka kwa baba yake na babu zake

Hata tajiri kama Bakhressa na GSM huwezi kukuta wanatoa sadaka ardhi yao ya Kariakoo ama prime area kama masaki na oysterbay.

Ardhi ya kariakooo ni kama mgodi wa dhahabu isiyoisha... hakuna tajiri aliewahi kutoa sadaka ardhi ya kariakoo.. hao kina bakhressa sadaka wanazitoa ardhi za huko chamazi ama kisemvule, ila sio kariakoo


imagine hilo eneo lao kariakoo wangeingia mkataba na tajiri angejenga ghorofa la ma fremu hapo,,, watoto wake wangekula hadi kizazi cha nne kingekula matunda yake

View attachment 3379922
Hii ni shida..

Si angeliuza ama kuingia mkataba na wenye hela then angeenda kutafuta eneo lingine nje ya kariakoo
 
Back
Top Bottom