Baba mwenye nyumba hataki nifanye biashara ya pombe kali

1. Akurudishie pesa ya matengenezo yako yote uliyafanya ili uhamie pengine.

2. Akurudishie kodi ya nyumba uliyolipa ukaanze pengine.

3. Endelea na msimamo wako kwamba wazo la biashara ni lako huna wajibu wa kumwambia mtu mwingine as long as ni biashara halali kisheria. Ama alitaka umwambie wazo lako yeye akugeuke aanzishe hiyo biashara yeye? Wazo la biashara ni private.

Kama yeye ana ishu za kiimani ama binafsi kuhusu biashara flani yeye ndio alipaswa aweke wazi mapema kwamba biashara flani hazitaki kwenye nyumba yake.
 
Nini maana ya mkataba, au hapa huwa mnasaini tu, na je ipoje mkataba unapovunjwa ....kiufupi hapo unastahili fidia ya kodi yako plus muda na hasara ya kuleta mzigo hapo halafu akakubadilikia...nenda mahali tafsiri ya mikataba inapofanyika utafsiliwe huo mkataba.
 
Wewe mwambie akurudishie pesa yako ukatafute sehemu nyingine


Hata kama mkataba haujasema hivyo , wewe ulitakiwa uwe muwazi.

Watu wana heshima zao hawawezi kukupa fremu uuzie pombe, watu wapige makelele, watukanane, wapigane, wawachukize watu nk


Yote haya yeye atalazimika kupata lawama kwa majirani

Ukitaka kufanya biashara ya pombe kakodi fremu kwa walevi wenzako.


NB

Ukienda kwa mwanasheria utajisumbua na kupoteza pesa tu

Huwezi kumlazimisha mtu ufanye biashara asiyoitaka kwenye jengo lake
 
Huo mkataba umeuona ?


Mkataba wa mpangaji huwa unabase kwenye malipo tu


Ukizingua unatolewa muda wowote na huna cha kufanya
 
Huu ndio ushauri sahihi hapa.
 
Kwenye masharti ya mkataba wake kuna kipengele kinakataa biashara ya pombe? Kama hakipo january endelea na biashara yako kama kawaida
 
Huu ndio ushauri sahihi hapa.
Yaani mkuu mimi ilishawahi nitokea.

Nikamfata bibi nikamwambia bibi nataka utoe tamko watoto wake wakawa wanaleta maneno ya kejeli.

Nikasimama nikaondoka kwenda kumueleza mwanasheria, akaandika statment ndani ya siku 3 watoe tamko aidha sheria ichukuliwe.

Bibi yule alinifata akaniambia mwanangu naomba tuyaongee yaishe
tuongee kindugu tu.

Huyo babu anapima upepo yaani sema tu jamaa asifatilie.atalipa mpaka pesa ya bodaboda ningemuhesabia.
 
Kwenye masharti ya mkataba wake kuna kipengele kinakataa biashara ya pombe? Kama hakipo january endelea na biashara yako kama kawaida
Kwenye mkataba wake hakuna kifungu kinachokataza aina ya biashara ila mkata unainisha kunga chumba kwa ajiri ya biashara
 
Mwenye heshima zake anakuambia masharti yake kabla hajakupangisha. Huyo mwenye fremu ni muhuni TU.

Mind you, katika kutafuta nyumba nishakutana na mwenye nyumba anasema kabisa kuwa "Mimi sipangishi Mkristo", "Mimi siruhusu nguruwe aliwe nyumbani kwangu" na "Mimi sipangishi bachela" na mwingine alisema "sitaki mpangaji mwenye watoto" Haya ni masharti ambayo mtu mwenye busara huyaweka wazi kabla ya kuchukua Hela ya mpangaji.
 
Huo mkataba umeuona ?


Mkataba wa mpangaji huwa unabase kwenye malipo tu


Ukizingua unatolewa muda wowote na huna cha kufanya
Huna cha kufanya ni huko kwenu Kwa wajinga wajinga. Una shida ya Hela ndio maana unapangisha, otherwise Baki na vyumba vyako uweke misukule. Hiyo ni biashara Sio msaada.
 
Pombe haziharibiki, anafaulisha ama kuweka ome akiangalia sehemu ingine
Hiyo pesa yakuanzisha masaji anaipata wapi mtu alishalipia mzigo?

Hapo suala ni moja alipe gharama zote, mpaka mzigo kufika hapo ndani na kama kuna marekebisho jamaa kafanya alipe mpaka pesa aliyokula.

Huyo mzee anatingisha kiberiti.
Kama hawezi aache watu wafanye kazi mpaka mkataba uishe.
 
Mkuu kumbuka hii ni bongo kila jambo linaenda kijanja janja.
 
kubali hasara, akurudishie kodi ila pesa sijui ya hasara sahau

kwenda kwa mwanasheria unapoteza mda na pesa zako
 
Hili kuondoa mkanganyiko tumia hekima yaani asikuumize na wewe usimuumize.

Maana Kwa imani nikweli baadhi ya WATU wanazichukia Sana pombe .

Mwambie Kwa ustaharabu kuwa akurudishie pesa ikiwemo na fidia ambayo umeingia katika matengenezo.
 
kubali hasara, akurudishie kodi ila pesa sijui ya hasara sahau

kwenda kwa mwanasheria unapoteza mda na pesa zako
Mkuu dronedrake,

Kama mzee atashindwa kumpisha jamaa akafanya kazi. Pesa yote mpaka kwa mwanasheria atailipa yeye.

Kama hataki hayo akae pembeni atulie. Asubiri anmalize mkataba au jamaa afanye busara kuchukua kodi yake aondoke.
 
Huo mkataba umeuona ?


Mkataba wa mpangaji huwa unabase kwenye malipo tu


Ukizingua unatolewa muda wowote na huna cha kufanya
Kama ni hivyo basi hauna sifa ya kuitwa mkataba, lakini nijuavyo mkataba ni makubaliano kukiwa na mashahidi uwe wa maandishi au sauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…