Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 2,331
- 7,733
Akiongea na Azam News, Baba mzazi wa askari aliyejinyonga anasema hajaridhishwa na taarifa za kifo cha mwanae!
Anasema alipigiwa simu na kuambiwa mwanao tumpeleke akazikwe wapi? Akawaambia mleteni nyumbani kwangu Tabata, Dar Ea Salaam.
Pia soma Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga (26/01/2022)
Walipofika wakataka kushusha maiti na kuondoka, ndipo alipowagomea na kuanza vurugu baadae maiti ikaenda kuhifadhiwa hospitali ya Polisi Kilwa Road.
Baba mzazi ana mashaka na kifo cha mwanae, anasema mwanae ameuawa kwa kuwa mwanae alisimamia ukweli kuwa alitumwa na wakubwa wake kufanya mauaji ya mfanyabiashara.
Baba mzazi anamuomba IGP Sirro kuunda tume kuchunguza kifo hiko. Anasema haiwezekani sero ya polisi kuwe na tambala!
Baba mzazi wa marehemu ni askari mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
=====

"Nilipewa taarifa kuwa mwanao ameshikiliwa kwenye mahabusu ya Polisi, na Januari 22, 2022 nilipigiwa simu kuwa bahati mbaya mwanao amejinyonga, jambo ambalo lilinistua sana" Gaitan Mahembe, baba mzazi wa askari anayedaiwa kujinyonga Greyson Mahembe
"Polisi walifanya mambo haraka, wakaleta mwili hadi kwangu Segerea haraka walipofika wakawa wanasema shusha hapa, tukakataa nusura tupigane, tukawaambia mwili huu ukahifadhiwe kisha tuje hapa tuzungumze" Gaitan Mahembe, baba mzazi wa Greyson Mahembe, askari anayedaiwa kujinyonga
"Tuliwaambia askari waliouleta mwili, safari yetu ni ya Iringa lakini hatuwezi kuupokea hadi mtueleze, mwanangu ni afisa wa jeshi alitakiwa asindikizwe kijeshi na azikwe kijeshi kwanini halikufanyika hilo"Gaitan Mahembe, baba mzazi wa Greyson Mahembe, askari anayedaiwa kujinyonga
"Kama mwanangu alijinyonga wangeitwa ndugu upande wetu wakathibitishe au tungeoneshwa picha hata za kutoka jeshi la polisi zikionesha amejinyonga, au picha zozote kwenye vyombo vya habari. Hakuna hilo" Gaitan Mahembe, baba mzazi wa Greyson Mahembe, askari anayedaiwa kujinyonga
"Ndugu yetu aliitwa wakati marehemu alishapelekwa hospitali ya Ligula na akaoneshwa michubuko akielezwa ni ya kamba, kisha akaambiwa ni ya tambara la deki, hivi mahabusu ya jeshi kuna tambara la deki?" Gaitan Mahembe, baba mzazi wa Greyson Mahembe, askari anayedaiwa kujinyonga
"Mimi na familia yangu hatujaridhishwa, tunamuomba IGP alifafanue hili na ukweli uwekwe wazi. Hatuna kipato, hivyo tunaomba tupate mwanasheria wa kujitolea au wa serikali akatusaidia katika hili tutashukuru"Gaitan Mahembe,baba mzazi wa Greyson Mahembe,askari anayedaiwa kujinyonga
"Hakuna picha inayoonesha marehemu alijinyonga au ananing'inia, ukweli wake ndio uliomponza, marehemu alisema kwanini nihangaishwe wakati mimi nilitumwa? wakubwa wenyewe wapo, mimi nilikuwa ni mtekelezaji"Gaitan Mahembe, baba mzazi wa Greyson Mahembe, askari anayedaiwa kujinyonga