Akiongea na Azam News, Baba mzazi wa askari aliyejinyonga anasema hajaridhishwa na taarifa za kifo cha mwanae!
Anasema alipigiwa simu na kuambiwa mwanao tumpeleke akazikwe wapi? Akawaambia mleteni nyumbani kwangu Tabata, Dar Ea Salaam.
Walipofika wakataka kushusha maiti na kuondoka, ndipo alipowagomea na kuanza vurugu baadae maiti ikaenda kuhifadhiwa hospitali ya polisi kilwa road.
Baba mzazi ana mashaka na kifo cha mwanae, anasema mwanae ameuwawa kwa kuwa mwanae alisimamia ukweli kuwa alitumwa na wakubwa wake kufanya mauaji ya mfanyabiashara.
Baba mzazi anamuomba IGP Sirro kuunda tume kuchunguza kifo hiko. Anasema haiwezekani sero ya polisi kuwe na tambala!
Baba mzazi wa marehemu ni askari mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.