Baba mzazi wa Askari Polisi anayedaiwa kujinyonga Mtwara adai kutoridhishwa na taarifa ya mwanae kujiua

Baba mzazi wa Askari Polisi anayedaiwa kujinyonga Mtwara adai kutoridhishwa na taarifa ya mwanae kujiua

Kama alitumwa kuuwa na akakubali huo ni upumbavu wake.
Kwani angegoma angefukuzwa Kazi?
Ndiyo yaleyale ya Urio aka homeboy. Amri za kijeshi huwaga hazina maswali.wewe unatekeleza tuu amri ya bosi. kawaulize wale askari wa Hai,chini ya SABAYA.ambao leo hii unamsikia Sabaya pekee yake anahangaika na mikesi.Hata makonda wale askari walioingia clouds huwezi wapata.ila makonda unaweza mpata.


Huyo alikuwa shahidi mhimu angeeleza jinsi alivyotekeleza amri ya mkubwa wake
 
Wamemuuwa polisi wenzake kwenye ili kupindisha kesi, safari hii jamuhuri isifanye uzembe wa Kama kesi ya zombe ambapo kwa kujua kesi itakavyokuwa walimtorosha SADI aliyeamuliwakupiga risasi wafanyabiashara na kupora pesa, Askari aliyetubu na kueleza ukweli aliuwawa kabla ya ushaidi wake kupokelewa Kama kizibiti. So walipunguza nguvu ya mashaidi. Ndicho walichofanya Hawa polisi wa kihuni, alafu polisi wanamdharau Sana mama, mbona yule baba aliyefariki masika mwaka Jana hawakumchezeachezea figisu, dharau mama wamezidi ukiwaachia waendelee kuuwa uwa raia wema, iko siku watajaribisha kwenu viongozi, oooh nyie wachekeeni
Huyo Sadi yupo wapi.
Maana wa Mahenge waliapa kulipiza kisasi kwa majambazi hao
 
Nyepesi nasikia, hao hao wakubwa wa juu walipoenda huko Mtwara kuwahoji askari walohusika, aliye jinyonga alisimamia ukweli kuhusu kila kitu kilichotokea. Nasikia walimwijia juu, na kumtisha saana. Askari alie huyo baada ya kutoka kuhojiwa alieleza kwao nyumbani kilichojiri kwamba katishwa saaana.
Japo baadae alipiga simu na kumwambia mama yake mambo si mabaya, na baada ya hapo wakapewa taarifa kajinyonga. Hili swala Rais aingilie kati tu, kama Kikwete alivyofanya na kuunda tume huru kwenye sakata lile la Zombe. Huyu Mkuu wetu wa jeshi la Polisi hakuna kitu.
CHAI CHAI
 
Huyo kauliwa na mapolisi ili wamsingizie kesi ,uhuni umerudi tena serikalini mama anaangaika na mambo ya kipumbaavu vya machifu na kuvaa ngozi ,wakati nchini mambo yanaharibikaHuyo kauliwa na mapolisi ili wamsingizie kesi ,uhuni umerudi tena serikalini mama ana angaika na mambo ya kipumbaavu vya machifu na kuvaa ngozi ,wakati nchini mambo yanaharibika
Yupo bize na vi Birthday na kupigia simu akina Mwijaku,. Ameshaingia kwenye Mtego wa kusifiwa na kuabudiwa
 
Hapo jaji awape kesi mbili za mauaji.
Moja ya mfanyabiashara mbili ya jambazi mwenzao. Kesi ya tatu uporaji. Jumla ya miaka 90 KILA mmoja inawatosha
 
Dah hii

Dah hizi kazi za haya majeshi hazifai bas kabisa..
Bora nikamwage pili pili zangu hoho barbrn,
Kazi ni kutumwa kuua mtu asokua na hatia na hutakiwi kukataa
Ila hatia,laana,kuwindwa na ndugu kimwili na kiroho shughuli unabakia nayo wewe muuaji. Waliokutuma wanachoma nyama. Hapa ni za kuambiwa
 
Ccm na police wanalindana kuwapora wananchi kwa common interests za kulindana.
Mmoja anapora kura zetu mwingine anapora pesa zetu. Ndo maana ma police wanauchikia Sana upinzani.
 
Wamemuuwa polisi wenzake kwenye ili kupindisha kesi, safari hii jamuhuri isifanye uzembe wa Kama kesi ya zombe ambapo kwa kujua kesi itakavyokuwa walimtorosha SADI aliyeamuliwakupiga risasi wafanyabiashara na kupora pesa, Askari aliyetubu na kueleza ukweli aliuwawa kabla ya ushaidi wake kupokelewa Kama kizibiti. So walipunguza nguvu ya mashaidi. Ndicho walichofanya Hawa polisi wa kihuni, alafu polisi wanamdharau Sana mama, mbona yule baba aliyefariki masika mwaka Jana hawakumchezeachezea figisu, dharau mama wamezidi ukiwaachia waendelee kuuwa uwa raia wema, iko siku watajaribisha kwenu viongozi, oooh nyie wachekeeni
Lakini hata kesi ya Zombe na wenzake baada ya tume kuundwa na kutoa majibu kuhusu ukweli, tatizo likaja kwenye uandishi wa mashitaka!

Mtu wa taaluma hiyo alipokwisha kulambishwa mlungula akajifanya mamuma wa taaluma, akaandika kesi miguu juu kichwa chini, hali iliyofanya Zombe akaonekana ni muungwana, afisa mpole na hajashiriki kabisa kwenye mauaji hayo na kuachiwa huru kula pensheni na hewa tulivu ya uraiani!

Na hata sasa nasikia harufu ya mambo hayo kujirudia ingawa Makamo kafoka sana hadi povu limemtoka kumshurutisha Igp aingilie kadhia ya mauaji yanayoendelea kote nchini, lakini mwisho wa jambo hili tusitarajie lolote la maana.
 
Kama kundi zima la watuhumiwa walikuwa wameswendekwa ndani, ni nani aliyeshawishi na kusimamia mauwaji ya polisi mtuhumiwa mwenzao aliyefia mahabusu?

Hii cyndicate inamgusa moja kwa moja Rpc na viongozi wengine wakubwa wa polisi mkoa kama Rco!

Hawa watu wakiwekwa pembeni ama nao kuunganishwa katika tuhuma itasaidia kuupata ukweli wa jinsi mnyororo wa wauwaji ulivyokuwa umejipanga na kutekeleza uovu huo.

Kuwaacha hawa watu muhimu kuendelea kuvaa magwanda ya polisi na kukalia viti vya nyadhifa zao watasaidia kupotosha na kupoteza uelekeo wa kupata ukweli wa jambo hili haraka.
 
Back
Top Bottom