Baba mzazi wa Askari Polisi anayedaiwa kujinyonga Mtwara adai kutoridhishwa na taarifa ya mwanae kujiua

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Akiongea na Azam News, Baba mzazi wa askari aliyejinyonga anasema hajaridhishwa na taarifa za kifo cha mwanae!

Anasema alipigiwa simu na kuambiwa mwanao tumpeleke akazikwe wapi? Akawaambia mleteni nyumbani kwangu Tabata, Dar Ea Salaam.

Pia soma Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga (26/01/2022)

Walipofika wakataka kushusha maiti na kuondoka, ndipo alipowagomea na kuanza vurugu baadae maiti ikaenda kuhifadhiwa hospitali ya Polisi Kilwa Road.

Baba mzazi ana mashaka na kifo cha mwanae, anasema mwanae ameuawa kwa kuwa mwanae alisimamia ukweli kuwa alitumwa na wakubwa wake kufanya mauaji ya mfanyabiashara.

Baba mzazi anamuomba IGP Sirro kuunda tume kuchunguza kifo hiko. Anasema haiwezekani sero ya polisi kuwe na tambala!

Baba mzazi wa marehemu ni askari mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

=====

Your browser is not able to display this video.
 
Akiongea na Azam News, Baba mzazi wa askari aliyejinyonga anasema hajaridhishwa na taarifa za kifo cha mwanae!

Anasema alipigiwa simu na kuambiwa mwanao tumpeleke akazikwe wapi? Akawaambia mleteni nyumbani kwangu Tabata, Dar Ea Salaam...
Baba mzazi ana mashaka na kifo cha mwanae, anasema mwanae ameuwawa kwa kuwa mwanae alisimamia ukweli kuwa alitumwa na wakubwa wake kufanya mauaji ya mfanyabiashara.

Baba mzazi anamuomba IGP Sirro kuunda tume kuchunguza kifo hiko. Anasema haiwezekani sero ya polisi kuwe na tambala
 
ASKARI ALIYESHTAKIWA KWA MAUAJI AJINYONGA MAHABUSU KWA TAMBALA LA KUDEKIA


ASP Greyson Mahembe ambaye ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi anayedaiwa kujinyonga kwa tambala la kudekia akiwa mahabusu ya kituo cha Polisi Wilaya ya Mtwara, Mkoani Mtwara.

Greyson alikuwa miongoni mwa Maafisa wengine wa Polisi saba wanaotuhumiwa kuumua kijana Mussa Hamisi (25) ambaye ameuawa baada ya kudai fedha zake shilingi Milioni 33.7 ambazo Maafisa hao wanadaiwa kuzichukua kutoka kwa kijana huyo baada ya kumfanyia upekuzi, uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Source : millard ayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…