Baba mzazi wa Askari Polisi anayedaiwa kujinyonga Mtwara adai kutoridhishwa na taarifa ya mwanae kujiua

Baba mzazi wa Askari Polisi anayedaiwa kujinyonga Mtwara adai kutoridhishwa na taarifa ya mwanae kujiua

"Mimi na familia yangu hatujaridhishwa, tunamuomba IGP alifafanue hili na ukweli uwekwe wazi. Hatuna kipato, hivyo tunaomba tupate mwanasheria wa kujitolea au wa serikali akatusaidia katika hili tutashukuru"Gaitan Mahembe,baba mzazi wa Greyson Mahembe,askari anayedaiwa kujinyonga https://t.co/zFXRBwxek8
 
"Ndugu yetu aliitwa wakati marehemu alishapelekwa hospitali ya Ligula na akaoneshwa michubuko akielezwa ni ya kamba, kisha akaambiwa ni ya tambara la deki, hivi mahabusu ya jeshi kuna tambara la deki?" Gaitan Mahembe, baba mzazi wa Greyson Mahembe, askari anayedaiwa kujinyonga https://t.co/1ezV2Sk4KQ
 
"Kama mwanangu alijinyonga wangeitwa ndugu upande wetu wakathibitishe au tungeoneshwa picha hata za kutoka jeshi la polisi zikionesha amejinyonga, au picha zozote kwenye vyombo vya habari. Hakuna hilo" Gaitan Mahembe, baba mzazi wa Greyson Mahembe, askari anayedaiwa kujinyonga https://t.co/Su4FKmdQKc
 
"Tuliwaambia askari waliouleta mwili, safari yetu ni ya Iringa lakini hatuwezi kuupokea hadi mtueleze, mwanangu ni afisa wa jeshi alitakiwa asindikizwe kijeshi na azikwe kijeshi kwanini halikufanyika hilo"Gaitan Mahembe, baba mzazi wa Greyson Mahembe, askari anayedaiwa kujinyonga https://t.co/0TrfFANEOK
 
"Polisi walifanya mambo haraka, wakaleta mwili hadi kwangu Segerea haraka walipofika wakawa wanasema shusha hapa, tukakataa nusura tupigane, tukawaambia mwili huu ukahifadhiwe kisha tuje hapa tuzungumze" Gaitan Mahembe, baba mzazi wa Greyson Mahembe, askari anayedaiwa kujinyonga https://t.co/gzxb5o3EeL
 
"Nilipewa taarifa kuwa mwanao ameshikiliwa kwenye mahabusu ya Polisi, na Januari 22, 2022 nilipigiwa simu kuwa bahati mbaya mwanao amejinyonga, jambo ambalo lilinistua sana" Gaitan Mahembe, baba mzazi wa askari anayedaiwa kujinyonga Greyson Mahembe https://t.co/Ef1tshRwrD
 
Kifo cha askari polisi aliyedaiwa kuhusika katika mauaji ya mfanyabiashara wa madini Mtwara na kisha kujinyonga akiwa mahabusu, kinazidi kuibua utata baada ya baba mzazi wa askari huyo kueleza kwamba taarifa za mazingira ya mtoto wake kujinyonga akiwa mahabusu haziridhishi. https://t.co/ULU5Utb6Tu
 
Askari7 wako mahabusu,siku ya pili mmoja akajinyonga na tambala
1.Polisi Mtwara wanazo mahabusu nyingi kila askari alifungiwa chumba chake?
2.Kama waliwekwa pamoja imetokeaje askari mmoja akajinyonga bila kumzuia?
3.Imetokeaje kukawa na kitu cha kuwezesha ha mahabusu kujinyonga?
 
"Hakuna picha inayoonesha marehemu alijinyonga au ananing'inia, ukweli wake ndio uliomponza, marehemu alisema kwanini nihangaishwe wakati mimi nilitumwa? wakubwa wenyewe wapo, mimi nilikuwa ni mtekelezaji"
Gaitan Mahembe, baba mzazi wa Greyson Mahembe, askari anayedaiwa kujinyonga https://t.co/QyZRDHG7tF

Kupitia DarMpya Blog imeripotiwa kuwa baba mzazi wa Polisi anayedaiwa kujinyonga akiwa mahabusu akiwa ni miongoni mwa polisi waliokuwa wakishikiliwa Kwa kumuua mfanya biashara na kumpora milioni 70 amezua mapya. Mzee huyo anadai kifo Cha mwanaye kinatia mashaka mno na Kuna uwezekano mwanaye huyo aliuawa pale alipotaka kuwachoma wakubwa waliokuwa nyuma ya mauaji ya mfanyabiashara huyoView attachment 2098697View attachment 2098699View attachment 2098700View attachment 2098701
Mungu atalitupia mgongo Taifa la tz sio mda kutokana na Mambo yanayoendelea,
 
Baba anakiri mwanae alimuua kijana Musa asiye na hatia, naye anaomba huruma ya wananchi, kama kweli Baba mzazi anakili mwanae aliua, hata angebaki Hai si Bado hukumu yake ingekua kunyongwa hadi kufa....
Kwasababu Musa aliuwawa kwa kuchomwa sindano ya sumu. Uwezekano mkubwa ni askari mmoja alifanya hivyo. Wengine ni “accomplices”
 
Tambarara la deki ni nguo chakavu na haina uwezo wa kubeba kilo 70
Yaani haya majibu ya polisi yananifanya nielewe polisi wanahisi raia akili hatuna.Babake marehemu kasema kawaida tukio la kujinyonga ilibidi apigwe picha au ndugu aitwe kushuhudia .lkn yote hayo hayakufanyika.Na bado tuwaamini marehemu alijinyonga tena mbaya zaidi na tambara la deki?Tena akiwa mahabusu. Hilo tambara la deki lenye urefu wa kutosha kujinyonga na uimara wa kubeba mtu mzima let say kg 70 ni la aina gani?

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
"Hakuna picha inayoonesha marehemu alijinyonga au ananing'inia, ukweli wake ndio uliomponza, marehemu alisema kwanini nihangaishwe wakati mimi nilitumwa? wakubwa wenyewe wapo, mimi nilikuwa ni mtekelezaji"
Gaitan Mahembe, baba mzazi wa Greyson Mahembe, askari anayedaiwa kujinyonga https://t.co/QyZRDHG7tF

Kupitia DarMpya Blog imeripotiwa kuwa baba mzazi wa Polisi anayedaiwa kujinyonga akiwa mahabusu akiwa ni miongoni mwa polisi waliokuwa wakishikiliwa Kwa kumuua mfanya biashara na kumpora milioni 70 amezua mapya. Mzee huyo anadai kifo Cha mwanaye kinatia mashaka mno na Kuna uwezekano mwanaye huyo aliuawa pale alipotaka kuwachoma wakubwa waliokuwa nyuma ya mauaji ya mfanyabiashara huyoView attachment 2098697View attachment 2098699View attachment 2098700View attachment 2098701
Je ni kazi gani ya uaskari ina baraka?
 
Back
Top Bottom