DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Dokta Hashimu Titho Kilosa alikua ni mwanafunzi wa udaktari bingwa katika Chuo cha Muhimbili na pia ni mtumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini (Mtwara).
Juhudi za kumtafuta Dk.Hashimu zilianza mwanzoni mwa mwezi wa tano baada ya kutopatikana kwa takribani wiki moja, ambapo baba yake, mzee Titho Kilosa ilimbidi kufika Dar es Salaam kufuatilia kilichojiri.
Siku ya Juni 04, 2025, iliweza kuthibitika kuwa mwili wa Dr. Hashim kuwa uliokotwa mnamo Aprili 24, 2025, maeneo ya Coco Beach, na taarifa hiyo kutolewa na Polisi siku hiyo hiyo.
Dk.Hashimu ni mtoto wa tatu katika familia ya watoto sita wa Mzee Titho Kilosa ambaye makazi yake yapo mkoani Morogoro.
Chanzo: The Chanzo
