Baba wa Manabii na Mitume wote Ibrahimu au Abrahamu alikuwa Dini gani?

Uwashauri sasa baadhi ya ndugu zako. Maana hao ndiyo wako mstari wa mbele kwenye kudhihaki imani ya watu wengine.
 
Katika kuukuta UKRISTO safari ilianza hivi-
1- IBRAHIMU ALIMZAA ISAKA.
2- ISAKA ALIWAZAA ESAU NA YAKOBO.
3- YAKOBO alizaa mataifa 12 ya ISRAEL.
Katika mtiririko huu wa vizazi baada ya vizazi UNAKUTANA na kuzaliwa kwa YESU KRISTO ambaye HAKUJA kuitengua Torati Bali KUITIMILIZA. matukio yote , matendo yake yote yalifanyika kwa WAYAHUDI.

kifo chake na ufufuko wake, ndiyo UKRISTO ulipotapakaa na kutufikia hadi sisi huku nje ya UYAHUDI. ndo maana ya HABARI NJEMA KWA WOTE.
 
Hivi ni vichwa vya Train vyenye njia tofauti za kuendesha injini,zinazotofautiana kutokana na wakati.

Kichwa cha kwanza kiliitwa steam Locomotive engine,kilitumia mvuke miaka ya 1800 hukoo!.
Kichwa cha pili, kinaitwa Deasel Locomotive engine ambacho kiligunduliwa miaka ya 1900 huko na
Kichwa cha tatu,kinaitwa electrical locomotive engine.

Mkuu!Pamoja na vichwa hivi kutofautiana katika mfumo wa kuendeshea ingini,bado vyote vinapita katika njia yenye kufanana yaani Rail.

Sasa na katika Uslamu ni hivyohivyo kwa maana mitume wote walipita katika Dini(njia) ya Uslamu lakini kwa nguzo tofauti.

 
Alikuwa myahudi. No 2 ways about it. Japo wazee wa kung’ang’ania vitu vya watu watadai alikuwa team mnyaazi[emoji23] jamaa hawa huenda wakadai hata baraba alikuwa mvaa kubadhi[emoji23]. Hawanaga aibu wala haya
Maneno matupu bila uthibitisho ni sawa na Chai tu bila sukari.
 
Mkuu!
Unaielezeaje hii aya?

وَجَاهِدُوا فِي اللَّهِ حَقَّ جِهَادِهِ ۚ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ ۚ مِّلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ ۚ هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ مِن قَبْلُ وَفِي هَـٰذَا لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ ۚ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَاعْتَصِمُوا بِاللَّهِ هُوَ مَوْلَاكُمْ ۖ فَنِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ

(AL -HAJJ - 78)
Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur'ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa.

22:78 Quran
Strive for ˹the cause of˺ Allah in the way He deserves, for ˹it is˺ He ˹Who˺ has chosen you, and laid upon you no hardship in the religion—the way of your forefather Abraham. ˹It is Allah˺ Who named you ‘the ones who submit’1 ˹in the˺ earlier ˹Scriptures˺ and in this ˹Quran˺, so that the Messenger may be a witness over you, and that you may be witnesses over humanity. So establish prayer, pay alms-tax, and hold fast to Allah. He ˹alone˺ is your Guardian. What an excellent Guardian, and what an excellent Helper!
 


Mkuu, very nice.

Tafadhali nitafutie ile aya ambamo Allah anasema maneno yanayofanana na haya; "Amewausia manabii dini--- ya kwamba wasimshirikishe Allah na chochote---"

Hiyo aya inayo maneno yanayofanana na hayo niliyoyaandika ila nimesahau mtiririko wake na ipo wapi katika Qur'an , hiyo aya ndiyo inajibu nini maana ya neno الدين lilotumika hapo kwenye hiyo aya uliyoileta kwani neno Dini, mbali, na maana ya Religion linazo maana zingine nazo waweza kuzipata kulingan na context ya aya.

Mfano katika 1:5,
ملك يوم الدين Maliki yaumi din, yaani; Mmiliki wa SIKU YA MALIPO, hapo utaona neno "Dini" limetafsiriwa kuwa "malipo" ya siku ya Qiyama..
 
Umeeleza na kufafanua vizuri mkuu🙏
 
Ibrahimu hakuwa myahudi bali alikuwa mkurdi kutoka Iraq.
Ibrahim alimzaa ISAKA
Isaka akamzaa YAKOBO
Yakobo akazaa wana 12 ambao ndiyo makabila 12 ya Israel (Wayahudi).
So, kama Ibrahim ndiye chanzo cha hao Wayahudi, jibu ni wazi tu kuwa alikuwa Myahudi
 
Maneno matupu bila uthibitisho ni sawa na Chai tu bila sukari.
Uthibitisho unaotaka wewe ni upi? Nenda kamfufue huko middle east umuulize, vinginevyo hakuna mahali utapata huo uthibitisho. Kila mtu atakuja na jibu lake.
 
Bora wewe unayejaribu kuyafundisha haya mapumbavu yanayocrame lugha za mudi na ndugu zake bila kufikiria
 
Kwa uchache niseme t
kwa hiyo Yesu alikuwa Dini gani?
 
Sie African kipindi hicho tulikuwa wap
 
Wakristo wote wanafahamu Ukristo ulianza baada ya Yesu kuja na kwamba agano la kale liliandikwa na watu wa dini ya Uyahudi. Sijui wewe hizi porojo zako na matango pori uliyoandika hapa ulilishwa na nani?!
Eti Wakristo wote!! Unaposema wote unamjumuisha hadi huyu Yohana jirani yangu? 😂

Hatakama Wakristo wanaamini Abraham hakuwa mkristo lakini wanaamini kabisa Mungu aliyemteua Abraham ndiye baba wa Yesu huyo huyo aliyekuja miaka mingi baadae. Lakini hii si imani ya Wayahudi wa wakati huo au wa leo.

Kwa Waislam wanaamini tangu Adam alikuwa Muislam! Sio kwamba alikuwa akipiga swala tano kama ilivyo kwa Waislam baada ya Muhammad bali ni kwasababu alikuwa ni mwenye kuamini (Mungu). Wanaamini wote waliopita ilikuwa ni mtiririko wa Mungu huyu huyu aliyemtuma Muhammad, Waristo hawakubali maana hawaamini katika Uislam ila wao kuamini Mungu wa Ibrahim ndiye Mungu wa Petro ni sawa😂
 
Hicho kitabu chenyewe sasa
 
Ibrahim alimzaa ISAKA
Isaka akamzaa YAKOBO
Yakobo akazaa wana 12 ambao ndiyo makabila 12 ya Israel (Wayahudi).
So, kama Ibrahim ndiye chanzo cha hao Wayahudi, jibu ni wazi tu kuwa alikuwa Myahudi
Ibrahim alimzaa Ishmael,
Ishmael akamzaa KEDARI,
KEDARI akazaa wana 12 ambao ndiyo makabila 12 ya waarabu (Waislamu).
So, kama Ibrahim ndiye chanzo cha hao Waislamu, jibu ni wazi tu kuwa alikuwa Muislamu.


[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaani kirahisi tu!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…