Baba wa Mwimbaji wa Injili aliyeimba "Mnatuona Nyani tu" ahukumiwa miaka 3 jela kwa kuendesha Kanisa bila kibali

Sawa Mudi
Ni GOOGLE vizuri hata huko nyuma nilikwisha sema mimi ni Mkristu wa madhehebu ya RC. Lakini lazima niseme kweli wakati hivi vidhebu uchwara vya kipentekoste vinaharibu UKRISTU wetu wote
 
Hivi unajua Nyerere alilipiga marufuku kanisa/dhehebu la Mashahidi ya Yehova? Kila kitu kinataratibu zake sio holelaholela
Mwaka gani?

Mashahidi wa Yehova mbona walikuwa wanakuja kwetu Upanga?
 
Ni kweli kabisa.

Ila kuna watu wanajitoa ufahamu kwa mahaba/ujinga.
 
Madhehebu ya kishenzi yanafahamika, mengi ni haya ya walokole
Wewe unavyosema madhehebu ya mwenzako ni ya kishenzi, na mwenzako anasema madhehebu yako ni ya kishenzi.

Haponi mtu hapo.

Serikali ijikite kuwekeza kwenye elimu iki watu waweze kuchagua mbivu na mbichi vizuri.

Ikijiingiza kwenye kufungia makanisa kwa sababu hayana usajili itakuwa inakosea sana na inaanzisha moto isioweza kuuzima.
 
Ukomunisti ulijaribu kupiga marufuku dini.

Ukomunisti umekufa, dini iko palepale.

Wapeni watu elimu wajue mbivu ni zipi na mbichi ni zipi.

Hizi habari za ku force central planning kwenye mambo ya utamaduni mtashindwa kama mlivyoshindwa kupata vazi la taifa kwa kutumia kamati ya Nchimbi.
 
Wakati kanisa katoliki chini ya papa likiongoza dola ya rumi liliomba wapi kibali cha kuendesha kanisa.
 
Hivi misikiti lazima ipate vibali vya serikali hata Ile midogo isiyo ya ijumaa?

Serikali ya Samia mnataka wenyewe maswali kama haya muanze kuita watu wachochezi wa kidini.
Hii serikali mkiiendekeza itawabadilishieni Kibla muangalie Chamwino Dodoma badala ya Maka.
 
Madhehebu ya kishenzi yapo, yanamwita Rais eti ni nyani. Inawezekana kabisa huyu baba ema ni shoga au analala na hiyo bi to yake, sintoshangaa huu uhuru holela unaosemwa. Baadaye itakuwa kanisa la kifisadi kama sodoma na ghomora huyu askofu a atembeaxna hawo waombaji wote. Tulishayaona, ni lazima kuyawahi.
 
Ni GOOGLE vizuri hata huko nyuma nilikwisha sema mimi ni Mkristu wa madhehebu ya RC. Lakini lazima niseme kweli wakati hivi vidhebu uchwara vya kipentekoste vinaharibu UKRISTU wetu wote
Sawa, ila msome vizuri huyo YESU utajua changamoto alizopitia. Mbingu sio mchezo ila kuna mataji kutokana na kile ulichokifanya.
 
Ushahidi huo unao ?!!!

Wewe una HALLUCINATIONS?!!![emoji15][emoji1787]

Ni "auditory"?!!!

BWANA ASEMA....TIINI MAMLAKA!
Hivi vitu vinahitaji akili kubwa ndugu, Unataka ushahidi subiri utaukuta siku ya Judgement, alafu sio kila kinachofanyika ukitii tu, utasubiri sana ukombozi si lelemama ndugu.
 
Yaani dini iruhusiwe kuitukana Serkali. Ni wapi Quraan au Biblia inasema Rais ni nyani?
Mmh hayo maneno umeyaona wapi? Punguzeni mahaba basi msikilize kwa makini na mpende kufatilia taarifa kwa usahihi
 
Well said
 
Hivi vitu vinahitaji akili kubwa ndugu, Unataka ushahidi subiri utaukuta siku ya Judgement, alafu sio kila kinachofanyika ukitii tu, utasubiri sana ukombozi si lelemama ndugu.
Ukombozi upi?!!!

Delusion
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…