CHADEMA wawe tu makini na yafuatayo:-
1. "Join the chain" ilikuwa ni turufu kubwa sana kwenu kuliko maridhiano mliyoyakimbilia na kuelekeza nguvu kubwa huko kiasi sasa haijulikani
kama hiyo "join the chain" ipo au imekufa kifo cha ghafla. Sasa hivi ukisoma maandiko mbali mbali utaona viongozi na wafuasi
wengi wa CHADEMA wamekomaa na maridhiano badala ya kuendelea kupambana kujenga chama chao. Hatari yake ni kuwa huko mbele ya
safari ikitokea maridhiano yasipoleta yaliyotarajiwa huenda chama chenu kikayumba sana.
2. Hamjifunzi kuwa wasi wasi ni akili. Kamati kuu ilipanda ndege kwenda Mwanza enzi za JPM lakini mkatoka bila bila. Juzi kati hapa wakati
mpo kwenye mazungumzo ya maridhiano COVID 19 wakapewa "greenlight" mjengoni. Haya hawajakaa sawa jana huko Manyara BAVICHA
wakawekwa chini ya ulinzi. Zote hizi sio dalili njema kwa watu mnaojadiliana kuondoa tofauti zenu.
3. Na hata hili la Mbatia na msajili kuwabeba wakina Selasini linapaswa liwafumbue macho CHADEMA lakini bado watakuwa hawaoni wala
kuchukua tahadhari. Mtu kama Mbatia na NCCR kwa ujumla hawana ushawishi mkubwa kwenye siasa za nchi hii lakini wanafanyiwa figisu
kubwa kiasi kile. Vipi nyie CHADEMA mkiingia/mkiingizwa kwenye 18 hata kwa bahati mbaya tu itakuwaje? Si ndio chama kitafutwa kabisa?
Kwa mtizamo wangu naona ni vyema CHADEMA wakendelea kupambana usiku na mchana kuendelea kukijenga chama chao na wapunguze matarajio yao makubwa kwenye maridhiano. Na hili la kukamatwa BAVICHA pamoja na kuwa wameshaachiwa liwafumbue macho wajue kuwa safari bado ni ndefu sana kufika wanakotaka wao.