Babu Tale: P Diddy alituita chumbani kwake tukaangalie runinga, Swizz Beatz akatukataza na tukaondoka bila kuaga

Babu Tale: P Diddy alituita chumbani kwake tukaangalie runinga, Swizz Beatz akatukataza na tukaondoka bila kuaga

Nimeshangaa sana

Hawa watu wakienda kwa didy siku kibao wakahudhuria party

Hawajatuambia walichoona chochotee huko

Leo hii mnakuja

Ati pdidy akitualika chimban kwake

Sijui nani akawambia msiende mkaondoka bila kuoga

Huyu mwingine anasema ooh kweli tulialikwa kwa didy

Ila kuna mambo yalifanyika kwenye party siwezi kuyaongea hadharan

Yapi??tutajuaje kweli hamkuoga na mkakimbia

Tutajuaje hamkwenda chumban kwa didy.....

Kama mlikuwa kwa party mnasema kunamambo yalifanyika OK

Hamwezi kuyaweka hadharan
Mambo gani

Na kwanini hamtuamboa mkivyorudi mlijua siri Mungu hadhihakiwi

Wenzenu wameanza itwa fbi wote wakioshiriki ile party

Mnafundisha nn watoto wetu

G2k
Didyoil com
 
Mkuu hizo clip ni za muda mrefu walifanyiwa interview na millard ayo kipindi crew nzima ya Wasafi walivyoenda marekani hakuna sehemu Diamond kazungumza kuhusu Pdidy sema baada ya scandal za Pididy kuibuka kipindi hiki ndio zikaibuliwa hizo clip
 
Akihojiwa na Rick Media, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki ambaye pia ni Meneja wa msanii nguli Diamond Platnumz, Mh. Hamis Taletale au kwa jina maarufu Babu Tale amekiri walipoenda kumtembelea msanii P.Diddy, alionesha viashiria ambavyo wao hawakujua maana yake.

Mojawapo ya tukio la ajabu ni pale Diddy alipowakaribisha juu ghorofani wakaangalie runinga. Lakini mwenyeji wao waliyeenda naye, Produza Swizz Beatz aliwakataza kata kata. Na hata wakati wanaondoka hawakuagana na P Diddy.

Pia soma: Kitendo cha Diamond Platnums kwenda nyumbani kwa P. Diddy kimemlipa

Kesho yake Swizz alikuwa na party pia, walienda kushiriki na baada ya kumaliza Swizz aliwaonya tena wasije wakajaribu kwenda nyumbani kwa Diddy, Swizz aliwakabidhi kwa dereva awarudishe hotelini, huku akimpa maonyo makali dereva asije akajaribu kuwapeleka mahali popote.

Waseme tu ukweli kama mafuta yaliwaingia. Wanaogopa nini? Wajikaze kiume waseme ukweli.
 
Back
Top Bottom