Babu Tale: Wanaharakati uchwara siasa zimewashinda sasa wanashindana na Diamond Platnumz

Babu tale anakosea sana kuliingilia hili swala kisiasa. Atayaona matokeo yake. Bora angekaa kimya au angeiga busara za Diamond mwenyewe
Hata kujua nini unatakiwa kufanya, na nini hustahili, inahitaji akili.
 
Pesa tunazo za wastani na halali!! Nyie logeni,ueni na muingie frimasoni kulazimisha utajir wakipepo!! Tamaa mbele...
Achana na maneno ya mtaani hakuna pesa za mapepo, pesa yote inatengenezwa ulaya, tafuta pesa wewe
 
Mazingira walioishi kina Marley na Makeba ni tofauti na haya ya Tanzania.

Huko ambako wanajisifu kuwa watetezi wa haki kuna yale yale maovu na udhaifu kama huku kwingine panapolazumishwa paonekane pana udhalimu.

Ni mtafutaji wa riziki anayetazama maslahi yake kama wewe na mimi.
 
Mimi mpaka kesho ukiniambia tale ni mbunge huwa siamini. Imagine tu Tale ni Mbunge then kina Lissu, Mbowe, Lema, Sugu, Zitto, Heche, Msigwa eti sio wabunge. Watanzania tujitafakari kama tunataka kusonga mbele.
Wote uluowataja walipokuwa wabunge ulisonga mbele kwenye nini?
 
Mkuu samahan, sio kila mtu humu ni mwanasiasa au yuko upande fulani.
Jaribu kuwa objective wakati mwingine.
Angalia majibu ya Diamond kuhusu kadhia hii utajifunza kitu.
Hawezi jifunza huyo mkuu 🤣🤣 Yaan huyo jamaa utaumiza akili yako tu, ni totally hopeless, low IQ.
 
Siyo kweli,diamond ni msanii lakini ni mwananchi wa Tanzania hivyo ana haki ya kukipenda/shabikia chama chochote nchini.
Siasa siyo chuki mkuu.
Angalia washabiki wa YANGA,walimchangia MANARA alipoumwa hali ya kuwa yupo simba
DIAMOND ni mshabiki lialia wa YANGA,lakini sisi SIMBA tunanunua video zake.Mo anauza bidhaa zake kwa wanasimba na wanayanga
MWACHENI KIJANA WETU AFANYE MUZIKI,wivu tu!
 
soma upya nilichoandika. hasa mstari wa mwisho. Nimesema music is a universal language inamgusa kila mtu. ukijiegemeza upande mmoja upande mwingine lazima ukurushie mawe. na nimesema hata waliojiegemeza upande wa upinzani hasa chadema nao watarajie ipo siku watarushiwa mawe.

Lady Jaydee analijua hilo, ndiyo sababu tangu mwaka 2000 aliweka wazi kuwa mashabiki wake ni wa vyama vyote vya siasa, alikataa kujihusisha na chama chochote cha siasa iwe mikutano ya ndani au ya nje au kampeni. Jaydee hata akiwa nominated hakuna mtu atathubutu kurusha mawa kwa kigezo cha siasa kwamba yuko chama fulani.

Kwa kuwa Diamond ameshajitanabaisha kwa kutumia haki yake ya utanzania kuwa yeye ni mwana ccm kindakindaki, ni lazima wasio wana ccm wamrushie mawe. Ukipingana na hilo ujue wewe ni mwehu. Anachopaswa kufanya ni kuithibitishia BET kuwa hakubaliani na mawe anayorushiwa na atoe sababu za msingi na hasa ikiwa BET haipendi influence za siasa kwa wanamusic wanaokuwa nominated na wao. Huo ndiyo kweli, mengine yote ni porojo tu.

Aliyekosea zaidi ni Tale, ambaye tayari ni mbunge na ni meneja wa diamond kwa kuanza kupersonalize issue hiyo. angenyamaz akimya, yeye kama meneja wa Diamond, akasuka mikakati kulishughulikia jambo hilo kisayansi.
 
Wanafiki lazima mjibiwe
 
Chadema hawawezi kuelewa hilo
 
Mkuu wewe najua una uelewa mzuri tu na hata jibu lako linajieleza
Maana yangu hata diamond akijitanabaisha kwamba ni ccm mawe ya nini? tuchukulie 2025 anagombea uraisi na akapata unataka kuniambia atawahudumia waccm tu?
ILA sikatai wapo WAJINGA tena wengi tu wanaodhani siasa ni uadui na ndio hao unaowazungumzia.
Kuwa CCM,CHADEMA.CUF,ACT au NCCR.sio dhambi na si uadui na huku mtaani tunaishi hivyo(kindugu)
 
Mtu anayemnukuu Babu Tale,huyo hana tofauti naye,empty,empty,empty!!
Ukuwa na utimamu kichwani,huwezi hata kujinasibisha na mtu kama Babu Tale.
 
Ndiyo maana wakaitwa nyumbu
Sasa inaonekana diamond ana akili zaidi kuliko chama kizima kwa jinsi anadili na hii ishu(bwa mdogo kaonyesha ukomavu)sio tu kwenye muziki bali hata siasa(ccm inampika vizuri)
 
Mtu anayemnukuu Babu Tale,huyo hana tofauti naye,empty,empty,empty!!
Ukuwa na utimamu kichwani,huwezi hata kujinasibisha na mtu kama Babu Tale.
Huu ni mtazamo wako tu,lakini wala haiko hivyo,Babu tale ana akili tena vizuri na ndio maana WCB inasonga mbele,lakini bado analisemea jimbo na kuishauri serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…