Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Serikali imesitisha kwa muda utoaji wa tiba (miracle cure) unaofanywa na Babu wa Loliondo mpaka uchunguzi wa dawa unaofanywa na wataalamu wa serikali utakapothibitisha kuwa tiba yenyewe inafanya kazi kweli.

Pia serikali inataka kujiridhisha kuwa dawa ya Babu ni safi na salama kunywa ili isilete magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, typhoid, etc kwa wagonjwa.

Source: Clouds FM

Mimi nafiiri wizara ya afya imetekeleza wajibu wake wa kuwalinda raia wake kwa kufuata sheria ya chakula na dawa pamoja na ile ya tiba mbadala. Kama babu angekuwa anaombea tu watu bila kuwapa kitu cha kunywa nafikiri serikali isingeingilia kati. Unapochanganya spiritual healing pamoja na dawa ya kunywa hapo ndipo utata unapokuja. Ingekuwa afadhali kama hiyo dawa ingekua ya kujpaka au kuchangaja na maji na kuogea.

Iron Rock kwa kweli umenifariji mno na habari yako. Mimi mzazi wangu anasumbuliwa na figo na kisukari na ninajiandaa kumpeleka huko, ila kinachonichanganya wengine wanasema unachukua siku mbili umeshapata dawa, wengine wanasema wiki, wengine wanasema hata wiki mbili, basi hata sijui lipi ni lipi, nataka nichukue likizo ya wiki lakini naona huenda isitoshe kumuona babu. Haya mara serikali nayo imepiga stop, basi ndio niko njia panda.

zakaria kakobe shopping mall aka Full Gospel Fellowship pale sam Nujoma sasa itakosa wateja ..... hizi huduma nyingine za kiroho zimekua ghali kuliko hata huduma muhimu za kujikimu na maisha .... tunashukuru babu anatuonyesha mfano ..... hata mashuleni na vyuoni wale magenious watoe shule kwa vilaza kama msaada bila kuringa

Leonardo a big Thank you, button yangu imepotea ningekugongea. Ubarikiwe sana kwa jinsi mnavyozidi kutupasha habari za huko.

Serikali imesitisha kwa muda utoaji wa tiba (miracle cure) unaofanywa na Babu wa Loliondo mpaka uchunguzi wa dawa unaofanywa na wataalamu wa serikali utakapothibitisha kuwa tiba yenyewe inafanya kazi kweli.

Pia serikali inataka kujiridhisha kuwa dawa ya Babu ni safi na salama kunywa ili isilete magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, typhoid, etc kwa wagonjwa.

Source: Clouds FM

mbona akina kakobe hwajawahi kuambiwa wakathibishe dawa/tiba zao? wamuache askofu Laizer na KKT Arusha na mradi wao.

Hizo dawa safi na salama za serikali zinatibu ukimwi? Huu ni upumbavu wa hali ya juu.

Tuandamane kwa hili maana ni upumbavu wa hali ya juu. Eti kipindupindu. Ridikualas

Why now? kama alianza kutibu since mwaka jana. Hivi na maelfu wanaotibiwa na akina Ndodi, Matumbe, Kifimbo, Majimarefu, Majungu na wengineo, serikali imeshawathibitishia usalama?

zakaria kakobe shopping mall aka Full Gospel Fellowship pale sam Nujoma sasa itakosa wateja ..... hizi huduma nyingine za kiroho zimekua ghali kuliko hata huduma muhimu za kujikimu na maisha .... tunashukuru babu anatuonyesha mfano ..... hata mashuleni na vyuoni wale magenious watoe shule kwa vilaza kama msaada bila kuringa

umenena vyema

Serikali imesitisha kwa muda utoaji wa tiba (miracle cure) unaofanywa na Babu wa Loliondo mpaka uchunguzi wa dawa unaofanywa na wataalamu wa serikali utakapothibitisha kuwa tiba yenyewe inafanya kazi kweli.

Pia serikali inataka kujiridhisha kuwa dawa ya Babu ni safi na salama kunywa ili isilete magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, typhoid, etc kwa wagonjwa.

Source: Clouds FM
Imekula kwa edwadi lowassa iyo!!! Nasikia ilikuwa dili ya kujipatia umarufu na thuma za ufisadi kusahaulika!!

Habari zilitoka muda siyo mrefu huduma ya kutoa dawa kwa mchungaji loliondo imesimamishwa kwa muda hadi taratibu za afya na mazngra zitakapo kuwa sawa

Imekula kwa edwadi lowassa iyo!!! Nasikia ilikuwa dili ya kujipatia umarufu na thuma za ufisadi kusahaulika!!

kama hujui kitu nyamaza sio kukurupuka na kuongea vitu usivojua sana sana unaonekana mjinga .

Nilihoji hii kitu asubuhi!!! Inakuwaje mtu anaachiwa kugawa dawa kwa wananchi ambayo wala haijachunguzwa ubora na madhara yake. Nikashauri wasimamishe na kuomba watalaam wa WHO waichunguze.

Kwa vile inasemekana inaponya, naona itakuwa ngoma kwelikweli kuwakatisha watu ambao wana imani nayo tayari!!

kuna siku hawa serikali watatahitaji kupima maji yanayotumika kubatiza watu ...au hata haya majivu niliyopakwa leo...

ki msimgi hapo hawapimi dawa ila wanatafuta kipima nguvu za Mungu.......mungu anaweza kuniotesha mimi hapa akaseam: mwanangu Edson huo mti wa mlonge unaouona hapo mbele ni dawa ya kutibu a, b, c, d, e, f, g, ect...chukua majan yake chemsha na kisha wape watu na watapona....kupitia wewe nasi mtu mwingine.....

jaman kuna miti mingi ya aina hii..lakini Mungu kauchagua mlonge huu na mimi pekee ndo nitoe dawa.....sasa hapa si mti wa mimi tunapaswa kupimwa...maana mimi ni chombo tu ila mungu kupitia mimi anatibu watu.....hawa serikali ni wapumbavu wakubwa......

maana hapa wanatak kumjaribu Mungu...kwa nini wasitumie wale waliopina kujiridhisha? kipindu pindu huwa kinachukua mda gan jamani...shemeji yangu schola amepona kisukari na mpka leo amepona sasa, alikunywa sawa ya babu sasa hawa wanaema nini

hapan ndipo pa kuandamana ndugu zangu......

mmmm, labda wanataka kumtorosha akahudumie wakubwa ambao hawataki kuonekana hadharani kwanza ndipo wamrudishe! otherwise mi naona mazingira yanaweza kutengenezwa wakati wananchi wanaendelea kupata huduma

Back
Top Bottom