Badala ya kubinafsisha mashirika yanayotushinda kwa kampuni za nje kwanini tusitafute ma CEO kutoka nje, wenye uzoefu na kazi hizo?

Kwa hawa viongozi wabovu na wezi wa CCM hata umlete malaika hakuna kitu kitaenda, tatizo siyo watanzania tatizo ni mfumo wa upatikanaji wa hao watu
 
Njia Bora ya kuendesha mashirika na bado yakawa Mali yetu ni kukodisha menejimenti toka nje, unaweza kuwa na CEO toka nje lakini Bodi ya wazawa au maamuzi yanafanywa na wanasiasa tatizo likawa palepale
Inabidi kuwe na mabadiliko ya sheria au walau mkataba wa kazi umuhakikishie kutoingiliwa na wanasiasa na viwavi wengine. Bodi kama hazina tija tuachane nazo au zipunguziwe nguvu katika kuangalia utendaji wa kila siku.
 
Ni utapeli tupu
 
Ukweli usiopingika kabisa
 
Hapa umegusa kwenye msingi wa tatizo. Urais ndio tatizo.
Mobutu alionaga benki kuu ipo hovyo sana. Basi akatoa gavana wa Kiafrika na kuleta mzungu mwenye uzoefu. Mzungu akaingia na kufanya mabadiliko makubwa sana. Lakini akagundua shida ilipo. Mobutu mwenyewe na chawa wake walikuwa wameifanya benki kuu kama kibubu chao! Mzungu na mori wote wa kazi ukamuisha, akafunga virago vyake.

Watu wa juu ndiyo wanatakiwa kuwa wa kwanza kuhakikisha mashirika yanaenda kwa weledi. Wasipoonyesha hivyo kwa vitendo hakuna kinachoweza kufanyika hata CEO awe mzuri vipi.
 
Waswahili kuendesha kampuni kuna shida.
Mfano kampuni ya mabasi binafsi ya Scandinavia ilipoanzishwa walileta CEO mzungu kampuni ilikuwa Inaendeshwa kisasa na mabasi ya kisasa .ikakua vizuri mno .Mzungu alipoondoka yule CEO ikafa hadi leo
Kampuni ilikufa sumaye alipoondoka madarakani. I kaja awamu ya 4.
 
Nafasi za CEO zingekuwa zinatangazwa watu wanaomba na kupewa target
Ilitakiwa zote nafasi kubwa za umma kuanzia wakuu wa wilaya,mikoa,wakurugenzi wa Idara na taasisi ,wakuu wa mashirika na vitengo yao nk Zingekuwa za ushindani wa kuomba nchi ingepata viongozi wazuri sana.Wanaomba wengi wanafanyiwa interview na Panel independent. Raisi anapelekewa majina machache achague mojawapo .Hapo tutapata wakuu wa wilaya ,mikoa ,maafisa wakuu ea serikali wazuri sana.Ikitangazwa ruksa kuomba aliye ndani na aliye nje washindanishwe.Na akipata inatakiwa kuwa ya mkataba mfano wa miaka mitatu mitatu anayoweza ongezewa muda kutegemea na performance
 
Tatizo sio Ma C.E.O mimi naona mashirika yauzwe kwa wawekezaji wa ndani Serikali ichukue chake maisha yaende. Hawa wawekezaji wapewe masharti ya kuwauzia watanzania wenzao pindi watakaposhindwa. Hao watanzania watakaopewa nafasi ya kupewa hizi kampuni wawe watanzania halisi(Sio Wahindi wala Waarabu). Baaada ya kusafiri nchi mbali mbali duniani nimegundua Serikali Tanzania haiwapi kipaumbele Raia wake. Ukienda nchi nyingine mgeni hawezi kupendelewa kuliko Raia halisi wa nchi. Lakini Tanzania ni vice-versa. Haiwezekani mtu kama Mo ambaye ameshahamishia familia U.A.E unampa mashamba ya mikonge na anatishia kufunga kiwanda cha sukari unamdekeza. Mo ni muislamu wa Gujirati India ni mtu ambaye ni minority kule kwao kwa hio hafungamani na nchi anaenda palipo na maslahi. Hivi vitu inabidi umwezeshe mtu ambae ukoo wao wote na familia yake ipo hapa. Kenya na South Africa zimeeendelea kwa sababu matajiri wao wakubwa(wazungu) walikuwa settlers waliamua kuishi hapo kama nyumbani. Matajiri wakubwa bongo(wenye asili ya asia) wana ndugu Uarabuni, India, Uingereza, Canada na Marekani. Lazima Dola ipungue maana haiwezekani mtu awe na ndugu huko na asifanye uwekezaji huko. Kuna watanzania kibao wana mitaji wauziwe mashirika mazima kwa masharti wakishinda wawauzie watanzania wenzao. Hii italeta maendeleo makubwa sana.
 
Hata ukileta CEO kutoka Makampuni ya Wall Street au kwa lugha yao Fortune 500 bado watawajibika kwenye bureaucracy ya Serikali kama; Treasury Registrar, Board of Directors, Waziri wa Sekta husika, Kamati za hesabu za Bunge etc


Bado kuna Mamlaka ya Manunuzi ya Umma, Sekretariati ya Ajira, Sekretaria ya Maadili.

Huko ndiko kuna red tape ambayo inapunguza performance ya ma CEO.

Dawa pekee ni PRIVATIZE 80-90% kwa sekta binafsi halafu kaa pembeni kusubiri mgawo kama ambavyo NMB au CRDB wanavyo gawa
 
Kabisa, tatizo huku kwetu ni cheo Cha urais ambapo hugeuzwa Mungu mtu. Ukishaona mtu hashitakiwi akiwa au ametoka madarakani, hapo utegemee majizi kushika hatamu.
 
Hii ni siri ya nchi kuendelea ambayo viongozi wengi wa Kiafrika hawaifahamu au wanaifahamu ila wakipewa vimilioni kadhaa wanajidai hawaioni. Lazima uwezeshe wazawa ambao utahakikisha pesa inabaki humu humu kuendeleza nchi. Leo Mo ana nyumba ya dola milioni 50 Dubai. Hizo ni dola alizozipata huku. Dola ambazo zimeletwa na wakulima wa korosho, kahawa na wachimbaji. Kesho unalia kuna upungufu wa dola.
 
Na hiyo ndo akili....tutafute CEOs na baadhi ya operations managers kutoka nje na wakati wanaendesha wawepo wazawa wakijifunza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…