Badala ya kubinafsisha mashirika yanayotushinda kwa kampuni za nje kwanini tusitafute ma CEO kutoka nje, wenye uzoefu na kazi hizo?

Inaonekana wazi serikali haiwezi kuendesha shirika lolote. Mwendokasi na hasara za ATC ni mfano wa karibuni juu ya kushindwa huko. Mwendokasi unaenda kutafutiwa muwekezaji kutoka nje!! Huku ni kujirudisha nyuma maana muwekezaji huyo hata kama atatoa huduma nzuri namna gani lakini atachota uchumi wetu na kupeleka kwao.

Kwa nini mashirika haya yasitafutiwe ma CEO, ma CFO nk nk kutoka nje wenye uzoefu. Wapewe madaraka na malengo. Wakifeli wanatimuiwa na kuletwa wapya.

Kama vile kwa makocha wa timu za mpira? Kwanini tusitafute mameneja wa ATC kutoka Ethiopia na nchi nyingine zilizofanikiwa kwenye upande huo.

Kwanini tusisake duniani mameneja na watu wenye ujuzi na uzoefu wa kuendesha mwendokasi.

Kiuchumi gharama za kuwalipa wakuu hao ni ndogo sana ukilinganisha na hasara za kiuchumi zitokanazo na kuleta kampuni za kigeni.
Kwa hawa viongozi wabovu na wezi wa CCM hata umlete malaika hakuna kitu kitaenda, tatizo siyo watanzania tatizo ni mfumo wa upatikanaji wa hao watu
 
Njia Bora ya kuendesha mashirika na bado yakawa Mali yetu ni kukodisha menejimenti toka nje, unaweza kuwa na CEO toka nje lakini Bodi ya wazawa au maamuzi yanafanywa na wanasiasa tatizo likawa palepale
Inabidi kuwe na mabadiliko ya sheria au walau mkataba wa kazi umuhakikishie kutoingiliwa na wanasiasa na viwavi wengine. Bodi kama hazina tija tuachane nazo au zipunguziwe nguvu katika kuangalia utendaji wa kila siku.
 
Sikiliza: CCM haiwezi kufanya hivyo kwa sababu imejaa mafisadi. Lengo lao kuu ni kushibisha matumbo yao na siyo kuendeleza nchi. Hata huo mwendokasi kuna tetesi kuwa hao ''wawekezaji'' kutoka sijui Dubai, ni mama wa Kisimkazi amefungua li-kampuni lake huko na ndilo linakuja kufanya yake.
Ni utapeli tupu
 
60% ya watumishi hawana uwezo naa ndio hao wapo nafasi za juu ,wale walioingia kweny utumishi kwa uwizi.

Kumleta mzungu bila ya team yake ni nadra sana ndio maana hata makocha wakija wanataka wachezaji fulani wanaoendana nao...Mkuu nimefanya kazi kweny mashirika ya umma mengi ila ukweli usemwe hapa nimefunga.

Wabongo ni wapenda starehe na kama upo nondo lazima uletewe zengwe , watanzania ukiwaweka sehemu basi ni umbea tu.

Mwaka fulani nyuma ,siku moja huduma zilichelewa maana pale ofisini watu walihost part ya HDB ya kijinga ...Mda wa kutoka mtu hana mda wa kuangalia foleni ya wanaotaka kutoa huduma yeye anaondoka ikiwa lengo la kutoa huduma kwa siku bado hatujafikia .

Wanawake ni kichefuchefu hizo excuses mara mwanae kafanya hivi ni hatari sana ,kuwahi napo ni ovyo.

Haya mambo hata chuo ndio hivyo hivyo ,mkipanga discussion kesho basi excuses kibao hata kufika ni kutegeana ila watu wanataka wawe kweny front pages pale hata kwa kuhonga.

Sababu kubwa[emoji117] watanzania wengi hawapendi kazi wanazofanya ,wanachoshwa na kazi zao mapema zaidi ndani ya miaka 3 tu..Hawana morale kabisa siasi ni nyingi .

Ushauri[emoji117] kijana umri wa ujana ni wakufanya kazi kwa bidii ili kufika mbali ,hayo mambo mengine hayana mpango maendeleo ni muhimu kwa kizazi chako kuliko hizo bata unazokula .
Ukweli usiopingika kabisa
 
Hapa umegusa kwenye msingi wa tatizo. Urais ndio tatizo.
Mobutu alionaga benki kuu ipo hovyo sana. Basi akatoa gavana wa Kiafrika na kuleta mzungu mwenye uzoefu. Mzungu akaingia na kufanya mabadiliko makubwa sana. Lakini akagundua shida ilipo. Mobutu mwenyewe na chawa wake walikuwa wameifanya benki kuu kama kibubu chao! Mzungu na mori wote wa kazi ukamuisha, akafunga virago vyake.

Watu wa juu ndiyo wanatakiwa kuwa wa kwanza kuhakikisha mashirika yanaenda kwa weledi. Wasipoonyesha hivyo kwa vitendo hakuna kinachoweza kufanyika hata CEO awe mzuri vipi.
 
Waswahili kuendesha kampuni kuna shida.
Mfano kampuni ya mabasi binafsi ya Scandinavia ilipoanzishwa walileta CEO mzungu kampuni ilikuwa Inaendeshwa kisasa na mabasi ya kisasa .ikakua vizuri mno .Mzungu alipoondoka yule CEO ikafa hadi leo
Kampuni ilikufa sumaye alipoondoka madarakani. I kaja awamu ya 4.
 
Nafasi za CEO zingekuwa zinatangazwa watu wanaomba na kupewa target
Ilitakiwa zote nafasi kubwa za umma kuanzia wakuu wa wilaya,mikoa,wakurugenzi wa Idara na taasisi ,wakuu wa mashirika na vitengo yao nk Zingekuwa za ushindani wa kuomba nchi ingepata viongozi wazuri sana.Wanaomba wengi wanafanyiwa interview na Panel independent. Raisi anapelekewa majina machache achague mojawapo .Hapo tutapata wakuu wa wilaya ,mikoa ,maafisa wakuu ea serikali wazuri sana.Ikitangazwa ruksa kuomba aliye ndani na aliye nje washindanishwe.Na akipata inatakiwa kuwa ya mkataba mfano wa miaka mitatu mitatu anayoweza ongezewa muda kutegemea na performance
 
Inaonekana wazi serikali haiwezi kuendesha shirika lolote. Mwendokasi na hasara za ATC ni mfano wa karibuni juu ya kushindwa huko. Mwendokasi unaenda kutafutiwa muwekezaji kutoka nje!! Huku ni kujirudisha nyuma maana muwekezaji huyo hata kama atatoa huduma nzuri namna gani lakini atachota uchumi wetu na kupeleka kwao.

Kwa nini mashirika haya yasitafutiwe ma CEO, ma CFO nk nk kutoka nje wenye uzoefu. Wapewe madaraka na malengo. Wakifeli wanatimuiwa na kuletwa wapya.

Kama vile kwa makocha wa timu za mpira? Kwanini tusitafute mameneja wa ATC kutoka Ethiopia na nchi nyingine zilizofanikiwa kwenye upande huo.

Kwanini tusisake duniani mameneja na watu wenye ujuzi na uzoefu wa kuendesha mwendokasi.

Kiuchumi gharama za kuwalipa wakuu hao ni ndogo sana ukilinganisha na hasara za kiuchumi zitokanazo na kuleta kampuni za kigeni.
Tatizo sio Ma C.E.O mimi naona mashirika yauzwe kwa wawekezaji wa ndani Serikali ichukue chake maisha yaende. Hawa wawekezaji wapewe masharti ya kuwauzia watanzania wenzao pindi watakaposhindwa. Hao watanzania watakaopewa nafasi ya kupewa hizi kampuni wawe watanzania halisi(Sio Wahindi wala Waarabu). Baaada ya kusafiri nchi mbali mbali duniani nimegundua Serikali Tanzania haiwapi kipaumbele Raia wake. Ukienda nchi nyingine mgeni hawezi kupendelewa kuliko Raia halisi wa nchi. Lakini Tanzania ni vice-versa. Haiwezekani mtu kama Mo ambaye ameshahamishia familia U.A.E unampa mashamba ya mikonge na anatishia kufunga kiwanda cha sukari unamdekeza. Mo ni muislamu wa Gujirati India ni mtu ambaye ni minority kule kwao kwa hio hafungamani na nchi anaenda palipo na maslahi. Hivi vitu inabidi umwezeshe mtu ambae ukoo wao wote na familia yake ipo hapa. Kenya na South Africa zimeeendelea kwa sababu matajiri wao wakubwa(wazungu) walikuwa settlers waliamua kuishi hapo kama nyumbani. Matajiri wakubwa bongo(wenye asili ya asia) wana ndugu Uarabuni, India, Uingereza, Canada na Marekani. Lazima Dola ipungue maana haiwezekani mtu awe na ndugu huko na asifanye uwekezaji huko. Kuna watanzania kibao wana mitaji wauziwe mashirika mazima kwa masharti wakishinda wawauzie watanzania wenzao. Hii italeta maendeleo makubwa sana.
 
Hata ukileta CEO kutoka Makampuni ya Wall Street au kwa lugha yao Fortune 500 bado watawajibika kwenye bureaucracy ya Serikali kama; Treasury Registrar, Board of Directors, Waziri wa Sekta husika, Kamati za hesabu za Bunge etc

Bado kuna Mamlaka ya Manunuzi ya Umma, Sekretariati ya Ajira, Sekretaria ya Maadili.

Huko ndiko kuna red tape ambayo inapunguza performance ya ma CEO.

Dawa pekee ni PRIVATIZE 80-90% kwa sekta binafsi halafu kaa pembeni kusubiri mgawo kama ambavyo NMB au CRDB wanavyo gawa
 
Mobutu alionaga benki kuu ipo hovyo sana. Basi akatoa gavana wa Kiafrika na kuleta mzungu mwenye uzoefu. Mzungu akaingia na kufanya mabadiliko makubwa sana. Lakini akagundua shida ilipo. Mobutu mwenyewe na chawa wake walikuwa wameifanya benki kuu kama kibubu chao! Mzungu na mori wote wa kazi ukamuisha, akafunga virago vyake.

Watu wa juu ndiyo wanatakiwa kuwa wa kwanza kuhakikisha mashirika yanaenda kwa weledi. Wasipoonyesha hivyo kwa vitendo hakuna kinachoweza kufanyika hata CEO awe mzuri vipi.
Kabisa, tatizo huku kwetu ni cheo Cha urais ambapo hugeuzwa Mungu mtu. Ukishaona mtu hashitakiwi akiwa au ametoka madarakani, hapo utegemee majizi kushika hatamu.
 
Tatizo sio Ma C.E.O mimi naona mashirika yauzwe kwa wawekezaji wa ndani Serikali ichukue chake maisha yaende. Hawa wawekezaji wapewe masharti ya kuwauzia watanzania wenzao pindi watakaposhindwa. Hao watanzania watakaopewa nafasi ya kupewa hizi kampuni wawe watanzania halisi(Sio Wahindi wala Waarabu). Baaada ya kusafiri nchi mbali mbali duniani nimegundua Serikali Tanzania haiwapi kipaumbele Raia wake. Ukienda nchi nyingine mgeni hawezi kupendelewa kuliko Raia halisi wa nchi. Lakini Tanzania ni vice-versa. Haiwezekani mtu kama Mo ambaye ameshahamishia familia U.A.E unampa mashamba ya mikonge na anatishia kufunga kiwanda cha sukari unamdekeza. Mo ni muislamu wa Gujirati India ni mtu ambaye ni minority kule kwao kwa hio hafungamani na nchi anaenda palipo na maslahi. Hivi vitu inabidi umwezeshe mtu ambae ukoo wao wote na familia yake ipo hapa. Kenya na South Africa zimeeendelea kwa sababu matajiri wao wakubwa(wazungu) walikuwa settlers waliamua kuishi hapo kama nyumbani. Matajiri wakubwa bongo(wenye asili ya asia) wana ndugu Uarabuni, India, Uingereza, Canada na Marekani. Lazima Dola ipungue maana haiwezekani mtu awe na ndugu huko na asifanye uwekezaji huko. Kuna watanzania kibao wana mitaji wauziwe mashirika mazima kwa masharti wakishinda wawauzie watanzania wenzao. Hii italeta maendeleo makubwa sana.
Hii ni siri ya nchi kuendelea ambayo viongozi wengi wa Kiafrika hawaifahamu au wanaifahamu ila wakipewa vimilioni kadhaa wanajidai hawaioni. Lazima uwezeshe wazawa ambao utahakikisha pesa inabaki humu humu kuendeleza nchi. Leo Mo ana nyumba ya dola milioni 50 Dubai. Hizo ni dola alizozipata huku. Dola ambazo zimeletwa na wakulima wa korosho, kahawa na wachimbaji. Kesho unalia kuna upungufu wa dola.
 
Inaonekana wazi serikali haiwezi kuendesha shirika lolote. Mwendokasi na hasara za ATC ni mfano wa karibuni juu ya kushindwa huko. Mwendokasi unaenda kutafutiwa muwekezaji kutoka nje!! Huku ni kujirudisha nyuma maana muwekezaji huyo hata kama atatoa huduma nzuri namna gani lakini atachota uchumi wetu na kupeleka kwao.

Kwa nini mashirika haya yasitafutiwe ma CEO, ma CFO nk nk kutoka nje wenye uzoefu. Wapewe madaraka na malengo. Wakifeli wanatimuiwa na kuletwa wapya.

Kama vile kwa makocha wa timu za mpira? Kwanini tusitafute mameneja wa ATC kutoka Ethiopia na nchi nyingine zilizofanikiwa kwenye upande huo.

Kwanini tusisake duniani mameneja na watu wenye ujuzi na uzoefu wa kuendesha mwendokasi.

Kiuchumi gharama za kuwalipa wakuu hao ni ndogo sana ukilinganisha na hasara za kiuchumi zitokanazo na kuleta kampuni za kigeni.
Na hiyo ndo akili....tutafute CEOs na baadhi ya operations managers kutoka nje na wakati wanaendesha wawepo wazawa wakijifunza
 
Back
Top Bottom