Badala ya kubinafsisha mashirika yanayotushinda kwa kampuni za nje kwanini tusitafute ma CEO kutoka nje, wenye uzoefu na kazi hizo?

Kuuzia mashirika ya nje ni hasara kubwa kwa nchi. Kama kuprivatize basi iwe kwenda kwa wazawa hasa. Lakini tunaweza kufanya kitu ili kuyakinga mashirika haya ya kibiashara dhidi ya urasimu wa kawaida wa kiserikali ili kuyapunguzia hizo red tapes.
 
Shida sio CEO, shida ni mtazamo wa wafanyakazi. Nimewahi kufanya kazi nje ya Tanzania na baadae Tanzania. Niliyoyaona ni watanzania wanapenda kupata mishahara na marupurupu bila ya kuitolea jasho. Tanzania tuna kizazi kisichoamini kutimiza wajibu bali ujanja ujanja.
 
CEO wa nje hawezi kuleta hiyo culture ya kazi kazi kwenye shirika iwapo akipewa uwezo wa kufanikisha hilo?
 
Aiseee umeongea ukweli 100+%, na hapo ndo ambapo tunafeli, sio katika siasa wala maofisini hali ni hiyo hiyo, Sasa una mpata rais mwenye tabia hizo since Secondary na chuo, au waziri then tutegemee kutoboa? Never

Tukubali kufanya kazi kwa bidii, tutafute watu na kuwapa kazi, majukumu au kuajiriwa kwa kufuata merits za mtu na sio connection kama ambavyo tupo leo
 
Unaumwa wewe, maharage ndio wa kutolea mfano kwa mantiki anayosema mleta mada?
 
Kuuzia mashirika ya nje ni hasara kubwa kwa nchi. Kama kuprivatize basi iwe kwenda kwa wazawa hasa. Lakini tunaweza kufanya kitu ili kuyakinga mashirika haya ya kibiashara dhidi ya urasimu wa kawaida wa kiserikali ili kuyapunguzia hizo red tapes.
Hasara iko wapi ? Mbona NMB, TCC na TBL viliuzwa na vinafanya vizuri sana kwenye kodi na gawio?
 
Sheria zinazofanya mashirika ya umma yawe ngumu kufanikiwa,

Ugumu wa kufukuza mtu, pvt ukizingua, dakika ya pili tu huna kazi, serikalini mtu anajua anazingua ila zaidi zaidi watamuhamisha,

pia gvt kuna mapumziko mengi sana tofaut na pvt


Serikali inalipa mishahara mikubwa, (pvt unaweza lipa mishahara sawa na serikali ila kazi utapiga mara tatu ya serikalini)

Mlolongo wa manunuzi, kununua gari za mwendokasi inabidi waziri sijui nani ahusike,
 
CEO wa nje hawezi kuleta hiyo culture ya kazi kazi kwenye shirika iwapo akipewa uwezo wa kufanikisha hilo?
Hailetwi na CEO peke ake inabidi team nzima yenye authority full,
Ukileta CEO lakin bado anawajibika kwa waziri mara kamati za bunge, mara raia wapige kelele unakuwa umemfunga, si unaona viwanda vya wahindi kazi zinavyofanyika ? Ila njoo viwanda vya serikali
 
Hasara iko wapi ? Mbona NMB, TCC na TBL viliuzwa na vinafanya vizuri sana kwenye kodi na gawio?
Yanafanya vizuri lakini hao wawekezaji wanachukua sehemu kubwa ya faida wanayopata na kupeleka kwao. Na si kwamba wanachukua Tsh, wanachukua dola. Yaani humu wanafanya biashara kwa Tsh lakini wanapopeleka faida kwao wanaondoka na dola. Akiba yetu ya dola inapungua huku thamani ya pesa yetu ikizidi kuporomoka.
 
Mkipata ceo mchapa kazi kawaida atataka wanaofanana nae Magufuli alimwomba Mkapa ambadilishie katibu mkuu, akatolewa Odunga akapewa Kijazi na kazi ilionekana, unahitaji watu wawili au watatu hapo juu kuleta matokeo that's why nafasi za juu zitangazwe watu waombe apatikane anayeweza kufanya kazi kwa viwango vinavyotakiwa..mambo ya kuteua kwa sasa ni km kukirimu watu ulaji au waibe inajulikana hivyo wala huhitaji kufundishwa..lakin watu wanafahamu mabadiliko ya utawala ndani ya shirika yanapotokea wao pia watabadilika..
 
Ndiyo. Inatakiwa mkataba wa kazi umpe yeye na timu yake madaraka ambayo kazi yake haitaingiliwa lakini anaweza kuwajibishwa.
 
ataundiwa zengwe ataondoka mwenyewe bila kufukuzwa
 
CEO best Tanzania wapo. Tatizo kubwa ni politics za wakubwa. Usishangae waziri anakuja anatak mil 500 kwenye shirika ambalo wewe ni CEO na anakuambia katumwa na rais. So mpaka kizazi cha kutoa rushwa ili kishinde uchaguzi kife chote
 
Sio Mo tu kuna Manji Canada, Rostam U.A.E na Marekani, Bakhresa U,A,E, Somaiya India. Kuna madogo wa kihindi huku Ujerumani ambao ni Raia wa Zimbabwe, Tanzania na Uganda wana maisha mazuri kuliko wahindi kutoka India mpaka mimi nashangaa. Mpaka wahindi wananiuliza kumbe Afrika kuna hela. Wapo waliotoka India kukimbilia huku ila wamebadilisha mtazamo wakimaliza chuo wanakuja Afrika. Halafu tupo busy na mpira sijui Simba na Yanga. Yaani nchi ni kama mtu anaelewa na kufuja fedha huku bado amepanga hana hata kiwanja.
 
Ceo anayefahamu kazi anayopewa na amewekewa viwango vya kufikia cha kwanza atakuonyesha njia itakayomuwezesha kufikia malengo ikiwa ni pamoja na kuondoa red tape na bureaucracy zisizo za lazima..utakuwa mjinga wewe unayempa kazi km utakataa kufanya anayokushauri mtendaji! Hizo bureaucracy sio misahafu zinabadilishwa au hata kuondolewa kabisa kwa mwenye kutaka matokeo..!
 
Tena huko kwenye bodi za wakurugenzi ndio kabisa kuna watu weupe vichwani hamna kitu hupewa tu kama eneo la kupumzika tu.Wanakuwa hawana mchango wowote wa maana
Mahali ambako tunakosea ni huko kwenye bodi.
Utakuta bodi imejaa wastafuu.
Mtu ametumikia taifa mpaka amestaafu, bado unampa ujumbe wa bodi ili iweje?
Hawa wazee waachwe wapumzike, wapeni nafasi vijana wafanye kazi.
Kila mahali kwenye nchi hii tumejaza wazee.
Utaambiwa ni wazoefu, lakini mashirika wanayosimamia yanafirisika.

Kwa mtindo huo hatuwezi kupata tija.
 
Ndiyo. Inatakiwa mkataba wa kazi umpe yeye na timu yake madaraka ambayo kazi yake haitaingiliwa lakini anaweza kuwajibishwa.
Sasa hio haiwezekani, lazima awe anajibu kwa kamati za bunge, mawaziri nk,
Ukimpa full authority ni sawa na kumpa kampuni bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…