Bado Km 51 ili Kigoma-Dar iwe lami. Rais Samia anaenda kuunganisha mikoa yote kwa lami

Bado Km 51 ili Kigoma-Dar iwe lami. Rais Samia anaenda kuunganisha mikoa yote kwa lami

Tukiwaambia kwamba hakuna alichofanya Cha maana Mwendazake kwenye Barabara za lami wakati wa Uongozi wake muwe mnaelewa.

Imagine Hadi Leo hii huwezi fika Kigoma bila kutembea kwenye mavumbi na hali Iko hivyo kwenye Mikoa Mingi sana.

Sasa kipele kimepata mkunaji ambao km 51 zilizosalia zinaenda kukamilika kabla ya desemba 2024 hivyo Kigoma-Dar itakuwa lami.Kazi hii ya kutukuka anaifanya Rais Samia.

==============

BADO KM 51.1 KUUNGANISHA TABORA-KIGOMA KWA LAMI

IMEELEZWA kuwa bado kilomita 51.1 ili kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa barabara ya lami na hivyo kuandika historia ya aina yake nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tabora- Kigoma sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 na Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1.

“Kwa kweli nimeridhika na kasi ya ujenzi sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 99”, amesema Eng. Kasekenya.

Naibu Waziri huyo amemtaka mkandarasi STECOL Cooperation Ltd anayejenga sehemu ya Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1 kufanya kazi usiku na mchana ili kuandika historia ya kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa lami mapema iwezekanavyo.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma amesema ujenzi huo umefikia asilimia 45 na watamsimamia kikamilifu mkandarasi ili maeneo yanayoweza kuathiriwa na mvua yakamilishwe mapema ili kuepuka visingizio na kuwawezesha wasafiri na wasafirishaji wa mikoa hiyo kunufaika na barabara ya kisasa.

Zaidi ya shilingi bilioni 62.7 zinatumika katika ujenzi huo ambazo ni matapo ya ndani na mkopo nafuu kutoka mifuko ya OPEC na Abu Dhabi.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kasekenya amemtaka Mbunge wa Urambo Mhe. Margareth Sitta kuhamasisha wananchi wa jimbo hilo kulinda miundombinu inayojengwa katika jimbo hilo ikiwemo taa na alama za barabarani ili kuepusha ajali na kuendana na kasi ya Serikali ya kupendezesha barabara nchini.

“Tunawajengea barabara na mzunguko wa kisasa round about ili kupunguza ajali eneo lililokuwa na kona kali na kutengeneza taswira nzuri ya Urambo hivyo hakikisheni miundombinu hii inalindwa na kuendelezwa kwani inatumia fedha nyingi za Serikali “, amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.

Kwa upande wake Mhe. Margareth Sitta ameishukuru Serikali kwa uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya kisasa katika wilaya ya Urambo na kuahidi kutoa elimu kwa wananchi kuthamini uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ili kuchochea maendeleo ya wananchi.
Baada ya hapo ndiyo pale watu watakapokuja kugundua kuwa Kigoma ni moja ya mikoa potential na strategic iliyopo tanzania.
Kigoma ni mkoa usiokuwa na majengo ya maghorofa, ila una hali ya hewa na ardhi yenye rutuba ambayo mikoa iliyo mingi Tanzania haina.
 
Maumivu ya wivu 😂😂😂
Ni kukosa akili pekee, wakoloni waliteta shule, makanisa, misikiti, hospitali, reli, barabara, maji n.k lakini bado tuliona hawafai, tuna taka vitu vikubwa, ni aibu na ujinga leo hii nchi kuwa gizani huku mito, gas, misitu, mapori, mifugo, maziwa, bahari unavyo unazidiwa na Zambia ambao wanategemea bwawa pekee.
 
Rubbish gani Sasa,huu ndio ukweli hakuna kitu Cha maana alifanya Mwendazake kwenye Barabara Nchi hii badla yake Samia ndio ataweka historia.
Kwa kweli akili za wewe labda ni za matopeni sababu mwenye akili timamu hawezi andika huo uchafu.
 
Baada ya hapo ndiyo pale watu watakapokuja kugundua kuwa Kigoma ni moja ya mikoa potential na strategic iliyopo tanzania.
Kigoma ni mkoa usiokuwa na majengo ya maghorofa, ila una hali ya hewa na ardhi yenye rutuba ambayo mikoa iliyo mingi Tanzania haina.
Vyote vitakuja baada uchumi kufunguka maana hata umeme ni tia maji tia maji.
 
Ni kukosa akili pekee, wakoloni waliteta shule, makanisa, misikiti, hospitali, reli, barabara, maji n.k lakini bado tuliona hawafai, tuna taka vitu vikubwa, ni aibu na ujinga leo hii nchi kuwa gizani huku mito, gas, misitu, mapori, mifugo, maziwa, bahari unavyo unazidiwa na Zambia ambao wanategemea bwawa pekee.
Kama walikijengea shule Kwa nini mama Yako hakusoma?

Kama.walijenga saizi tunajenga za nini sasa?

Maumivu ya wivu 🤣🤣
 
Hoja ni vumbi na vyote vilimshinda Mwendazake na mama anaenda kufuta vumbi.
Hata kama ni uchawa kwa mama huwezi kudharau alichofanya jpm kwenye barabara kiasi hicho...
Ingawaje Kikwete set it all in motion kwenye barabara.
 
Hata kama ni uchawa kwa mama huwezi kudharau alichofanya jpm kwenye barabara kiasi hicho...
Ingawaje Kikwete set it all in motion kwenye barabara.
Hakilingani na sifa mnazompa.Samia anajenga takribani km 4,000 Kwa mpigo hizi ni Barabara kuu pekee sijazungumzia Tarura.

Nani aliwahi kujenga hivyo? Rais yupi? Ni mwendo wa facts tuu.

Mwisho bila kuongozwa Mwendazake hawezi kitu ndio maana rekodi yake kubwa ni akiwa chini ya Mkapa na JK ila alipokuwa yeye Rais hakuna Cha maana alifanya kwenye Barabara.
 
Vyote vitakuja baada uchumi kufunguka maana hata umeme ni tia maji tia maji.
Watu huwa wanai-rate Kigoma kwa kuangalia maghorofa pale mjini.
Kigoma ni mkoa mzuri mno ambao unaweza ukawa among the TOP 5 nchi hii. Subiri hii bararbara ikamilike, halafu watu watakuja kuona ndani ya miaka michache ijayo. Kigoma ina kila kitu isipokuwa maghorofa, halafu pia iko mpakani
 
Hakilingani na sifa mnazompa.Samia anajenga takribani km 4,000 Kwa mpigo hizi ni Barabara kuu pekee sijazungumzia Tarura.

Nani aliwahi kujenga hivyo? Rais yupi? Ni mwendo wa facts tuu.

Mwisho bila kuongozwa Mwendazake hawezi kitu ndio maana rekodi yake kubwa ni akiwa chini ya Mkapa na JK ila alipokuwa yeye Rais hakuna Cha maana alifanya kwenye Barabara.
Wewe taktaka hizo km zinajengwa wapi?

Njoo hapa ukonga uone kulivyochakaa
 
Hakilingani na sifa mnazompa.Samia anajenga takribani km 4,000 Kwa mpigo hizi ni Barabara kuu pekee sijazungumzia Tarura.

Nani aliwahi kujenga hivyo? Rais yupi? Ni mwendo wa facts tuu.

Mwisho bila kuongozwa Mwendazake hawezi kitu ndio maana rekodi yake kubwa ni akiwa chini ya Mkapa na JK ila alipokuwa yeye Rais hakuna Cha maana alifanya kwenye Barabara.
"Anajenga takribani km 4000"
Subiri azimalize hizo km ndo ulete uchawa.
Hizi barabara zimekuwa za kupokezana ujenzi tokea enzi za Mwinyi.Unless umeajiriwa juzi na wizara ya ujenzi/tanroads maana una vitakwimu vya afisa anayetumwa kufanya monitoring kwenye ujenzi.
 
Watu huwa wanai-rate Kigoma kwa kuangalia maghorofa pale mjini.
Kigoma ni mkoa mzuri mno ambao unaweza ukawa among the TOP 5 nchi hii. Subiri hii bararbara ikamilike, halafu watu watakuja kuona ndani ya miaka michache ijayo. Kigoma ina kila kitu isipokuwa maghorofa, halafu pia iko mpakani
Mama anaufungua Mkoa wa Kigoma kama ifuatavyo

Barabara zote za kuingia na kutoka Kigoma ziko under construction

Anajenga na kupanua Airport ya Kigoma(Gombe-Mahale International Airport) Kwa kupanua runway ,kujenga jengo la Abiria ,parking ya ndege na mnara wa kuongozea ndege ziruke usiku na mchana full taa.

Anajenga hospital ya Kanda ya Magharibi yenye hadhi ya Muhimbili

Muhimbili inayenga Branch ya Chuo Kikuu hapo

Anaipanua Bandari ya Kigoma

Anajenga meli Mpya 2 za Abiria Ziwa Tanganyika,anakafabati mv Liemba,Mt Sangara na kujenga meli Mpya za mizigo

Kuna tawi la BoT linajengwa

Kuna mradi wa grid ya Taifa wa umeme unaenda(Hapo uvinza kutajengwa substation kubwa sana itayopokea njia kubwa ya kutoka Kagera na kutoka Sumbawanga).

Hivyo ni vichache tuu kati ya vingi.
 
"Anajenga takribani km 4000"
Subiri azimalize hizo km ndo ulete uchawa.
Hizi barabara zimekuwa za kupokezana ujenzi tokea enzi za Mwinyi.Unless umeajiriwa juzi na wizara ya ujenzi/tanroads maana una vitakwimu vya afisa anayetumwa kufanya monitoring kwenye ujenzi.
Hakuna Cha uchwara ni facts tuu hata kama hutaki.Zinamalizika mwaka Hadi mwaka ndio maana ya takwimu.

Na Kwa taarifa Yako kama mama atajaaliwa Hadi kufika 2030 hakuna Kipande Cha Barabara kuu Tanzania hii litakuwa na vumbi ,kote itakuwa ni mkeka.
 
Back
Top Bottom