Bado Km 51 ili Kigoma-Dar iwe lami. Rais Samia anaenda kuunganisha mikoa yote kwa lami

Bado Km 51 ili Kigoma-Dar iwe lami. Rais Samia anaenda kuunganisha mikoa yote kwa lami

Wewe taktaka hizo km zinajengwa wapi?

Njoo hapa ukonga uone kulivyochakaa
Ukonga ndio Mkoani 😂😂😂😂

Zinajengwa kila Mkoa wa Tanzania ikiwemo huko Dar sio lazima iwe hapo Ukonga.
 
Hakuna Cha uchwara ni facts tuu hata kama hutaki.Zinamalizika mwaka Hadi mwaka ndio maana ya takwimu.

Na Kwa taarifa Yako kama mama atajaaliwa Hadi kufika 2030 hakuna Kipande Cha Barabara kuu Tanzania hii litakuwa na vumbi ,kote itakuwa ni mkeka.
We uvccm ni shida sana.
 
Utakuwa unaishi Canada.Nyie mlikuwa mnaishi Kwa propaganda za Mwendazake.

Sasa Kwa taarifa Yako Barabara zifuatazo ni vumbi tupu.

Kigoma-Tabora
Mpanda-Sumbawanga
Kigoma-Mpanda
Morogoro -Songea
Mbeya-Tabora
Mbeya-Singida
Arusha-Musoma
Arusha-Simiyu
Njombe-Morogoro via Ifakara.
Mtwara-Masasi via Tandahimba
Morogoro -Lindi
Kigoma-Kagera

Hiyo ni Baadhi tuu ya Barabara kuu za Mikoa kwa Mikoa ambazo zimejaa mavumbi au Baadhi ya vipande Bado ni mavumbi.

Wabunge wa hiyo mikoa wamekuwa na kazi gani?
 
Mama anaufungua Mkoa wa Kigoma kama ifuatavyo

Barabara zote za kuingia na kutoka Kigoma ziko under construction

Anajenga na kupanua Airport ya Kigoma(Gombe-Mahale International Airport) Kwa kupanua runway ,kujenga jengo la Abiria ,parking ya ndege na mnara wa kuongozea ndege ziruke usiku na mchana full taa.

Anajenga hospital ya Kanda ya Magharibi yenye hadhi ya Muhimbili

Muhimbili inayenga Branch ya Chuo Kikuu hapo

Anaipanua Bandari ya Kigoma

Anajenga meli Mpya 2 za Abiria Ziwa Tanganyika,anakafabati mv Liemba,Mt Sangara na kujenga meli Mpya za mizigo

Kuna tawi la BoT linajengwa

Kuna mradi wa grid ya Taifa wa umeme unaenda(Hapo uvinza kutajengwa substation kubwa sana itayopokea njia kubwa ya kutoka Kagera na kutoka Sumbawanga).

Hivyo ni vichache tuu kati ya vingi.
Na mwalimu wangu kutoka Pale TIA Dar, alishaanzisha Branch nyingine ya TIA hapo Kigoma tangu mwaka 2010 au 2011
Ukifika maeneno kama ya Mwakizega, unakuta watu wapo kijijini wanaishi kwenye Beach nzuri mno kando kando ya Ziwa Tanganyika, utadhani wako Ulaya
Kigoma ni kuzuri mno nilipapenda sana. Hatuwezi kuwa tuna-rate uzuri wa sehemu kwa kutumia uwingi wa maghrorofa yaliyopo mjini.

Huu mkoa Mungu bariki ngoja Mama aufungue halafu utaupaisha uchumi wa nchi yetu kwa kasi isiyotarajiwa; ni hakika
 
Utakuwa unaishi Canada.Nyie mlikuwa mnaishi Kwa propaganda za Mwendazake.

Sasa Kwa taarifa Yako Barabara zifuatazo ni vumbi tupu.

Kigoma-Tabora
Mpanda-Sumbawanga
Kigoma-Mpanda
Morogoro -Songea
Mbeya-Tabora
Mbeya-Singida
Arusha-Musoma
Arusha-Simiyu
Njombe-Morogoro via Ifakara.
Mtwara-Masasi via Tandahimba
Morogoro -Lindi
Kigoma-Kagera

Hiyo ni Baadhi tuu ya Barabara kuu za Mikoa kwa Mikoa ambazo zimejaa mavumbi au Baadhi ya vipande Bado ni mavumbi.
Wewe ukipata gepu piga mzee baba,hakuna kiongozi mwenye huruma na wewe mwananchi.
 
MBONA MIKOA MINGI TU. Manyara na Simiyu haijaunganishwa kwa Lami, Arusha na Simiyu haijaunganishwa na Lami, Manyara na Tanga bado, Morogoro na Ruvuma n.k
Bora Kwa Sasa Morogoro na Ruvuma Ina mkandarasi wa EPC

Manyara,Simiyu,Tanga Ina mkandarasi wa EPC +F
 
Mimi nimeishi Kigoma.Hapo naona unapiga propaganda tu.Unaweza kumulaumu JPM kwa mambo mengine lakini siyo kwa jitihada za kuboresha miundombinu ya barabara.
Hakuna kiongozi aliye boresha miundo mbinu ndani ya nchi hii kuanzia barabara ,vyanzo vya umeme , Elimu kumzidi kikwete hayo mengine ni propaganda.
 
Kazilambwa-Chagu ilikuwa na lami? Unajua kwamba Hadi anachukua kutoka Kwa JK ni km hizo hizo zilikuwa mavumbi na zilimshinda Kumalizia?
Tuambie kwa wakati wake alikuta kiasi gani na akajenga kiasi gani ila ukileta porojo wakati fika tunajua utendaji wake, utaonekana kituko tu.
 
Acha ujinga chawa wewe. Huenda ni kinda hapo mungu akusamehe. Kama zimebakia km 51 jiulize hizo zingine nani kasimamia. Jpm amekua waziri wa ujenzi miaka 20 kabla hajakua rais na yeye ndie aliyesimamia ujenzi mkubwa barabara za lami nchi hii. Alipoanza jpm ilikua kwenda mwanza toka dar lazima upite kenya na uganda. Kama unampapatikia mama kua na adabu kwa wale tunaomuenzi jpm.
Barabara zote zilizo jegwa kipindi JPM ni waziri wa ujenzi sifa zina takiwa kwenda kwa kikwete kwa sababu ndo alikuwa rais kipindi hicho.
 
Umeandika pumba na mashudu

Halafu JPM bado anawasumbua sana eeh vichwani mwenu hawatoki😁alijua kuwakomesha mpaka mnashindwa kumsahau
 
Tuambie kwa wakati wake alikuta kiasi gani na akajenga kiasi gani ila ukileta porojo wakati fika tunajua utendaji wake, utaonekana kituko tu.
Amejenga chini ya km 2500,taarifa hii utaikuta Kwenye Bunge la kufunga Bajeti
 
Hakuna kiongozi aliye boresha miundo mbinu ndani ya nchi hii kuanzia barabara ,vyanzo vya umeme , Elimu kumzidi kikwete hayo mengine ni propaganda.
Samia atafunika wote hao, wengine walikuwa wapiga propaganda
 
Tukiwaambia kwamba hakuna alichofanya Cha maana Mwendazake kwenye Barabara za lami wakati wa Uongozi wake muwe mnaelewa.

Imagine Hadi Leo hii huwezi fika Kigoma bila kutembea kwenye mavumbi na hali Iko hivyo kwenye Mikoa Mingi sana.

Sasa kipele kimepata mkunaji ambao km 51 zilizosalia zinaenda kukamilika kabla ya desemba 2024 hivyo Kigoma-Dar itakuwa lami.Kazi hii ya kutukuka anaifanya Rais Samia.

==============

BADO KM 51.1 KUUNGANISHA TABORA-KIGOMA KWA LAMI

IMEELEZWA kuwa bado kilomita 51.1 ili kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa barabara ya lami na hivyo kuandika historia ya aina yake nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tabora- Kigoma sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 na Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1.

“Kwa kweli nimeridhika na kasi ya ujenzi sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 99”, amesema Eng. Kasekenya.

Naibu Waziri huyo amemtaka mkandarasi STECOL Cooperation Ltd anayejenga sehemu ya Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1 kufanya kazi usiku na mchana ili kuandika historia ya kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa lami mapema iwezekanavyo.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma amesema ujenzi huo umefikia asilimia 45 na watamsimamia kikamilifu mkandarasi ili maeneo yanayoweza kuathiriwa na mvua yakamilishwe mapema ili kuepuka visingizio na kuwawezesha wasafiri na wasafirishaji wa mikoa hiyo kunufaika na barabara ya kisasa.

Zaidi ya shilingi bilioni 62.7 zinatumika katika ujenzi huo ambazo ni matapo ya ndani na mkopo nafuu kutoka mifuko ya OPEC na Abu Dhabi.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kasekenya amemtaka Mbunge wa Urambo Mhe. Margareth Sitta kuhamasisha wananchi wa jimbo hilo kulinda miundombinu inayojengwa katika jimbo hilo ikiwemo taa na alama za barabarani ili kuepusha ajali na kuendana na kasi ya Serikali ya kupendezesha barabara nchini.

“Tunawajengea barabara na mzunguko wa kisasa round about ili kupunguza ajali eneo lililokuwa na kona kali na kutengeneza taswira nzuri ya Urambo hivyo hakikisheni miundombinu hii inalindwa na kuendelezwa kwani inatumia fedha nyingi za Serikali “, amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.

Kwa upande wake Mhe. Margareth Sitta ameishukuru Serikali kwa uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya kisasa katika wilaya ya Urambo na kuahidi kutoa elimu kwa wananchi kuthamini uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ili kuchochea maendeleo ya wananc
Punguza uchawa. Magufuli ndo baba wa taifa katika eneo la ujenzi wa Barabara nchi hii.
 
Back
Top Bottom