Bado Km 51 ili Kigoma-Dar iwe lami. Rais Samia anaenda kuunganisha mikoa yote kwa lami

Bado Km 51 ili Kigoma-Dar iwe lami. Rais Samia anaenda kuunganisha mikoa yote kwa lami

Kwa Hiyo ukiunganisha kigoma= kuunganisha mikoa yote? Muwage na akili japo kidogo
 
Viumbe wanaoitwa wanaCCM ni watu wanafiki sana, kipindi cha Kikwete kuna mtu alitokea humu JF aliitwa Zomba alisumbua sana kwa upotoshaji, baada ya kuingia Magufuli then ID ya Zomba ikapotea.
Kipindi cha Magufuli akaibuka Msemajikweli akasumbua sana watu kwa upotoshaji.
Ameingia Samia, wameibuka akina Choice Variable wameanza upotoshaji, hua sijui wanajisikiaje wanapopotosha, je viongozi wakuu wanaposoma upotoshaji wao wanajisikiaje. Mitandao itumike kuwashauri viongozi.
 
Kipi kimepotoshwa?
 
Weka bajeti ya wizara ya pamoja na utekelezaji wake kipindi cha JPM tuone kama kweli hajafanya chochote
 
Weka bajeti ya wizara ya pamoja na utekelezaji wake kipindi cha JPM tuone kama kweli hajafanya chochote
Kuna sehemu nimesema hajafanya chochote? Bali alichofanya vs propaganda na sifa havilingani.

Kwa mda mfupi Samia has outperformed him.
 
Tukiwaambia kwamba hakuna alichofanya Cha maana Mwendazake kwenye Barabara za lami wakati wa Uongozi wake muwe mnaelewa.

Imagine Hadi Leo hii huwezi fika Kigoma bila kutembea kwenye mavumbi na hali Iko hivyo kwenye Mikoa Mingi sana.

Sasa kipele kimepata mkunaji ambao km 51 zilizosalia zinaenda kukamilika kabla ya desemba 2024 hivyo Kigoma-Dar itakuwa lami.Kazi hii ya kutukuka anaifanya Rais Samia.

==============

BADO KM 51.1 KUUNGANISHA TABORA-KIGOMA KWA LAMI

IMEELEZWA kuwa bado kilomita 51.1 ili kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa barabara ya lami na hivyo kuandika historia ya aina yake nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tabora- Kigoma sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 na Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1.

“Kwa kweli nimeridhika na kasi ya ujenzi sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 99”, amesema Eng. Kasekenya.

Naibu Waziri huyo amemtaka mkandarasi STECOL Cooperation Ltd anayejenga sehemu ya Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1 kufanya kazi usiku na mchana ili kuandika historia ya kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa lami mapema iwezekanavyo.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma amesema ujenzi huo umefikia asilimia 45 na watamsimamia kikamilifu mkandarasi ili maeneo yanayoweza kuathiriwa na mvua yakamilishwe mapema ili kuepuka visingizio na kuwawezesha wasafiri na wasafirishaji wa mikoa hiyo kunufaika na barabara ya kisasa.

Zaidi ya shilingi bilioni 62.7 zinatumika katika ujenzi huo ambazo ni matapo ya ndani na mkopo nafuu kutoka mifuko ya OPEC na Abu Dhabi.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kasekenya amemtaka Mbunge wa Urambo Mhe. Margareth Sitta kuhamasisha wananchi wa jimbo hilo kulinda miundombinu inayojengwa katika jimbo hilo ikiwemo taa na alama za barabarani ili kuepusha ajali na kuendana na kasi ya Serikali ya kupendezesha barabara nchini.

“Tunawajengea barabara na mzunguko wa kisasa round about ili kupunguza ajali eneo lililokuwa na kona kali na kutengeneza taswira nzuri ya Urambo hivyo hakikisheni miundombinu hii inalindwa na kuendelezwa kwani inatumia fedha nyingi za Serikali “, amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.

Kwa upande wake Mhe. Margareth Sitta ameishukuru Serikali kwa uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya kisasa katika wilaya ya Urambo na kuahidi kutoa elimu kwa wananchi kuthamini uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ili kuchochea maendeleo ya wananchi.
Hongera kwake Samia kwa kujitolea pesa za mshahara wake kujenga barabara ya kgm DAR, kongole kwake!!
 
Kwa taarifa tu ni kwamba hiyo barabara ilipaswa ikamilike mapema mno 2022 kama Magufuli angekuwepo, uongozi wa Samia ulaumiwe kwa uzembe mpaka sasa hiyo barabara haijakamilika.Nikiwaza safari ya kwenda nyumbani Kigoma kichwa huuma kiangazi vumbi la hatari masika tope hakuna unafuu
 
Alishindwa kukamilisha miaka mitano ndio aje kukamilisha sijui kama angekuwepo? 😁😁😁😁

Kwa taarifa tuu ni kwamba anagekuwepo hakuna hata mradi mmja wa Barabara angezindua kama alivyokuwa anazindua Barabara za JK.

Yeye angekuwa anahangaika na Sgr na vile hana hela uchumi ungeshaanguka
 
Unajua hiyo Barabara ilianza kujengwa lini?
 
Kazilambwa-Chagu ilikuwa na lami? Unajua kwamba Hadi anachukua kutoka Kwa JK ni km hizo hizo zilikuwa mavumbi na zilimshinda Kumalizia?
usipende uongo na upotoshaji hata Kama una chuki na mtu
magufuli katika
utawala wake kwa barabara ya Tabora to Kigoma kaanzisha na Kumalizia kipande Cha Urambo to kaliua
lakini pia bc vipande
vya Chagu to kazilambea na Uvinza to Malagalasi kavianzisha na kuviacha zaidi ya asilimia hamsini
Jitahidi kuwa mkweli usipende porojo na mapambio
 
Back
Top Bottom