Bado Km 51 ili Kigoma-Dar iwe lami. Rais Samia anaenda kuunganisha mikoa yote kwa lami

usipende uongo na upotoshaji hata Kama una chuki na mtu
magufuli katika
utawala wake kwa barabara ya Tabora to Kigoma kaanzisha na Kumalizia kipande Cha Urambo to kaliua
lakini pia bc vipande
vya Chagu to kazilambea na Uvinza to Malagalasi kavianzisha na kuviacha zaidi ya asilimia hamsini
Jitahidi kuwa mkweli usipende porojo na mapambio
Barabara imeanza kujengwa chini ya JK kuanzia Manyoni kwenda Tabora na pia kutoka Kigoma Hadi Uvinza plus Malagarasi bridge na Barabara zake alijenga JK.

Kwa hiyo hapo nani alianzisha? Kwa nini hakukamilisha kwa miaka 6?
 
Tukiwaambia kwamba hakuna alichofanya Cha maana Mwendazake kwenye Barabara za lami wakati wa Uongozi wake muwe mnaelewa.

Imagine Hadi Leo hii huwezi fika Kigoma bila kutembea kwenye mavumbi na hali Iko hivyo kwenye Mikoa Mingi sana.

Sasa kipele kimepata mkunaji ambao km 51 zilizosalia zinaenda kukamilika kabla ya desemba 2024 hivyo Kigoma-Dar itakuwa lami.Kazi hii ya kutukuka anaifanya Rais Samia.

==============

BADO KM 51.1 KUUNGANISHA TABORA-KIGOMA KWA LAMI

IMEELEZWA kuwa bado kilomita 51.1 ili kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa barabara ya lami na hivyo kuandika historia ya aina yake nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tabora- Kigoma sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 na Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1.

“Kwa kweli nimeridhika na kasi ya ujenzi sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 99”, amesema Eng. Kasekenya.

Naibu Waziri huyo amemtaka mkandarasi STECOL Cooperation Ltd anayejenga sehemu ya Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1 kufanya kazi usiku na mchana ili kuandika historia ya kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa lami mapema iwezekanavyo.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma amesema ujenzi huo umefikia asilimia 45 na watamsimamia kikamilifu mkandarasi ili maeneo yanayoweza kuathiriwa na mvua yakamilishwe mapema ili kuepuka visingizio na kuwawezesha wasafiri na wasafirishaji wa mikoa hiyo kunufaika na barabara ya kisasa.

Zaidi ya shilingi bilioni 62.7 zinatumika katika ujenzi huo ambazo ni matapo ya ndani na mkopo nafuu kutoka mifuko ya OPEC na Abu Dhabi.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kasekenya amemtaka Mbunge wa Urambo Mhe. Margareth Sitta kuhamasisha wananchi wa jimbo hilo kulinda miundombinu inayojengwa katika jimbo hilo ikiwemo taa na alama za barabarani ili kuepusha ajali na kuendana na kasi ya Serikali ya kupendezesha barabara nchini.

“Tunawajengea barabara na mzunguko wa kisasa round about ili kupunguza ajali eneo lililokuwa na kona kali na kutengeneza taswira nzuri ya Urambo hivyo hakikisheni miundombinu hii inalindwa na kuendelezwa kwani inatumia fedha nyingi za Serikali “, amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.

Kwa upande wake Mhe. Margareth Sitta ameishukuru Serikali kwa uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya kisasa katika wilaya ya Urambo na kuahidi kutoa elimu kwa wananchi kuthamini uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ili kuchochea maendeleo ya wananchi.
Una undugu na Lucas Mwashambwa?
 
Barabara imeanza kujengwa chini ya JK kuanzia Manyoni kwenda Tabora na pia kutoka Kigoma Hadi Uvinza plus Malagarasi bridge na Barabara zake alijenga JK.

Kwa hiyo hapo nani alianzisha? Kwa nini hakukamilisha kwa miaka 6?
mm nimekutajia
vipande alivyoanzisha na kuvijenga na
sio barabara yote mbona una uelewa mdogo hivyo
 
Utakuwa unaishi Canada.Nyie mlikuwa mnaishi Kwa propaganda za Mwendazake.

Sasa Kwa taarifa Yako Barabara zifuatazo ni vumbi tupu.

Kigoma-Tabora
Mpanda-Sumbawanga
Kigoma-Mpanda
Morogoro -Songea
Mbeya-Tabora
Mbeya-Singida
Arusha-Musoma
Arusha-Simiyu
Njombe-Morogoro via Ifakara.
Mtwara-Masasi via Tandahimba
Morogoro -Lindi
Kigoma-Kagera

Hiyo ni Baadhi tuu ya Barabara kuu za Mikoa kwa Mikoa ambazo zimejaa mavumbi au Baadhi ya vipande Bado ni mavumbi.
Kumbe unaweza kutoka Moro hadi Njombe kupitia Ifakara. Hii sikuijua.
 
Wakimalizie na kile kipande cha Nyakanazi-Kigoma ili mkeka ukamilike Mashariki hadi Magharibi mkeka.
 
Rubbish gani Sasa,huu ndio ukweli hakuna kitu Cha maana alifanya Mwendazake kwenye Barabara Nchi hii badla yake Samia ndio ataweka historia.
Yaan ujinga ni janga aisee barabara hizi zimeanzakujengwa miaka 60 ,Leo anayemaizia Ndio mnamsifia ....!
 
Utakuwa unaishi Canada.Nyie mlikuwa mnaishi Kwa propaganda za Mwendazake.

Sasa Kwa taarifa Yako Barabara zifuatazo ni vumbi tupu.

Kigoma-Tabora
Mpanda-Sumbawanga
Kigoma-Mpanda
Morogoro -Songea
Mbeya-Tabora
Mbeya-Singida
Arusha-Musoma
Arusha-Simiyu
Njombe-Morogoro via Ifakara.
Mtwara-Masasi via Tandahimba
Morogoro -Lindi
Kigoma-Kagera

Hiyo ni Baadhi tuu ya Barabara kuu za Mikoa kwa Mikoa ambazo zimejaa mavumbi au Baadhi ya vipande Bado ni mavumbi.
Sumbawanga-katavi tayari mkuu kilibakia kipande Cha hifadhi kl 70 ambazo tayari mkandarasi yupo barabarani.na katavi kigoma Kuna kilomita 50 mkandarasi anachapa kazi mama yupo kazini

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hoja Iko pale pale,Barabara alizozikuta Mwendazake Zina vumbi aliziacha vile vile hadi Sasa ambapo mama anazijenga.

Mwisho hiyo section ya kibaoni-Sitalike Ina km zaidi ya 85
 
Hata Samia ataondoka na kuziacha barabara zisizo na lami, huu ndio ukweli.
 
Tunazungumzia Barabara Kuu,hizo zote ataziweka lami zitasalia Barabara za Mikoa tuu.

Kufika 2030 hakuna Barabara kuu itakuwa na vumbi Tanzania hii.
 
Tukiwaambia kwamba hakuna alichofanya Cha maana Mwendazake kwenye Barabara za lami wakati wa Uongozi wake muwe mnaelewa.

Imagine Hadi Leo hii huwezi fika Kigoma bila kutembea kwenye mavumbi na hali Iko hivyo kwenye Mikoa Mingi sana.

Sasa kipele kimepata mkunaji ambao km 51 zilizosalia zinaenda kukamilika kabla ya desemba 2024 hivyo Kigoma-Dar itakuwa lami.Kazi hii ya kutukuka anaifanya Rais Samia.

==============

BADO KM 51.1 KUUNGANISHA TABORA-KIGOMA KWA LAMI

IMEELEZWA kuwa bado kilomita 51.1 ili kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa barabara ya lami na hivyo kuandika historia ya aina yake nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tabora- Kigoma sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 na Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1.

“Kwa kweli nimeridhika na kasi ya ujenzi sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 99”, amesema Eng. Kasekenya.

Naibu Waziri huyo amemtaka mkandarasi STECOL Cooperation Ltd anayejenga sehemu ya Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1 kufanya kazi usiku na mchana ili kuandika historia ya kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa lami mapema iwezekanavyo.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma amesema ujenzi huo umefikia asilimia 45 na watamsimamia kikamilifu mkandarasi ili maeneo yanayoweza kuathiriwa na mvua yakamilishwe mapema ili kuepuka visingizio na kuwawezesha wasafiri na wasafirishaji wa mikoa hiyo kunufaika na barabara ya kisasa.

Zaidi ya shilingi bilioni 62.7 zinatumika katika ujenzi huo ambazo ni matapo ya ndani na mkopo nafuu kutoka mifuko ya OPEC na Abu Dhabi.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kasekenya amemtaka Mbunge wa Urambo Mhe. Margareth Sitta kuhamasisha wananchi wa jimbo hilo kulinda miundombinu inayojengwa katika jimbo hilo ikiwemo taa na alama za barabarani ili kuepusha ajali na kuendana na kasi ya Serikali ya kupendezesha barabara nchini.

“Tunawajengea barabara na mzunguko wa kisasa round about ili kupunguza ajali eneo lililokuwa na kona kali na kutengeneza taswira nzuri ya Urambo hivyo hakikisheni miundombinu hii inalindwa na kuendelezwa kwani inatumia fedha nyingi za Serikali “, amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.

Kwa upande wake Mhe. Margareth Sitta ameishukuru Serikali kwa uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya kisasa katika wilaya ya Urambo na kuahidi kutoa elimu kwa wananchi kuthamini uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ili kuchochea maendeleo ya wananchi.

Baaba ya miaka 60! tuna kazi. Hivi tujiulize tumefikaje miaka 60 !!
 
Back
Top Bottom