Bado Km 51 ili Kigoma-Dar iwe lami. Rais Samia anaenda kuunganisha mikoa yote kwa lami

Kwa Hiyo ukiunganisha kigoma= kuunganisha mikoa yote? Muwage na akili japo kidogo
 
Viumbe wanaoitwa wanaCCM ni watu wanafiki sana, kipindi cha Kikwete kuna mtu alitokea humu JF aliitwa Zomba alisumbua sana kwa upotoshaji, baada ya kuingia Magufuli then ID ya Zomba ikapotea.
Kipindi cha Magufuli akaibuka Msemajikweli akasumbua sana watu kwa upotoshaji.
Ameingia Samia, wameibuka akina Choice Variable wameanza upotoshaji, hua sijui wanajisikiaje wanapopotosha, je viongozi wakuu wanaposoma upotoshaji wao wanajisikiaje. Mitandao itumike kuwashauri viongozi.
 
Kipi kimepotoshwa?
 
Weka bajeti ya wizara ya pamoja na utekelezaji wake kipindi cha JPM tuone kama kweli hajafanya chochote
 
Weka bajeti ya wizara ya pamoja na utekelezaji wake kipindi cha JPM tuone kama kweli hajafanya chochote
Kuna sehemu nimesema hajafanya chochote? Bali alichofanya vs propaganda na sifa havilingani.

Kwa mda mfupi Samia has outperformed him.
 
Hongera kwake Samia kwa kujitolea pesa za mshahara wake kujenga barabara ya kgm DAR, kongole kwake!!
 
Kwa taarifa tu ni kwamba hiyo barabara ilipaswa ikamilike mapema mno 2022 kama Magufuli angekuwepo, uongozi wa Samia ulaumiwe kwa uzembe mpaka sasa hiyo barabara haijakamilika.Nikiwaza safari ya kwenda nyumbani Kigoma kichwa huuma kiangazi vumbi la hatari masika tope hakuna unafuu
 
Alishindwa kukamilisha miaka mitano ndio aje kukamilisha sijui kama angekuwepo? 😁😁😁😁

Kwa taarifa tuu ni kwamba anagekuwepo hakuna hata mradi mmja wa Barabara angezindua kama alivyokuwa anazindua Barabara za JK.

Yeye angekuwa anahangaika na Sgr na vile hana hela uchumi ungeshaanguka
 
Unajua hiyo Barabara ilianza kujengwa lini?
 
Kazilambwa-Chagu ilikuwa na lami? Unajua kwamba Hadi anachukua kutoka Kwa JK ni km hizo hizo zilikuwa mavumbi na zilimshinda Kumalizia?
usipende uongo na upotoshaji hata Kama una chuki na mtu
magufuli katika
utawala wake kwa barabara ya Tabora to Kigoma kaanzisha na Kumalizia kipande Cha Urambo to kaliua
lakini pia bc vipande
vya Chagu to kazilambea na Uvinza to Malagalasi kavianzisha na kuviacha zaidi ya asilimia hamsini
Jitahidi kuwa mkweli usipende porojo na mapambio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…