ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
- Thread starter
-
- #161
Barabara imeanza kujengwa chini ya JK kuanzia Manyoni kwenda Tabora na pia kutoka Kigoma Hadi Uvinza plus Malagarasi bridge na Barabara zake alijenga JK.usipende uongo na upotoshaji hata Kama una chuki na mtu
magufuli katika
utawala wake kwa barabara ya Tabora to Kigoma kaanzisha na Kumalizia kipande Cha Urambo to kaliua
lakini pia bc vipande
vya Chagu to kazilambea na Uvinza to Malagalasi kavianzisha na kuviacha zaidi ya asilimia hamsini
Jitahidi kuwa mkweli usipende porojo na mapambio
Una undugu na Lucas Mwashambwa?Tukiwaambia kwamba hakuna alichofanya Cha maana Mwendazake kwenye Barabara za lami wakati wa Uongozi wake muwe mnaelewa.
Imagine Hadi Leo hii huwezi fika Kigoma bila kutembea kwenye mavumbi na hali Iko hivyo kwenye Mikoa Mingi sana.
Sasa kipele kimepata mkunaji ambao km 51 zilizosalia zinaenda kukamilika kabla ya desemba 2024 hivyo Kigoma-Dar itakuwa lami.Kazi hii ya kutukuka anaifanya Rais Samia.
==============
BADO KM 51.1 KUUNGANISHA TABORA-KIGOMA KWA LAMI
IMEELEZWA kuwa bado kilomita 51.1 ili kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa barabara ya lami na hivyo kuandika historia ya aina yake nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tabora- Kigoma sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 na Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1.
“Kwa kweli nimeridhika na kasi ya ujenzi sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 99”, amesema Eng. Kasekenya.
Naibu Waziri huyo amemtaka mkandarasi STECOL Cooperation Ltd anayejenga sehemu ya Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1 kufanya kazi usiku na mchana ili kuandika historia ya kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa lami mapema iwezekanavyo.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma amesema ujenzi huo umefikia asilimia 45 na watamsimamia kikamilifu mkandarasi ili maeneo yanayoweza kuathiriwa na mvua yakamilishwe mapema ili kuepuka visingizio na kuwawezesha wasafiri na wasafirishaji wa mikoa hiyo kunufaika na barabara ya kisasa.
Zaidi ya shilingi bilioni 62.7 zinatumika katika ujenzi huo ambazo ni matapo ya ndani na mkopo nafuu kutoka mifuko ya OPEC na Abu Dhabi.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kasekenya amemtaka Mbunge wa Urambo Mhe. Margareth Sitta kuhamasisha wananchi wa jimbo hilo kulinda miundombinu inayojengwa katika jimbo hilo ikiwemo taa na alama za barabarani ili kuepusha ajali na kuendana na kasi ya Serikali ya kupendezesha barabara nchini.
“Tunawajengea barabara na mzunguko wa kisasa round about ili kupunguza ajali eneo lililokuwa na kona kali na kutengeneza taswira nzuri ya Urambo hivyo hakikisheni miundombinu hii inalindwa na kuendelezwa kwani inatumia fedha nyingi za Serikali “, amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.
Kwa upande wake Mhe. Margareth Sitta ameishukuru Serikali kwa uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya kisasa katika wilaya ya Urambo na kuahidi kutoa elimu kwa wananchi kuthamini uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ili kuchochea maendeleo ya wananchi.
HapanaUna undugu na Lucas Mwashambwa?
mm nimekutajiaBarabara imeanza kujengwa chini ya JK kuanzia Manyoni kwenda Tabora na pia kutoka Kigoma Hadi Uvinza plus Malagarasi bridge na Barabara zake alijenga JK.
Kwa hiyo hapo nani alianzisha? Kwa nini hakukamilisha kwa miaka 6?
Kumbe unaweza kutoka Moro hadi Njombe kupitia Ifakara. Hii sikuijua.Utakuwa unaishi Canada.Nyie mlikuwa mnaishi Kwa propaganda za Mwendazake.
Sasa Kwa taarifa Yako Barabara zifuatazo ni vumbi tupu.
Kigoma-Tabora
Mpanda-Sumbawanga
Kigoma-Mpanda
Morogoro -Songea
Mbeya-Tabora
Mbeya-Singida
Arusha-Musoma
Arusha-Simiyu
Njombe-Morogoro via Ifakara.
Mtwara-Masasi via Tandahimba
Morogoro -Lindi
Kigoma-Kagera
Hiyo ni Baadhi tuu ya Barabara kuu za Mikoa kwa Mikoa ambazo zimejaa mavumbi au Baadhi ya vipande Bado ni mavumbi.
Ndio MkuuKumbe unaweza kutoka Moro hadi Njombe kupitia Ifakara. Hii sikuijua.
Sasa kama Barabara ilishaanza kujengwa Kwa nini hakumalizia? Sifa zote kwa Samia.mm nimekutajia
vipande alivyoanzisha na kuvijenga na
sio barabara yote mbona una uelewa mdogo hivyo
ndio nimetoka kuangalia kwenye google map hapa sikujua aisee. Hii nchi kubwa sana.Ndio Mkuu
Yaan ujinga ni janga aisee barabara hizi zimeanzakujengwa miaka 60 ,Leo anayemaizia Ndio mnamsifia ....!Rubbish gani Sasa,huu ndio ukweli hakuna kitu Cha maana alifanya Mwendazake kwenye Barabara Nchi hii badla yake Samia ndio ataweka historia.
Siku zote anaemalizia ndio husifiwaYaan ujinga ni janga aisee barabara hizi zimeanzakujengwa miaka 60 ,Leo anayemaizia Ndio mnamsifia ....!
Subutuuu....!Hongera kwake Samia kwa kujitolea pesa za mshahara wake kujenga barabara ya kgm DAR, kongole kwake!!
Sumbawanga-katavi tayari mkuu kilibakia kipande Cha hifadhi kl 70 ambazo tayari mkandarasi yupo barabarani.na katavi kigoma Kuna kilomita 50 mkandarasi anachapa kazi mama yupo kaziniUtakuwa unaishi Canada.Nyie mlikuwa mnaishi Kwa propaganda za Mwendazake.
Sasa Kwa taarifa Yako Barabara zifuatazo ni vumbi tupu.
Kigoma-Tabora
Mpanda-Sumbawanga
Kigoma-Mpanda
Morogoro -Songea
Mbeya-Tabora
Mbeya-Singida
Arusha-Musoma
Arusha-Simiyu
Njombe-Morogoro via Ifakara.
Mtwara-Masasi via Tandahimba
Morogoro -Lindi
Kigoma-Kagera
Hiyo ni Baadhi tuu ya Barabara kuu za Mikoa kwa Mikoa ambazo zimejaa mavumbi au Baadhi ya vipande Bado ni mavumbi.
Hoja Iko pale pale,Barabara alizozikuta Mwendazake Zina vumbi aliziacha vile vile hadi Sasa ambapo mama anazijenga.Sumbawanga-katavi tayari mkuu kilibakia kipande Cha hifadhi kl 70 ambazo tayari mkandarasi yupo barabarani.na katavi kigoma Kuna kilomita 50 mkandarasi anachapa kazi mama yupo kazini
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hata Samia ataondoka na kuziacha barabara zisizo na lami, huu ndio ukweli.Hoja Iko pale pale,Barabara alizozikuta Mwendazake Zina vumbi aliziacha vile vile hadi Sasa ambapo mama anazijenga.
Mwisho hiyo section ya kibaoni-Sitalike Ina km zaidi ya 85
Tunazungumzia Barabara Kuu,hizo zote ataziweka lami zitasalia Barabara za Mikoa tuu.Hata Samia ataondoka na kuziacha barabara zisizo na lami, huu ndio ukweli.
Koo zipi hizo?Wewe unaona hicho ndicho cha maana sana! Kwa ujinga huu ndio unatufanya tutawaliwe na koo kumi miaka nenda miaka rudi, wenzetu wanaendelea sisi tumebaki kuhesabu kilomita za lami!
Kwenye lile Pori la Ndorobo.Mwisho hiyo section ya kibaoni-Sitalike Ina km zaidi ya 85
Tukiwaambia kwamba hakuna alichofanya Cha maana Mwendazake kwenye Barabara za lami wakati wa Uongozi wake muwe mnaelewa.