Wanabodi,
Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala za Kwa Maslahi ya Taifa, leo ni swali tuu kuhusu hiki Chuma kipya.
Baada ya mtu kupelekewa moto na akaachia ngazi mwenyewe, bado kuna ubishi kuwa hili ingizo jipya ni chuma cha ukweli kama chuma cha Mjerumani?. Je chuma hiki ni chuma kipya kingine ila ni kinafana tuu kama kile chuma au chuma hiki ni chuma kile kile kimerejea kivingine?!
Hili ni bandiko la dhana tuu ya kufikirika, yaani an hypothetical situation ya just thinking aloud by imaginations.
Naomba nianze na hadithi hii fupi.
Japo Mungu ni mmoja na ndie aliyeumba ulimwengu na kila kilichomo!,
Ila wakati anaamua kumuumba binadamu, kuna viumbe Mungu alisemezana navyo " Na tuumbe binadamu kwa mfano wetu" hii maana yake japo Muumba ni Mungu, lakini kuna viumbe alisemezana navyo viwe ni Mwana, yaani Neno, Roho Mtakatifu na malaika, hivyo God was not alone!.
Na baada ya binadamu kumuasi Mungu kwa kutenda ile dhambi ya kumega lile tunda la mti wa katikati, Mungu alikasirika akawafukuza Adam na Hawa kutoka bustanini, ila licha ya kuwatimua, aliwaaahidi hata waacha atawatumia Mkombozi.
Huko mbinguni, inasemekana Mungu aliwauliza hao aliokuwa nao, nimtume nani aende kuookoa ulimwengu?. Ndipo Neno akajibu, "unitumie mimi Bwana". Ndipo Mungu akamtoa mwanawe mpenzi na kumtuma duniani kuja kuukomboa ulimwengu, akazaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kwake yeye Bikira Maria, akawa mwanadamu. Akasulubiwa na kuteswa kwa mamlaka ya Ponsio Pilato, akafa akazikwa, siku ya tatu, akafufuka, akapaa mbinguni, toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu, na ufalme wake hautakuwa na mwisho!.
Nikumbukwe Masiha alikuja kwa ajili ya taifa la Mungu, ila alikataliwa na wakamsulubisha, ni kwa kuteswa kwake au kwa kupigwa kwake, sisi tumeponywa!.
Hivyo ndivyo Taifa letu la Tanzania, ni taifa la Mungu. Mungu akatuletea mkombozi Nyerere, akamtwaa!.
Taifa likayumba rumba, tukamlilia Mungu atuletee mkombozi mwingine, Baba Mungu akakisikia kilio chetu akatupatia Magufuli.
Akamtwaa na kumchukua kwake mbinguni, Mungu akatuletea Samia. Magufuli alikuwa chuma na alitawala taifa hili kwa mkono wa chuma, hivyo JPM alikuwa ni chuma!.
Tuambizaze ukweli, Rais Samia sio chuma, ila ana jicho hilo!, linaona kila mahali na kila pahali!. Sasa ili mambo yaende, hili taifa linahitaji chuma cha kulikimbiza mchaka mchaka!. Jicho la Mama Samia lika kispoti chuma fulani kikiwa kipo tuu!, Samia akakisajili na kukiita kumsaidia, na kusema ukweli kilikuja moto, kwa mwendo wa mchamchaka, alianza kuwakimbiza kwa kuanza na kinara wao kwa kupewa ultimatum!, kisha mawaziri na watendaji.
Mara yakaibuka mayowe kila kona!.
Ndani ya CCM pia kuna baadhi ya makapi yalikuwa yamedanda, na kujishikiza kwa kujibananisha kama kuna!, baada ya chuma kuingia baadhi ya makapi haya yakaanza kuishiwa nguvu, yakaanza kushindwa na kulegea!, baadhi yao wameanza kuachia ngazi mwenyewe kwa kutafuta visingizio!.
Ni baada ya makapi haya kuanza kuachia ngazi, ndio sasa macho yangu yameanza kufunuka na kuona kwa hakika hakuna ubishi kuwa hiki ni chuma!. Swali ni, je chuma hiki ni chuma kingine ila ni kinafanana kama kile chuma, au chuma hiki ni chuma kilekile kimerejea kivingine?, ili kuja kuikamilisha kazi ya ukombozi mpya wa taifa letu!.
Ili kujua kama hiki ni chuma kile kile au ni chuma kipya karibu mitaa hii
Nikimwangalia Makonda, mambo anayoyafanya namuona kama Magufuli
Nawatakia Ijumaa Kareem
Paskali.